Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Mtandao wa Vod COM kwa siku za karibuni umekuwa hauaminiki tena kwani makato yamekuwa yakibabe bila kujali customer care, mteja akiweka salio anaahidiwa zawadi lakini cha ajabu zawadi ya salio inakuwa adhabu kwani wanakati kwa speed mbaya.

Tunaomba mlioko VODA mtambue tunaumia sana kwa makato haya yasiyo na huruma kwa mteja
 
wametoka wananitafuna buku yangu muda si mrefu naona hadi uvivu kuwapigia maana hata ufanyeje hela hua hawarudishi hawa deci wakubwA nyie voda acheni ujambawazi tutaandamana. mpaka ofsini kwenu na ugali halafu tuwachome moto muwe kitoweo
 
Aisee hii mitandao naona wote ni watoto wa panya. Ndugu wala usihame utakuwa unamkimbia nyani na kwenda kwa ngedere. Mhimu tu komaa nao ikiwezekana nenda customer care wakakupatie majibu stahiki ndugu inaweza kukusaidia. Mm nna airtel shida tupu ilikuwa kila wiki lazima wakate 500airtime. Nikiwapigia majibu eti umejiunga na huduma za wiki lakini hawasemi ni nini hizo. Ilinilazimu niende hadi ofisini kwao nusura tukunjane na helpdesk mmoja pale moroko. Kikubwa ni kuwa TCRA hawana meno kwenye haya makampuni ya simu ndio maana kila siku wanakuja na vigezo vya promotion ili watuibie vizuri.
 
Mimi kuanzia leo siweki salio hadi wajirekebishe, hii nchi wawekezaji wote ni wezi tu
 
Vodacom mna matatizo makubwa sana.

Kwanza Sim Banking haiaminiki. Nahamisha pesa toka benki na zinatoka, linapokuja suala la kusubiri Mpesa ninachoka.

Pili, mna tatizo la LUKU. Mteja anakaa sana bila kupata token na akipiga simu anajulishwa kuna matatizo ya kiufundi. Sawa, matatizo yapo, ila iweje nyie ndo mkithiri?

Jipangeni bwana
 
Your not serious na biashara..bundle la week linakaa siku 4 limeisha? Salio usipounga package linakatwa ukiuliza uliwasha 3g wakat nikiuliza hiyo huduma unasema hapo nilipo haipo....


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kila siku voda wananipigia zaidi ya mara 10 kwa namba hzo, nipo kazini, kwenye mkutano nashangaa simu inaita kupokea nakuta wananiambia mambo ya nyimbo, are they serious? Muda huu nimeonekana kama msumbufu ndani mkutano. Embu achane bana @Vodacom
 
Vodacom kazi ni kwako😍, maisha murua ukiwa na Vodacom 😋
 
Voda mnamatatizo sana ktk mtandao wenu na pia tengenez system ambayo km mtu akikosea kutoa pesa kwa m-pesa akanunua muda wa maongez inabid airudushe kwa m-pesa, hebu jitahid ktk hilo swala ht km haiwalip ila mtajiboreshea kaz na mtatuokoa na hilo janga
 
vodacom siipend na ndo maana nshaacha kutumia,,,,,,mnakatabia ka kukata salio bila xababu za mcng watu wakiuliza mnawacngizia either wamejiunga na huduma ya caller tunes na wakat yy hajajiunga naapengne mmemuonganxha wenyewe na ama anatumia huduma za kibenki na wakati mtumiaj hajaanza kutumia hduma hyo leo,,,,katika yote jitahd kuiga tigo na airtel katika huduma za kibenki kuangalia salio c lazma uwe na hela kwenye cm ,,,,kuhamsha napo,
 
voda nina mwezi sasa siweki salio, napokelea simu tu tena baada ya mwezi huu naitupilia mbali kabisa. airtel ndo mpango wa mjini, kuna ile OMG ni hatareeeeeee
 
Back
Top Bottom