Habari ndugu mteja, tafadhali tunaomba namba yako kwa mawasiliano zaidi kuhusu hili.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ukijiunga na kifurushi cha Tsh 495 dakika 30 cha ajabu ukitumia dakika 1 na sekunde 1 kisha ukiangalia salio la dakika na sekunde wanakuambia umetumia dakika 2 yaani umebakiza dakika 28, vivyo hivyo ata vifurushi vingine vya Tsh 250, Tsh 645, Tsh 995, Vodacom Tanzania WIZI MTUPU.
Hilo tatizo la kukuta salio limeyeyuka kinyemela pasipo kujua, kuwa na salio la kutosha kujiunga kufurushi unachohitaji lakini unaambiwa huna salio la kutosha sio la mmoja hata mimi limeshawahi kunitokea mara kadhaa, sasa nyie vodacom tz mkikimbiwa na wateja kutafuta nani mchawa wapeni wateja majibu na ufafanuzi unajitosheleza juu ya malalamiko yao, sio kuomba namba ya simu ya mteje
Ukiwa unaingiza vocha hakikisha unazima data connection
Tafadhali piga *149*01# chagua Simu.tv kisha chagua stesheni uliyojiunga nayo halafu chagua kujiondoa. AhsanteNataka nijiondoe na simu tv, nafanyaje? Vodacom Tanzania
Mnamsaidiaje mtu alie vijini mfano malinyi hakuna huduma za voda shop! nimeibiwa simu nimeomba msaada kua nikombali naomba muiblock simu isitumike tena mmeshindwa wakat nimewapa imei no za simu na anaye tumia nimewapa kwan simu imesetiwa kila unapotoa line mwenye simu anapata ujumbe kama simu yake inatumika!hakuna technologia ya kuziunguza simu za wizi?
Tafadhali piga *149*01# chagua Simu.tv kisha chagua stesheni uliyojiunga nayo halafu chagua kujiondoa. Ahsante
Wezi wakubwa nyie, nimeenda Dukan kwenu pale mwanza mnaniuzia modem tsh 30000 ? Alafu naona tangazo kumbe ni 25000, sasa familia yangu nahama nayo, umezidi uwizi kuanzia kwenye bundle zenu hadi m pesa
nilisajili laini yangu ya voda. nikaitumia miezi kadhaa, nikasafiri kama miezi 3 nje ya nchi. niliporudi ,laini kapewa mtu mwingine ,mnaboa
nilipeleka simu mlimani city vodacom. ilikuwa haitoi sauti , week nzima ikaisha nilipowafata na mikaratasi yangu ya warranty ,daah nilichoka yaani kumbe hata kazi haijafanyiwa bali ni story tu.