Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hameni huko wandugu mbona mnateseka hivyo? Voda ni majizi namba 1 wakifuatiwa na mitandao mingine.
Kweli kabisa. Bora niwe najiunga kifurushi cha airtel cha 10,000 kwa wiki niphase out kabisa huu mtandao wa majambazi
Yaani huku airtel sawa tunaibiwa lakini si sawa na wizi mkubwa wa vodacom
Sijui wakiona hizi chuki
juu yao wanajisikiaje au ndio mteja kwao sio mfalme bali
----............
Ha ha ha. Ina maana airtel wanadokoa ila haya mavoda yanachota
Vijamaa vya airtel vijizi lakini vinaiba kistaarabu yaani kama una debe la mahindi vinadokoa kikombe kimoja cha chai tofauti na voda wao wanakwiba debe zima. Kingine airtel ukiwasiliana nao kwa email yao ya msaada hayapiti masaa 24 wanakupigia wenyewe na mnatatua tatizo lako. Hebu wajaribu kuwapigia voda kama utawapata. Majanga yaani vodacom majanga
Msije mkalogwa mkanunua bundle la mwezi kama nilivyofanya mimi. Nimenunua bundle la la Mwezi la gb 1. Nimetumia siku 3. Tena katika whats app. Baada ya siku 3 naambiwa eti eti zimebaki bundle 365mb. Leo asubuhi zimebaki bundle 46mb. Wezi wakubwa hawa vodacom. Msije kufanya makosa niliyofanya mimi i thought nina save kumbe ndo ninaibiwa. Nilikuwa naitetea sana inaposemwa vibaya hii kampuni. Kwa tukio hili sina imani nao tena. Wezi wakubwa.