Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Jamani hapa nilipo nacheka eti VODACOM NJOO UJIBU!

Usicheke mkuu nipo serious!! Maana kwanza hata sielewi huyu VODACOM ni Mtu binafsi au Company !!

Naona Kama wamesha vimbiwa wateja! Nakama ndivyo basi watuambie. Mie juzi tu nimepoteza simu nimeenda ku Re-new line wakaniambia after 3 hours itakuwa on Air cha ajabu mpaka mchana huu naambiwa eti kuna tatizo la Network kwenye huduma ya m-pesa ndio maana bado hawajakamilisha kuirudisha!!

Huu ni Uhujumu! Masaa almost 32?? I'm Fade Up.
 
Wapuuzi sana Vodacom, pale wanapo funga na kugawa line yako salio la M Pesa ndo chakula chao, kama Vodacom anabisha, atuambie ni wateja wangapi wamewatafuta na kuwarejeshea fedha zao.

Binafsi ninawachukia kama kinyesi kwakweli siwapendi kabisa hao wadudu, kama wagekuwa ni watu wenye kuwajali wateja wangewek utaratibu wa kuomba mawazo ya wateja kabla ya kufanya mabadiliko ya kimifumo na hasa ile inayowagusa moja kwa moja wateja.

Iliwahi nitokea LUKU mzee mambo yakagoma nikaenda TANESCO naambiwa nenda VODA nikaenda VODA nikarudishwa TANESCO alafu umeme wenyewe nilikuwa namnunulia mtu ili anirudishie maana yeye hakuwa na salio na msela hata hakutaka ku-share hasara, mpaka leo hii biashara ya kununua sijui nini kwa Mpesa hapana taka unless kama sina haraka sana naweza kufanya transaction thru Mpesa lakini kama ni issue ambayo ni planned huwa napenda huduma ambazo ni mannually
 
Pole sana kaka yaani hao ni wakuwapeleka mahakamani tu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nimeipenda sana comment yako nilishapata kuwapa mapendekezo kama hayo hayo wakanijibu wao wanafanya biashara

Makampuni haya yameingiwa na tamaa saasa hivi na hawajui wanadrain out wateja wao na kujikosesha mapato
Hoja ya Husninyo ina mashiko maana hata mie yamenikuta kwani nilikuwa nina line ambayo nilikuwa naitumia kwa ajili ya moderm, wakati mwingi nipo poli alafu mbaya zaidi mtandao wa internet huwa unashika vizuri zaidi mijini lakini mawilayani huko ita-search mpaka utakoma hivyo nikawa naitumia mara chache chache, kwa sie tunaopiga misele sana vijijini tunakuwa tuna line mitandao yote na moderm mitandao yote, ikizingua Voda unatumia mtandao mwingine mpaka kazi yako itakapoisha ndio unarudisha. Kikubwa ni kuboresha mtandao wao ili uweze kupatikana kila mahali kuanzia internet mpaka simu alafu ndio waje na habari zao hizo, Bank wenyewe hata kama una salio linasoma sifuri au negative 1000 lakini bado wanakupigia kukuuliza kulikoni ili uweze kwenda kui-activate a/c yako sembuse mitandao ya simu
 
Last edited by a moderator:
Huawei Y300 naomba anayezijua APNs kwa line ya voda anitumie au afanye screenshot atume pic
 
mimi sielewi hiyo APN ina kazi gani ktk simu. Naiona kwenye simu yangu but no idea how it works.
 
Mimi nilikuwa na namba ya voda nikaa kwa muda bila kuitumia. Nikajaribu hivi juzi nikakuta wameshaifunga na wamempa mtu mwingine nikawamaindi wakasema ukikaa zaidi ya miezi 3 wanaifunga.

Kwa vile nilikuwa nahitaji nikanunua nyingine. Hii ndio ilikuwa majanga kabisa ilikuwa ya mtu mwingine full usumbufu kupigiwa na watu msg za ajabu. Voda mjicheki bana
 
Fuata na kuweka hivi
Name: Jina lolote unalopenda kuweka (All Network)

APN: internet

Authentication type: changua PAP and CHAP

APN type: andika default

Sehemu zingine acha wazi usijaze

Nimemaliza
 
Fuata na kuweka hivi
Name: Jina lolote unalopenda kuweka (All Network)

APN: internet

Authentication type: changua PAP and CHAP

APN type: andika default

Sehemu zingine acha wazi usijaze

Nimemaliza
Check hapa Kwa picha
http://support.mobipassport.com/wp-content/uploads/2012/05/androidapndefault.png
 
kwani wamekujibu vipi baada ya kununua line mpya nyingine? labda tuanzie hapo.
 
huawei Y300 naomba anayezijua APNs kwa line ya voda anitumie au afanye screenshot atume pic
D8MzbI
 
  • Ndio
  • VPN hata katika simu waweza kutumia
  • Mfano fungua hizi site NETFLIX, VEVO , utaona kwamba hutoweza kuzitumia
  • Ila ukitumia VPN utachagua server mfano ya USA hivyo utaweza kuzitembelea na kuangalia videos kama kawaida
  • SEma OS ya simu yako ili nikupe mapendekezo ya VPN nzuli.:cool2:
Mwl.RCT na @njuwa Wamavoko wanahusika na hizo VPN

Na VPN kwenye cm inafanyaj kaz?
 
Back
Top Bottom