Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

'Umeunganishwa na huduma ya breaking news BURE kwa siku 7.Kujiondoa bonyeza 1'

Sender:NIPASHE.

Huu ndo ujumbe niliopotokea just from nowhere na nilipojaribu kujiondoa kwa kubonyeza hiyo 1naambiwa FAILED(nimerudia several times lkn IMEGOMA) na tayari nimetumiwa breaking news moja mpaka sasa.

NASEMA HIVI:
Sihitaji hizo breaking news na ninaomba mniondoe haraka,utaniunganishe bila ridhaa yangu halafu uning'ang'anie? Sio biashara kabisa na mkianza kunikata tu,NATUPA LINE MAANA HUU SIYO UTARATIBU.

Huyu 'Sender: Nipashe' kanitumia hiyo breaking news na karudia kanitumia mara 4..! Mimi sikujiunga na huduma hii na kweli ukijiondoa inagoma, au Vodacom nao wameanza!!

Habari za asubuhi. Tafadhali tunaomba namba zenu za simu kwa msaada zaidi.
 
Kifurushi cha internet bila kikomo cha week ni wizi mtupu kama inawezekana kifutwe najua kinafaida kwenu ila ni kwakuwa mnatuibia mana ukijiunga yani hata ku download picha ni ngumu, huu ni wizi na mnafanya maksudi,

Habari Jese Pinkman kifurushi hiki kinakupa uhuru wa kweli kutumia mtandaoni,tafadhali hakikisha mpangilio wa Intaneti uko sahihi au tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Tafadhalini tunaomba kifurushi cha data kikibaki walau mb 10 basi uwe alerted maana utashangaa hata kama ulikua na salio la sh 10,000 litaliwa baada ya kuisha kifurushi then ndio unapata sms kuwa huna salio
Huu ni wizi
 
Huwa nakasirika sana hebu ku weni wawazi mnatuumiza sana
 
Habari za asubuhi. Tafadhali tunaomba namba zenu za simu kwa msaada zaidi.

Nimefanikiwa kujiondoa baada ya wao kunitumia tena habari nyingine na mimi kureply kwa kuandika 1.

HATA hivyo sijapenda kabisa huu utaratibu wa kuunganishana kinyemela.
 
VODACOM hakika mnakera sana.....mimi hivi sasa ni takriban wiki tatu sasa kila nikiunga chekabombastiki ambayo inajumuisha kifurushi na internet,huwa siambulii kitu katika kuzifaidi MBs zangu kabisaa(yaani net inakuwa veeery slow).Nimejaribu kupiga simu customer care maneno maneno mengiii ooooh tunakutumia configuration setting nyingine na tatizo litakwisha lakini wapi.Mbona hapo nyuma nilikuwa na browse net vizuri tu.SHIDA NI NINI HEBU NIWEKENI WAZI MAANA MBs zangu huwa zinapotea bure tu mpaka nitoe kadi niweke kwenye modem ndio walau nazifaidi.

NJOONI MNIJIBU HUKU MAANA MIMI HUU NAONA NI WIZI TU!
 
Tafadhalini tunaomba kifurushi cha data kikibaki walau mb 10 basi uwe alerted maana utashangaa hata kama ulikua na salio la sh 10,000 litaliwa baada ya kuisha kifurushi then ndio unapata sms kuwa huna salio
Huu ni wizi
Habari, ujumbe wa kufahamisha kuwa kifurushi kimekwisha unatumwa ndugu mteja, pia tunakushauri kuangalia salio la kifurushi kadri unavyoweza kulingana na matumizi, hii itakusaidia kupunguza matumizi ya Intaneti pindi kifurushi kinapokaribia kuisha. Ahsante
 
Nimefanikiwa kujiondoa baada ya wao kunitumia tena habari nyingine na mimi kureply kwa kuandika 1.

HATA hivyo sijapenda kabisa huu utaratibu wa kuunganishana kinyemela.
Huduma iliunganishwa kwa muda wa siku 7 bure na mteja anaweza kujiondoa endapo haihitaji huduma hiyo kama ambavyo umeweza kujiondoa. Pole
 
VODACOM hakika mnakera sana.....mimi hivi sasa ni takriban wiki tatu sasa kila nikiunga chekabombastiki ambayo inajumuisha kifurushi na internet,huwa siambulii kitu katika kuzifaidi MBs zangu kabisaa(yaani net inakuwa veeery slow).Nimejaribu kupiga simu customer care maneno maneno mengiii ooooh tunakutumia configuration setting nyingine na tatizo litakwisha lakini wapi.Mbona hapo nyuma nilikuwa na browse net vizuri tu.SHIDA NI NINI HEBU NIWEKENI WAZI MAANA MBs zangu huwa zinapotea bure tu mpaka nitoe kadi niweke kwenye modem ndio walau nazifaidi.

NJOONI MNIJIBU HUKU MAANA MIMI HUU NAONA NI WIZI TU!

Pole sana, tafadhali tunaomba namba yako ya simu na eneo ulilopo kwa msaada zaidi.
 
Habari flora msoffe utaratibu ni huo huo katika kuangalia salio, *149*01# chagua 1 kisha chagua Internet & BB ->Internet & BB10->Salio la Kifurushi

Una kiasi cha 103.125 MB za data kwenye akaunti yako binafsi na mwisho wa matumizi yake ni tarehe 19/09/2014 13:32:23. Asante kwa kuchagua V

Thanks sasa nimejua jins ya kuuliza Salio ya mb...
 
