Wajameni Vodacom,
Waoneeni huruma watanzania. Mmeleta utapeli mwingine wa JAY Millions. Mimi ni mteja wenu, hebu nijulisheni hadi leo watanzania wangapi wamenufaika na promosheni hiyo? Kwenye tangazo mnasema kuna mshindi wa zawadi mojaya Sh. Milioni Mia moja 100,000,000.00 kila siku, washindi 10 wa Sh. milioni kumi kila siku 10,000,000.00 na washindi 50 wa milioni moja moja na washindi wa salio la elfu moja.
Naomba kujuzwa hadi sasa ni watanzania wangapi wameshinda Milioni mia moja, wangapi milioni kumi, na wangapi milioni moja? Mimi nakumbuka mshindi mmoja tu wa milioni mia moja kutoka Iringa. Cha kushangaza mshindi huyo ambaye alikuwa anafanya kazi ya kuuza baa, amehama alipokuwa anafanyia kazi lakini aliko sasa ni masikini wa kutupwa.
Hizo pesa alizoshinda mwaka jana zimeishaje katika kipindi kifupi hivyo?