Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom mnaboa sana, mnaiibia kupitia huduma zenu mf , sokoni sijajiunga mimessage inaingia muda wote niki-stop ama kucansel haiwezekani ni kero mpaka natamani kuitupa
 
Upuuzi wa airtel ni kusajili kifurushi cha kutunia vocha zao zile kwa mitandao yetu ya bongo simi ikiwa na salio la kuanzia elfu 20 watakusumbua na mimeseji mpaka ukome
 
Mimi nimelipia kifurushi cha elifu 20 cha internet ambacho hakina kiwango kama wanavyodai.Kuna saa net inakatika ovyo yaani wakiona umejiunga tu manyanyaso mtindo mmoja ukidonload video ni kilio jamani mbunge wa zamani mbona unatuuzia matatizo kwa hela zetu!!?
 
Sasa Vodacom!! Nipo hapa ofisini kwenu. Naomba mnisaidie ni SWAP line yangu ryt nau.
 
Vilevile jaman watanzania tuangazie kwa upya mtandao huu tukikazia macho kitengo cha mpesa.kiukweli wanatoza pesa nyingi mno.hebu fikiria unamtumia mtu pesa,wewe unaemtumia unakatwa na anaezipokea pia atakatwa pindi atakapozitoa,hii ni haki?na wamefanya hivo ili kupunguza ukali kidogo tu kuwa badala ya kukata elfu saba mathlan basi mtumaj anakatwa elfu na mia tano na akizipokea atakatwa elfu tano.sio haki jaman.hizo hela ni nyingi mno.badala mngeweka unafuu hata hapo ukizingatia unakuta mtu kashakupa hela ya kutosha tu mathlan mfanyabiashara anaagiza mzigo wake kwa njia ya kupiga simu ameongea nusu saa nzima,stil akija kutuma hela yake ya manunuzi nayo mnaikata?inauma sana ila ndo hatuna jinsi,ila naamini ipo siku nanyi mtaanguka kama ttcl mtabak maofisini tu ipo siku.

Mtanzania mnyonge
 
Mbona hamnijibu. Internet bila kikomo kwa nn baada ya muda mnapunguza spidi?!
 
VODACOM NAOMBA MAJIBU.nina kifulushi cha internet cha mwezi na hapa kuna MB 4657.891 lakini internet inafungua kama ndo namalizia kifulushi..bola hata ningekua nje ya mji lakini niko katikati ya jiji la Arusha,nitaukimbia mtandao wenu sasa hv msipojilekebisha,nina uhuru wa kusema maadam nimeweka pesa na nimenunua kifurushi na mmekata pesa vizuri sana na kutuma ujumbe wa kuniambia nifulahie huduma ya kuperuzi.mnanichefua kwa kweli
 
Naomba voda taarifa ije zikibaki MB Angalau mbili maana ikija mwisho na salio liliopo linakata hata kabla hijasoma sms ya taarifa
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?



Vodacom Tanzania
[/F

mr voda habari yako!
mie niko poa! tatizo kwa upande wangu lipo kwenye huduma ya data hasahasa 3g! huduma hii nafikiri hadi sasa unafahamu ni kwa kiasi gani imekuwa na umuhimu kwa kila mtu mwenye uhitaji wa data! sasa hapa wilaya ya ngara mkoa kagera huduma hii mmeiweka katika roaming hali inayoifanya,
a,) isipatikane kwa kila mmtu mwenye simu yenye intenent 3g.
b) hata kwa wale wenye simu zenye uwezo wa kuipata hiyo net work voice call inadrop down kila baada ya sekunde kadhaa,
c) lakini pia haipatikani kwa uhakika kwa maana kwamba ipo upande mmoja tu wa mji upande mwingine hasa nyanda za chini ya na pembezoni mwa mlima ni majanga ispokua 2g!

mi naonelea kuwa kulingana na uhitaji wa huduma hii ni bora kama ule mnara wa karibu na magereza au niseme benki ambao ndio tegemeo la wengi ungepewa jukumu hili! kuliko huu mpya mliouweka hapa karibu na msikiti na kuupa hii roaming sevice!
naomba kuwasilisha!
 
Voda huduma Zime dolora a mtu anatuma SMS inakaa zaidi ya masaa 3 had 4 au anakupigia sipatkani imekuwa kero. Kama kuna uwezekano ongezen booster za mtandao ili kupunguza msongamano (network jam)
Habari Edson Ndile tafadhali tutumie taarifa PM zikihusisha namba unayotumia na sample ya namba ambazo zikikutumia ujumbe unachelewa kufika.
 
Last edited by a moderator:
Jamani nyie vodacom mmenikera na mnaendelea kunikera kwa kunikata hela za hivyo vichwa vya habari vya nipashe nimewapigia zaidi ya mara sita mnaahidi kutoa ila hamtoi nmeweka vocha sijaitumia ila sahivi imebaki nusu afu hao customer care wenu kila anayepokea Ananipa maelekezo yake mnanichefu kesho nikiamka salama hilo vumbi nitalowawashia mtajuta
Pole sana Sonia G, tutumie namba ya simu PM kwa msaada zaidi. Pole mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Wajanja night irudi 4gb itakua poa sana halafu gharama za.vifurushi kwenda mitandao yote mmepungza dk na bando sio poa wala nini bora mngeacha vilevile au mngeshusha mitandao mingine isingewakamata daima..
Ahsante kwa marejesho Bakari, tutayazingatia.
 
Kwakweli mtandao mkubwa kama Vodacom inasikitisha na kuaibisha pale inapoweka swala usanii ndani ufanisi wao wa kazi, nikianza na dk za cheka kuna usanii mtupu unaoendelea hapo ndani mpaka uwizi wa dk, mbili mkijua mnahitaji wateja wengi boresheni huduma zenu yaani network kwani hapo kuna kero kubwa sana ktk hilo, internet yenu ni tatizo kubwa ipo slow sana sana, namalizia na wafanyazi ndani ya kampuni sio wote ila wengi wao wanafanya kazi kama wana hisa ndani, wanafanya kwa ulegevu na kuangalia watu kama nyanya mbichi alimradi kakaa ktk kiti cha huduma jirekebisheni. Vodacom bado kazi ipo
Habari Shigella, ahsante kwa mrejesho wako na tutazingatia masuala haya. Tungependa kujua lini ulipata tatizo la wizi wa dakika tuweze kusaidiana. Ahsante
 
Back
Top Bottom