Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom mmeshindwa sehemu nyingi sana,mimi nimewahi kununua luku kwa mpesa wakakaa siku 3 ndio wanakutumia umeme na hii imekuwa zaidi ya mara mbili, na hata leo hii pia nimenunua luku nimeshakaa zaidi ya masaa matatu hawajaniletea majibu ila ela wamekata, mkae mkijua kwamba mtu anaponunua kitu anakuwa na shida nayo kwa mda huo sio kwamba apate kwa mda mnaojisikia nyinyi. biashara hii imewashinda waachieni wanaoweza hapa nawaza kutupa laini yenu tu.wezi nyie wakubwa
 
Vodacom mmeniangusha sana kwenye upande wa data...ukijiunga na kifurushi cha data, unapata taarifa kuwa kifurushi kimekwisha baada ya kutumia pesa yote kwenye account.

Airtel wenzenu wanatuma msg unapofikia mwisho wa kutumia. Naamini nyie mmeondoa hiyo facility maksudi kabisa. Msiporekebisha hili tutaandamana kwa regulator- TCRA
 
Sasa ni dhahili mawasiliano na mazungumzo ya wateja wa vodacom ambao ni wanasiasa wenye mtizamo usio endana na chadema mawasiliano yao yapo hatarini kufuatiliwa kwa vile imeshajulikana wazi kuwa Salim Mwalimu ndie alikua anaiba mazungumzo hayo na kupeleka chadema!
 

Habari kamanyora, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza tunaimani umekwishapokea token zako kwa sasa. Pole sana
 
Last edited by a moderator:

Habari DuppyConqueror tafadhali tunaomba ututumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Kero yako tumeisikia kesho tutamfukuza kazi.
 
vodacom sasa nashangaa mmepotea kwenye intanet.mimi nipo morogoro mjini,intanet ipo slow sana huku.si tatizo langu tu.sasa sijaelewa kwanini.hili tatizo limeanza mwezi huu tu
 

Na wanaoenda jela mwaka mmoja mnafanyaje kuwasadia???

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Nimetumiwa text msg jana ndio nimeipata sasa hivi na taarifa zilizokusudiwa kunifikia ni irellevant saa hizi hili mnaliongeleaje? Na hata msg niliyojibu bado haijamfikia mlengwa mpaka tukapigiana simu.

Sihitaji tena huduma ya text msg ni upuuzi mtupu, wakati nilipokuwa mteja wa Tritel tulikuwa wateja tuna mkataba na Tritel ikitokea mtandao ndio umesababisha ukose biashara au upate hasara kulikuwa na kipengele cha kuwashtaki kudai fidia je nyinyi mna hicho kipengele?
 
Kwann speed ya intaneti ni ndogo sana????

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 


Sio fresh aisee sasa na wanafunzi wanaoenda shule miezi 5 je

Fanyeni 6 months
3 months mnaonea sana
 
mm kunakipindi nilipoteza cm nikaenda vodashop bukoba kurenew mhudumu akaniuliza pass word nikamwambia akasema pesa wamechukua nikamwambia anipe jina la aliechukua akakataa lkn ukweli walichukuwa wao voda!!

Habari Kayabwe, namba ya siri hutakiwi kumpatia mtu yeyote na hata mfanyakazi wa Vodacom akikuomba usimpatie. Tafadhali tutumie taarifa zaidi kuhusu hili nasi tutashirikiana nawe.
Tunaimani tumeelewana vyema kama ambavyo tumezungumza kwa njia ya simu, pesa yako iliibwa kabla hujafika dukani kwetu. Tafadhali zingatia kuwa namba ya siri ni siri yako. Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…