Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

nyie vodacom ni wezi kabisa

Hii inawezekana,

Ukienda kwenye Mpesa ukaomba kutumiwa mini-statement ili uangalie movement ya akaunti yako hawakupi, bali wanatoa salio (final balance) tu, kwanini watufiche?

Halafu huyu anaejibu hapa aache kutoa General Answers kwenye specific na technical problems, majibu anayoyatoa hata Mimi mtu baki ningeweza kuyatoa tu hata kama Siijui Vodacom!
 
Vodacom Tanzania!

Nataka kujua ni kwa nini mmeiondoa/ 'disable' huduma ya 'Personal Hotspot' kwa sis wateja wenu wenye sim za I phone, tena bila hata kututaarifu, adi mwezi wa September huduma hii ilikuepo nini kimetokea?

Au tufanyeje nini ili huduma hii iweze kurudi tena kwenye sim zetu?
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Njoo hapa katika huu uzi utoe maelezo!https://www.jamiiforums.com/habari-...zinavyowaibia-wateja-wao-10.html#post11104195
 
Dah! Vodacom Tanzania mmekuwa wezi wakubwa sana. Leo nilinunua line yenu mpya pale Kibo Complex. Nikajiunga unlimited bundle ya siku then nikatumia internet ndani ya saa 1 na nusu bila kuangalia video wala kudownload chochote. Nika-disconnect net na baada ya 15min narudi ku-connect dashboard inakataa, kuja kucheck salio ya bando naambiwa sina data wakati nilitumia 60MB je zingine imeenda wapi ebu acheni wezi huu na kama biashara imewashinda fungeni mtandao wenu ili Tubaki TTCL yetu
 
Last edited by a moderator:
Huduma zenu mbovu. Mnakata salio bila kutumia huduma halafu mnang'ang'aniza kukata hela. Kupiga simu huduma kwa wateja ndo majanga halafu bado mnakata hela
 
Tunashukuru kwa kutufungia 3G speed internet katika miji mbalimbali hapa Tanzania. ILA: Kero yangu kubwa ni upatikanaji wa huduma ya internet nje ya miji! Mlivofanya utaratibu wa kufunga 3G ni kama mlinyonya speed yote ya internet nje ya miji na mkapeleka mijini! Nasema hivyo kwa uchungu kwani hii ina kera sana. Mfano, Mji mdogo wa Ilula ambao upo km 45 tu kutoka manispaa ya Iringa hauna kabisa access ya internet hasa nyakati za mchana licha ya minara yenu kuwepo. Usiku ndo angalau inakuwepo kwa shida sana. Nilishawapigia simu hadi mara mbili mkasema mtashughulikia lakini hadi leo ni kimya tu! Kiukweli inakera sana!
 
Juzi nmenunua umeme kupitia Mpesa. Pesa haikutosha nikaambiwa natakiwa niongeze Pesa .ili niweze kupata umeme Kwa vile ni mwanzo wa mwezi.
Sasa tokea siku ile hadi Leo .Pesa yangu haijarudishwa . sielewi nia yenu ,maana huu ni ujinga kama Pesa haitoshi rudisha Pesa yangu. Nini maana ya biashara?. Au system yenu ni batch processing? .
 
Kweli huduma zenu ni hovyo sana..hasa katika ofisi zenu sijui sehemu nyingine ila za kule Arusha unakuta wahudumu wananuka sigara na viroba pia wamebaa vivest tu mijashoo aaagh..

Kurenew line sasa ni kichefu chefu siju nini maana ya kutumia kitambulisho...ukweli huduma yenu natumia kwa mpesa malachache sana na moderm tu sasa ka line kangu kamepotea nalazimishwa taja namba tano za mwisho...nilizopiga...line yenu ni kwa voda tu and not otherwise. Line imesajiliwa kwa kitambulisho na kurenew line hatambuo kitambulishk mwataka namba tano zitoke wapi wapuuuzi nyie sana na nimesign off huduma zenu. Jirekebisheni kwa faida ya hao walio bakia vinginevyo watakimbia pia...ooops nikisahau na zile sms zenu za january makamba haha heri sasa nimetoka huko.
 
