Vodacom Tanzania
Official Account
- Aug 12, 2013
- 324
- 126
- Thread starter
-
- #1,701
Jamani vodacom mimi kama mteja wenu naomba mtuwekee kifurushi kipya cha mb na sms tu kwa sisi tunaoshinda mtandaoni. Hatuna mda wa kupiga cm. Mtujali tafadhari.
See my claim of 09/10/2014, #1645 page 165/170 and 168/170 with reply
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
Hao jamaa wa mlimani city hasa wanaohusika na data ni matapeli wa hawajui kilichowaweka pale bora wasiwepo hawana msaada wowote wanakula mshahara bure
Vodacom acheni 'upumbavu', na wizi wa kila siku!
Mtu umejiunga na vifurushi vya intaneti, sms na dakika za maongezi, kisha unaweka salio halafu in less than 3hrs unaambiwa akaunti yako ina Tsh 0?!!!!
Mf. jana nilikuwa nina unlimited internet bundle of 24hs(of which i subscribed jana jioni). Leo asubuhi(19/10/2014) muda wa saa tatu nimeongeza salio la 5,000Tshs nikajiunga na kifurushi cha Tsh 899 kikiwa na muda wa maongezi(mitandao yote), sms na internet bundle. Toka nijiunge na kifurushi hicho nimepiga simu moja ya dakika moja na sekunde sita(Vodacom to Vodacom). Lakini muda wa saa tano na dk 50 (1150Hrs). nikajikuta nikiambiwa salio langu ni Tsh 0.
Nimejaribu kupiga simu huduma kwa wateja nikaambiwa na mhudumu(JINA NINALO), hakuna maelezo yeyote katika system jipige baada ya saa moja na nusu.Ambapo most likely nitakutana na mhudumu mwingine kumweleza tatizo lile lile tena.
Nahitaji Kurudishiwa fedha yangu NILIYODHULUMIWA.Then muache tabia za kijinga.
-Kama ni PM, Kuongea na huyo mhudumu nimekwishafuata utaratibu wote.
Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Mimi kwa jinsi nisivyoshughulikiwa tatizo langu hata namba wakisema nitume PM situmi maana napata mashaka hata tunaowasiliana nao hapa jukwaani labda sio wenyewe VODACOM coz nilipopiga simu kutoa matatizo ya kukatwa kifulushi changu cha mwezi mzima bila kukitumia nikaambiwa naunganishwa na watu wa makao makuu na watanipigia muda si mrefu,sasa ni wiki sijapata call yao na pesa ya kifulushi wamebeba
Mkuu, mimi ninashidwa kuelewa..ni kwamba
1. Hawajui?
2. Wanajua na kupuuza?
3. Kama wanajua na kupuuza, kwanini unafiki wa kuja kujiulizisha hapa na
kuleta thread ya kinafiki kana kwamba wanasaidia watu?
4. Wanaiba kwa maana wamefilisika?
5. Hawajafilisika ila wanakusanya(WANAIBA) kwa wateja wao kwa ajili ya
fedha za uchaguzi mwakani?
6. Wanaona hatuwezi kufanya lolote kwasababu wanahisi wana wateja wengi
kuliko Kampuni nyingine za simu au?
Mbona sehemu nyingine Vodacom Nigeria, Vodacom South Africa na hata jirani hapo Kenya hakuna usumbufu huu?
Habari Shark pesa huwekwa katika akaunti maalum, endapo una ndugu yako akaunti imefutwa mshauri afike dukani kwetu na pia kama ni mrithi pia anaweza kufika dukani kwetu na vithibitisho akiwa na namba ya mteja kwa msaada zaidi.
That is poor customer service huwezi kama mhudumu umwache mteja ana hanging bila kujua what next vodacom jipangeniiMkuu mimi nimeomba msaada, naambiwa tutafute tena baada ya saa moja na nusu!Sasa unajiuliza ndani ya muda huu yeye kama mhudumu anafanya nini? Mimi kama mteja anategemea niendelee ku_hold shida yangu kwa saa moja na nusu zaidi? Muda huo niwe ninafanya nini?
Hii tabia inakera na inakera sana.
Jana nimeweka hela Tshs 1,000 lakini nikashindwa kujiunga na kifurushi cha 800/=. Kuangalia salio lishabaki 700/= muda huo huo. Hii si haki kabisa, acheni hizo bana. Tukianzisha uzi hapa mtasema tumetmwa kuwachafua kumbe mnakera sana aisee.
Mtu unatoka kazini unapitia vocha dukani kisha unafika home unaweka haikubali< na dukani mbali huwezi kurudi tena,
mhhh ni shidaaaaa
Mkuu nafikiri huu ni utaratibu wa Vodacom. Miye mwenyewe tatizo hilo lipo kwangu yaani ukiongeza tu salio umeliwa...! Sasa hivi Voda naigopa kama ugonjwa wa ukoma.