Binafsi nimewahi kutumia vodacom, tigo, airtel na zantel. Kote huko wana namna zao za kuiba ila vodacom kwa sasa inaongoza kukwapua pesa za wateja kinguvu tofauti na wengine wanaonyofoa kinyemela.
Tatizo kuu ni msimamizi wa mawasiliano ambaye ni TCRA, amewaacha wajanja watupige na tunapigika hasa bila hata msaada wowote.
Niliamua kuhama vodacom na niliahidi kuwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zangu wahame pia. Ninayo furaha kubwa kuwaambia kua ushawishi wangu umefanikiwa kwa 68% mpaka sasa toka December 2013.
Mwisho niwape pole wanaoendelea na vodacom maana ni chaguo lao kwa hiari yao. Japo huku niliko kwenye mitandao naibiwa pia lakini si kwa kasi kama ya voda. Wahudumu wa mitandao mingine wako makini na wepesi kusikiliza shida ya mteja. Jaribu huduma kwa wateja voda, oooh, kazi ni kwako.