Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

inaelekea mnara wenu Kinyerezi mwisho una matatizo au haufanyi kazi au labda eneo lile hamna mnara labda tunahudumiwa na mnara wa mbali sana. Mawasiliano kwa ujumla ni mabaya sana, kupiga simu shida wakati wowote mnara unashuka na simu inakatika, wakati mwingine mtu wa upande mwingine humsikii. Kwa upande wa internet ndio balaa kabisa, yaani huwezi kufanya chochote. Mbona tigo na airtel haina shida yoyote nyie kitu gani kinawashinda? Namba yangu ndio ninayotumia na inayofahamika na wengi lakini nyie mnanilazimisha niitoe kwrnye simu niweke airtel au tigo
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Tunaomba radhi kwa usumbufu.
 
Mtandao wenu internet iko chini sana. Mnataka nitaje nilipo ili ning'olewe meno na Sitta kwa ninavyomuandama sio? Shikeni adabu yenu,natumia voda kwa mpesa tu basi.
 
Habari,huduma iko sawa kwa sasa. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Nashangaa kusema kwamba kwa sasa internet iko sawa wakati ndo kwanza iko slow zaidi! Na kinachonishangaza ni kwamba nimejiunga na internet bila kikomo wiki! Jamani naomba mnirekebishie niweze kuenjoy ela yangu,imewashinda basi mniambie niangalie plan b.
 
Pole sana, tafadhali tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Tunaomba radhi kwa usumbufu.

Hivi wewe unalipwa kwa kazi hii? Unaijua kazi yako kweli?
Huyo mtu amekwambia mtandao wenu upo chini eneo hilo wewe unamjibu akupe namba yake!!

Useless kabisa wewe
 
Nilinunua salio kupitia ATM ya NBC lakini salio halikuingia kwenye namba yangu ambayo ni 0757371064
 
Hapa kila nikiweka salio nakatwa pesa vibaya mno mpaka nomeamua kusitisha tatizo nini bandugu
 
Nimenunua simu ya 4G baada ya kuweka laini nikaambiwa haisupport 4G je naweza badilisha laini inayosupport 4G?
 
Hivi wewe unalipwa kwa kazi hii? Unaijua kazi yako kweli?
Huyo mtu amekwambia mtandao wenu upo chini eneo hilo wewe unamjibu akupe namba yake!!

Useless kabisa wewe
Habari, kuna taarifa muhimu na za msingi unaporipoti tatizo kwa fundi ambapo namba ya simu ni muhimu zaidi. Ahsante
 
Hapa kila nikiweka salio nakatwa pesa vibaya mno mpaka nomeamua kusitisha tatizo nini bandugu

Habari kuhanda kawili tafadhali hakikisha umezima huduma za Intaneti katika simu yako kabla hujaongeza salio, ongeza salio nunua kifurushi cha Intaneti kisha fungua huduma.
 
Last edited by a moderator:
Vodacom, mnashughulikia tatizo langu kwa kuwa ni general problem au? Hii meseji yenu nitaitumia kama ushahidi ikitokea mmelamba salio langu muda huo ukifika
 
mimi wananikara sana siku hizi kifurushu chao cha speed bila kikomo hakina speed kabisayaani bora cha tigo
 
nahitaji kuelewaa malipo ya riba ya mpawa mnaya calculate kivipi na yanalipwaaa baaada ya mda ganiiiiiii maaana iko kibubuuu tangu nianzenacho sjaona nlichokipataa nikisoma brochures zenu riba mnalipa kuanzia 2%→ 5% kwa siku mi uwa naweka sometimes mpaka 1m na zaid kwakiutegemea napata kitu sasa naomba kujuaaa future value ya 1m per day ni calculate per month ndiooo niendeleee kutumia mpawa otherwise ni invest mtaani niuze mkaa nitoke tu
 
Mkuu yenyewe Vodacom Tanzania ndiyo mtandao pekee unaokupa uhuru wa kweli katika kutumia huduma zake.

Vodacom Tanzania naomba mnifahamishe kwanini mnaweke watu nyimbo za miito wakati hujachagua?
_nina baba yangu mdogo ni mchungaji ukimpigia simu inataja mawaidha ya shehe kishiki kweli hii si haki,au unaampigia mwislam simu nasikia nyimbo ya nibebe na ukimuuliza anashangaa kutokuweka hizo nyimbo....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom