nyie vodacom ni wezi kabisa
Njoo hapa katika huu uzi utoe maelezo!https://www.jamiiforums.com/habari-...zinavyowaibia-wateja-wao-10.html#post11104195Ndugu mteja,
Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?
Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.
Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:
- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.
Karibu
Vodacom Tanzania
Njoo hapa katika huu uzi utoe maelezo!https://www.jamiiforums.com/habari-...zinavyowaibia-wateja-wao-10.html#post11104195
Simu inakuwa ipo offline na hujajiunga na huduma yoyote inayolipiwa fedha.
Unaweka salio eg TShs 1000, na kujaribu kununua bundle labda ya TShs 1000 inasema salio halitoshi.
Ukiangalia salio unakuta limepungua pengine hadi kubaki TShs 870 huku ikiendelea kupungua kadri dakika zinavyokwenda.
Kwa Voda kuwapata huduma kwa wateja ni ngumu sana.
Naomba msaada namna ya kujiepusha na dhuluma au wizi huu hasa ukizingatia laini inayotumika ni muhimu kwa shughuli zako na kuibadilisha haiwezikani.
Pia, kwa anayejua namna ya kujitoa kwenye hizi huduma sijui nipashe habari, nyimbo, alert nk ambazo huja kama kirusi.
NB:
Nawashukuru Airtel maana wao unanunua moja kwa moja bundle kutoka AirtelMoney na hivyo huwezi kwa namna yoyote kuibiwa fedha yako.