Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Asubuhi ya leo nimenunua kifurushi cha wiki cha Vodacom kwa shs 5000, saa kumi naambiwa kifurushi kimeiisha,Du!! 😎
 
Rasmi , kesho naenda kutafuta na kusajili laini ya TTcl na kuichomeka kwenye hii pixel yangu sababu(internet bundle). Pia nafikiria kununua na kitochi niweke hii laini yangu ya voda itakua tu inatumika KwA miamala[emoji51]na TTCL ikizoeleka ndo BAsi ntaitupa tu hii voda maana siwez miliki Wala tembea na simu zaidi ya moja, lazima ntapoteza moja.
Kwa nini Vodacom?
 
Nyinyi ndiyo mnawapa viburi. Mm tangia wapandishe bei ya vifurushi sijaweka vocha yoyote na hawatalamba hata 100 yangu
Asubuhi ya leo nimenunua kifurushi cha wiki cha Vodacom kwa shs 5000, saa kumi naambiwa kifurushi kimeiisha,Du!! 😎
 
Kaangalie kwenye website Yao .....share holder NI Nani na Nani kwenye Vodacom, kisha niulize kwanini hao, wananguvu gani na wanamtandao ganiiiiii
 
Hatuna cha kufanya Zaid ya kufuta mnachotaka, yote haya ni kwa sababu serikali inawalea na hawana cha kuwafanya.

Serikali imalisheni TTCL, haya makampuni ya kigeni yana tuibia.
Voda com mlikuwa kama malaika wakati huu, mmepata pesa saivi mmevimba hata huduma zetu zimekuwa kichefu chefu na kero bila kutatua kero.

MNACHOSHA.
 
Vodacom mambo mnayoyafanya siyo kabisa Jana nilifanya clearence ya madeni yangu yoote ktatika line yangu ya voda, nikasema Leo acha ninujue vocha ya 500 niweke ili line iisiwe dormant cha ajabu naweka tu kosa imetafunwa yote,nikaone nipige HUDUMA kwa wateja niulize hili ile napiga 100 naambiwa nisishangae salio langu linekatwa kwa deni nililokuwa nadaiwa ikabidi nikae kwanza kimya nitafakari wamejuaje ya kwamba shida yangu ingekuwa ni salio langu kukwapuliwa?this looks like setup automations after be absorbed. kwa kweli nimevunjika sana moyo,
*my quest walijuaje ya kwamba shida yangu likuwa ni ningeuliza salio langu? BUT ALL THANKS YOU.
 
GHARAMA ZA VIFURUSHI.

Kwa nini hadi leo mmekaidi agizo la serikali la kurejesha bei za VIFURUSHI?

Mimi natarajia kuachana na kutumia line ya voda baada ya kuitumia tangu 2005, ila sitoacha salama, kwanza mm na familia yangu wote tutaacha mara moja kutumia line zenu, mm binafsi nitakopa songesha 34,000 nitakopa nipige tafu na baada ya hapo nitapita vodashop kufuta usajili wa line yangu na kamwe sitotumia mtandao wa voda kwa maisha yangu yaliyosalia
 
Sidhani kama mko serious na kuboresha huduma zenu. Nitakuwa mpole kurudia hoja zilizosemwa na watu wengi hapa:

1. Gharama zenu za bandle za internet ni kubwa sana - japo serikali ilisema mtazishusha mmekataa. Kmf. recently mlikuwa na bandle ya 'Ya Kwako tu' kwa siku ilikuwa 1024 MB kwa Tsh. 1000 lakini sasa ni elfu 2. elfu moja unaweza kupata MB 400 tu. that is a dramatic change.

2. Bandle zenu zinaisha haraka sana as if kuna mtu Vodacom anafanya kazi ya kuzipunguza. Jana niliweka bandle ya 2000 (1000 MB) ziliisha within 30 min. na nilikuwa siangalii movie bali news za kawaida tu za internet na video chache sana na fupi za youtube.

Watu wanaposema watahama hawatanii. Kwa mfano mimi nimedhamiria kwa dhati kuacha huduma zenu za internet. Unfortunately natumia 3G Vodafone smart tablet inayotumia line yenu tu. Nadhani kwa vile mna wateja wengi kama mimi na wengine mnadhani hakuna shida. Lakini bila shaka mtapoteza income na kibiashara sio healthy kujiamini that much! Mimi natafuta modem ya Airtel au TTCL (whatever cheaper network) ili niachane na nyinyi.
 
Back
Top Bottom