Habari zenu wanajamvi popote pale mlipo, Hoja yangu leo ni huu mtandao wa vodacom (Vodacom Tanzania). Mimi ni mteja wa mtandao huu wa vodaCOM toka muda mrefu sana nimekua nikiupenda sana kutokana na huduma zake za internet lakin sasa hiv nadirik kusema ipo siku nitauchukia kutokana na huduma zake. Vodacom Internet kwa sasa imekuwa kero sana kwangu yaan toka week mbili zilizopita napata shida nikijiunga na vifurushi vya internet kwa ajili ya kazi zangu pamoja na kudownload documentaries, movies na mambo mengine mtandao umekuwa slow sana unakuta speed iko chini ya 20kb/sec kila siku, nikajua labda ni kutokana na eneo nililopo labda kwamba ni bondeni au labda mida ya mchana watu wapo wengi sana wanaotumia so nikawa nakaa had saa saba usiku ili speed iongezeke but speed haiongezeki. Nikaona isiwe tabu nijaribu mtandao mwingine nikakuta hali ni tofauti kabisa speed ni 150 - 200 kb/sec, leo nimejiunga tena imebidi nije nifanyie kaz zangu posta but sioni mabadiliko yoyote hali ni ile ile 20kb/sec sasa nashindwa mim kuwaelewa hawa Vodacom Tanzania kwa huduma zao.
Ushauri wangu kwa Vodacom Tanzania ongezeni bandwidth za mtandao wenu ili muweze kunishawishi nijiunge na vifurushi vyenu. "WATEJA WANAVYOONGEZEKA ONGEZENI NA HUDUMA ZENU VODACOM TANZANIA"