Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

Hivi tarehe moja imepita?…. #Acha kutuchosha
 
inamaana unatumia laki mbili kumpa mteja aliyetoa pesa, wanamkata elfu 5, wewe unalipwa buku? huu ni wendawazimu.
 
Biashara mtandao
Unavuna ulichopanda
Watu hawajuagi tu bora kulima matiki au pilipili zinalipa badala ya kuhangaika na umessenger au ukuwadi wa hela za watu
Huu upigadebe wa hela sio
 
Ahaaaa!! ha ha haaa! jamani kumbe kulia kupokezana!

Mbona sisi siku ile ya mishahara kuchelewa mlikuwa mnasema humu kwamba tuwe na njia mbadala!!!

Kumbe na nyie hamna njia mbadala!!!!
 
Biashara kichaa kabisa, yaani kwenye buku 5 wakala anapata 600?
 
Naunga mkono hoja....

Ni biashara ya kipumbavu sana basi tunafanya hakuna namna.....

Ni kweli tunanyonywa sana lakin hata hicho kidogo tupewe

Mkuu sipati picha ikifika saa sita usiku hujapewa hilo gawio itakuwaje. Naona kama voda wanakulazimisha kwenda magereza kwa nguvu.
 
Nimesoma uzi huu nikiwa najiandaa kusajili line ya Mpesa, stimu yote imekata bora tuhela twangu tubakie huko huko benki!
...kwanza unaweka roho yako hatarini vibaka na wezi wa mtandao wanakuwinda kama swala bado kamisheni ndio hivyo ni za kinyonyaji bado kwenye kamisheni utakayopata ata kama ni elfu 10 inakatwa kodi 10% yaani aisee tumekua watumwa wa makampuni ya cm ndani ya nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…