Voda jibuni izi tuhuma zinazowahusu

Simu inakuwa ipo offline na hujajiunga na huduma yoyote inayolipiwa fedha.

Unaweka salio eg TShs 1000, na kujaribu kununua bundle labda ya TShs 1000 inasema salio halitoshi.
Ukiangalia salio unakuta limepungua pengine hadi kubaki TShs 870 huku ikiendelea kupungua kadri dakika zinavyokwenda.
Kwa Voda kuwapata huduma kwa wateja ni ngumu sana.

Naomba msaada namna ya kujiepusha na dhuluma au wizi huu hasa ukizingatia laini inayotumika ni muhimu kwa shughuli zako na kuibadilisha haiwezikani.

Pia, kwa anayejua namna ya kujitoa kwenye hizi huduma sijui nipashe habari, nyimbo, alert nk ambazo huja kama kirusi.

NB:
Nawashukuru Airtel maana wao unanunua moja kwa moja bundle kutoka AirtelMoney na hivyo huwezi kwa namna yoyote kuibiwa fedha yako.
 
Kwa yeyote ayehusika,

Mimi ni mteja wenu kwa kipindi kirefu, naishi eneo la Yombo vituka nyuma ya uwanja wa ndege. Kwa muda mrefu nimekuwa nikipata matatizo ya kukatika kwa mawasiliano nitumiapo internet, niliwahi kwenda hata mlimani city kuripoti shida yangu.

Jibu nililolipata wakati huo lilikuwa ninunue modem nyingine, ninayotumia ni ya zamani. Nikaridhika na kupata taabu hiyvo hivyo, cha ajabu mwezi uliopita nimenunua modem nyingine toka duka lenu lililopo uchumi na kuanzia j'pili tatizo lile lile limejitokeza tena.

Unaweza kufikiri ni computer, lakini computer ninayotumia ni mpya vile vile nimenunua miezi 2 tu iliyopoita.

Naomba msaada kama inawezekana, hata nilipo nimekuwa hewani kwa nusu saa tayari imeshakata mawasiliano mara 1.


Natanguliza shukrani!
 
Dah voda wanakera niliunga kifurushi cha wiki 5000 mb 300 lakin siku tatu hazijaisha no downloading now video watchng kwenye mtandao lakin wananiambia mb zako zimeisha dah
 
Hawa ni kuwahama tu nimenunua Salio toka mpesa limepotea katika mazingira tatanishi nimewapigia wakasema ngoja wacheck watanitafuta lakini hadi kimya au Serikali inahusika mbona hawalifanyii kazi na mtandao huu wanapita kila mara.
 
me binafsi hawa jamaa sita waweza kifurushi cha masaa 24 kinatumika masaa kimi tu, kidogo tigo wana unafuu
 
Wez tuuu na vbando vyenu vya kikudaaaaa customer care vischana vnaongea pumbaaa tuu hata havijielewiii mnaweka maelezo mia nane ili kula hela ya mtejaaa tuuu mnaboaaa laaaanaaaa dawa yenu inakujaaaaa nikusepaaa tuuuu
 
likosekane tatizo vodacom kivipi wakuu izo vifurushi tukijiunga hela jinsi inavo katwa inazidi kasi ya upepo kwa ujumla mnaboa mnamakato ya ajabu ajabu sana kifupi huduma zenu mbovu mnaiba sana mpaka wananchi tuna jua tunaibiwa makato ovyo ovyo uwizi huu mwisho lini?
 
Mimi sijatumia line yangu ya fodakomu miaka 2 sasa, sipo afrika kbs..je nikija bado naweza itumia tena?
 
Net zenu zinaboa sana mkishakuwa na mafanikio kampuni nyingi mnajisahau sana huduma zenu sio kama zamani
 
Back
Top Bottom