Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.
Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.
Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.
Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom
UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.
Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.
UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.
Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.
Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.
Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.