Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Habari Franakim, tumeshawasilisha suala hili kwa mafundi wetu kwa utatuzi. Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
 
Hili la VODA KUKATAA kuweka bando ya SH 1000 (INTERNET BILA KIKOMO) WAKATI HIYO PESA IMO INASHANGAZA KWELI
Habari Gamba, hili hutokea endapo mteja ametumia Intaneti bila kuwa na kifurushi na ameacha pages ziko wazi kisha anajaribu kujiunga na kifurushi, katika hali hii inakuwa kwamba simu inasync mtandaoni hivyo salio hilo hilo haliwezi kukubali kujiunga. Anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha amefunga pages zote au kufunga huduma za Intaneti ''Mobile Data'' ajiunge kisha afungue baada ya kununua kifurushi. Ahsante
 
Vodacom Tanzania kama mtu ameweka mia tano kwenye simu ikatokea kwamba hiyo miatano amekwata bila yeye kuitumia je? hiyo hela hurundishwa.

asanten san
 
Last edited by a moderator:
kwanini kuunga kifurushi cha mitandao yote kinasumbua sana hata kams salio lipo utaambiwa halipo hivi kweli mmejipanga kweli .
 
Habari Franakim, tumeshawasilisha suala hili kwa mafundi wetu kwa utatuzi. Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

mbona hapa ihanda -mbozi hatupati internet ya uhakika pia tigo wana 3g network lakin vodacomo ni edge tu hebu tusaidieni hili wateja wenu tigo wanawapiga bao.
 
Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa kujitokeza ktk jamiiforum kujua matatizo/changamoto zinazowakabili kupitia maoni yetu sisi wateja.
Nipo Rungwa, wilaya manyoni. Sisi hapa tunatumia mnara ambao ni kero kubwa sana kwa kweli. Mawasiliano hukutika na kupotea kabisa mara nyingi kipindi cha mvua. Ila tangu jana aubuhi saa 12 mawasiliano yamekatika kabisa hadi sasa hivi ninapowandikia hii taarifa. Pia hata kama mtandao upo, basi mawasiliano ni shida sana, kiasi kwamba kuelewana na unayewasiliana naye ni taabu. Tumeshazoea kuongea kwa sauti kubwa hapa Rungwa kana kwamba labda unayempigia hakusikii vizuri kwa sababu ya sauti. Tafadhali sana Vodacom makao makuu mtusaidie kutatua hili tatizo maana ndio mtandao pekee hapa kwetu. Kazi njema
 

Nimelalamika mpaka nimechoka kusema sasa basi nyie bingwa
 
tunauliza maswali hapa mnajibu baadaya mwezi hii thread si muondoe tu ijulikane kuliko ubabaishaji
 
Kwanin msiweke alert ya kumjulisha mtu kama salio limeisha??? Na msilete siasa za haiwezekan..mbona tigo wanajulisha zikiwa zimebaki 2MB!!! Au nyie mnaleta UJAMBAZI TU??
wakuwekee alert wakose kukuibia?
 
Mbona hamuweki 3g mitambo Marangu wenzetu wa tigo wanatunyanyasa sana mpaka tunawaza kununua line za tigo sasa by the way Marangu ni centre ya kitalii fanyeni mipango hiyo maisha yawe ni murua..
 
Kuna tatizo kubwa la mtandao huku chuo kikuu cha dodoma hasa college ya humanities unaweza k utuma sms asubuhi mtu akaipata kesho yake je tatizo ni nini? Tunawaomba mfike na kulitatua kwani imekua ni kero kubwa sana
 
Ile bundle ya 5gb kwa mwezi ilikua very fast and efficient. This new unlimited thing is just not working.
 
Vodacom mtandao wa kijinga sana, kuanzia tarehe 1 naanza kutumia Tigo,maana nimehitaji huduma yao ya mpawa lakini sijafanikiwa utafikiri ni maombi ya kazi, nimepiga ccare, nimeenda kny maduka yao na nimetuma shida yangu kny ukurasa wenu hp JF. Nimeamua kubwaga manyanga.
 

ref this msg
 
Nyie jirekebisjen yangu sa mmoja na dk kumi nimenunua umeme hakuna majibu y? Kkama
N km tigo unanunua umeme mesej inayorud ni token za umeme sio huu upuuz wenu wa muamala umetumw tanesko halafu baada ya wiki ndo mnarudisha hela?. Tigo ukiona habari za muamala ujue kunashida na hela inarejeshwa ili uendelee kujarib achen upuuz mnakaa na pesa yangu dakika arobain mnajua nlipoitoa rudishen nkaninue na Tigo pesa Nina mambo ya kufanya
 
Rudishen hela yangu nkatafte huduma kwingine kabla vibanda havijafungwA na Wapuuzi wenzenu tanesco hawajakata umeme nikashindwa kunyosha nguo za kaxini Masaa mawili yanakaribia ntawasue hamnipi Huduma na hela hamrudishi
 
Rudishen hela yangu nkatafte huduma kwingine kabla vibanda havijafungwA na Wapuuzi wenzenu tanesco hawajakata umeme nikashindwa kunyosha nguo za kaxini Masaa mawili yanakaribia ntawasue hamnipi Huduma na hela hamrudishi

Ha ha ha, naona wamekukwaza kweli mrembo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…