Hiyo ishu ilinipata last week, nakumbuka nilituma muda wa maongezi kwa simu nyingine na kubakiwa na salio la >40,000/- jioni ya saa 10, simu sikuitumia tena ila kesho yake jioni naangalia salio 00, kuwapigia.wahudumu, wakwanza akakomaa may be nimetumia kwa data nikajisahau, nikamhakikishia simu hiyo haipo connected akakomaa nikaona mzushi nikaachana nae, baada ya muda nikapiga na kumpata mhudumu mstaarabu tukafuatilia matumizi yalivyokuwa kwenye system na kugundua kweli toka mda huo wa mwisho kutumia kulibakiwa na salio >40,000/- na baadae inaonesha 00, alinihakikishia baada ya masaa 24 watarekebisha, nashukuru wslirekebisha na kurudisha hela yangu, Kiukweli mitandao hii ya simu inachofanya siyo, je nisingekomaa si ningeshapoteza? Na sasa wamekuja na mbinu hii ya data, je, nini mkongo wa taifa waliotuhubiria? Wapi TCRA?