Last edited by a moderator:
Hata mnipe line ya bure na muweke GB100 za data,sitakaa nitumie mtandao wenu washenzi nyie.mliiba salio langu sh. 100000 La MPESA na nilifatilia mpaka nkachoka nkaamua kuhama.
 
Habari, ujumbe wa kufahamisha kuwa kifurushi kimekwisha unatumwa ndugu mteja, pia tunakushauri kuangalia salio la kifurushi kadri unavyoweza kulingana na matumizi, hii itakusaidia kupunguza matumizi ya Intaneti pindi kifurushi kinapokaribia kuisha. Ahsante

Pengine hujanielewa au sijakuelewa
Ni hivi, nina salio la sh 10,000 then nanua kifurushi cha mb200 kwa sh 500 nabakiwa na balance ya sh 9500.

Nikitumia hicho kifurushi cha mb200 kikiisha sipati sms yoyote then balance yangu ya sh 9500 inaanza kutafunwa yote hadi ikiisha tu immediately napokea sms kifurushi changu mb200 kimekwisha

Sasa utakapo taka kununua tena unakuta una 0 sh

Ndio tunasema kwanini msiset ikiwa bado mb kama 10 hivi sms inakuja kuwa Zinaisha bado mb10 au tano?

Biashara ya kuangalia kifurushi cha data nani ataiweza kila dakaki jamani bora hata ingekuwa na short cut kama ya kuangalia salio la cheka

Mbona kwenye calls za cheka ikibaki dakika unakuwa alerted
Biashara ya kuchungulia salio ni ngumu maana matumizi yanatofauti wakati mwingine bila wewe kujua, kama updates mbalimbali nk
 
Huu wizi wa mchana wa VODACOM lazima ukomeshwe, wanakuwa kama vibaka wavaa tai!

Nakushangaa maana hapo tatizo ni la kwako sio la Voda, jamaa unawalaumu bure tu... simu yako inakula pesa kutumia data lawama unapeleka kwingine..
 
Nipo nje ya nchi simu yenye simcard ya Vodacom niliisahau Tz nimewaomba walioko huko wa-recharge wanaambiwa(Vodacom) wanashindwa kuitambua number. Nini ninaweza kufanya ili line isiingizwe sokoni?

Pole sana, tafadhali tutumie namba hiyo PM tuiangalie katika mifumo yetu.
Habari ngafu tafadhali wafahamishe waweke vocha katika simu hiyo sasa.
 
Line yangu huwa nawekewa salio na ofisi na naweka salio pia. Sasa nina salio niliweka huwa halitumiki mpaka la ofs liishe. Nikiangalia salio kwa sasa mnaniambia kufikia 04.12.2014 niwe nimelitumia limeisha!! Je, hii ni haki? Kwanini mniwekee limit ya muda ya kuwa na salio kwenye cm yangu?
 
Malalamiko yangu in kuhusu huduma ya wimbo ya mwito kwenye Simu , huwa mnaweza kumkata Mteja fedha kila anapokuwa na salio mila mpango nahii ilinitokea hadi nikaamua kujiondoa, acheni hayo mambo kuweni waminifu.
 
Nimefanikiwa kujiondoa baada ya wao kunitumia tena habari nyingine na mimi kureply kwa kuandika 1.

HATA hivyo sijapenda kabisa huu utaratibu wa kuunganishana kinyemela.

hata mimi wa.wameniunganisha na nipashe wananikata hela. huu ni wizi kabisa nimeamua kununua laini yamtandao mwingine ndo naweka hela. ila ukiwauliza wanakataa wanajifanya umeunganisha mwenyewe wakati uongo
 
Pole sana, tafadhali tunaomba namba yako ya simu na eneo ulilopo kwa msaada zaidi.

Naomba kusema hii tabia ni ya KIPUMBAVU, kuweka vocha then inayeyuka bila matumizi, WIZI uliokithiri.

Ni takribani wiki mbili sasa nimekuwa nikinunua muda wa maongezi katika simu, nimeweka 'vocha' ya elfu tano, zaidi ya mara nane, hii ikiwa kila vocha ninaitumia ndani ya siku mbili hadi tatu, Tena hapa kila siku mtu unajiunga kwa vifurushi vya kila siku vya CHEKA.(Intaneti, muda wa maongezi na ujumbe mfupi wa maneno).

Tatizo hili lilishawahi kunitokea hapo kipindi cha nyuma na baada ya mzozo mrefu HQ Mlimani City walirudiaha vocha ya 20,000/= .Sasa hii tabia imejirudia, Acheni usanii wa kuomba namba za simu hapa na kisha kutofanya marekebisho.

Kitu kibaya ni kuwa nimekwisha tupa karatasi(vocha hizo nikizozitumia) lakini kama mkihitaji namba nitawatumia. Hii tabia inakera, mtu unaweka vocha pengine unakwenda sehemu isiyo na huduma kwa uharaka then unakuja kudhtuka eti hua salio na unakuta hujafanya matumizi yeyote tena hapa umejiunfa kwa vifurushi vyenu. Ninaomba kusema acheni UPUMBAVU huu na jirekebisheni.
 
Kwa kusoma hizi comment za watu tayari nimeshawishika kuhamia airtel. Kwaheri voda,
 
Back
Top Bottom