Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi tarehe moja imepita?…. #Acha kutuchoshaHabarini za asubuhi wanajamvi.....
Si kawaida Voda kutokuwalipa mawakala wao wanaotoa huduma kwa wateja wao mpaka sasa muda huu napoandika Uzi huu,
Huwa ukiamka asubuhi siku ya tarehe 1 unakuta message ya kamisheni kwenye simu yako lakin Leo mpaka sasa hakuna kitu kulikoni?
Je humu jamvini kuna wakala wa MPESA
na mpaka sasa haoni chochote kwenye simu yake?
Si kawaida Voda kutokuwalipa mawakala wao mpaka sasa
Kama kuna tatizo kwanini hawakutoa taarifa mapema kwamba hawatopewa kamisheni Leo?
Mwenye kujua tatizo atusaidie...
inamaana unatumia laki mbili kumpa mteja aliyetoa pesa, wanamkata elfu 5, wewe unalipwa buku? huu ni wendawazimu.Kamisheni zenyewe za kipumbavu sana. Yaani mtu anatoa laki mbili yeye anakatwa elfu 5 af wewe wakala unaambulia mia sita. Huo si Ugolo? yaani hamna biashara ya kijinga kama uwakala huu. Kwa jicho LA nje watu wanaona kama ni biashara nzuri ila ukiingia ni upuuzi tu. Kuna watu ndio wanafaidi kama wakala mkuu na voda wenyewe ila we unaepingwa jua na kuzungufusha pesa yako ni njaa tu. Unapewa mpaka sh 100 kwa muamala wa elf 10? Ndio maana Mzee wakala hapo juu anawenge anaulizia kamisheni saa moja asubuhi ya tar 1 as if tar 1 imaisha bila kupewa hyo kamisheni ya elf 43 kwa mwezi.
Bora hiyo mkuu luku za umeme ukiuza laki unapata 500 kamisheni. Hapo bado hujanunua roller za mashine 2,000/=Daaa upuuzi mtupu,yaani kwenye buku 5 napewa Tsh 600? Khaaaaa!!
Fedha zote zinaenda kwa Wahindi.Bora hiyo mkuu luku za umeme ukiuza laki unapata 500 kamisheni. Hapo bado hujanunua roller za mashine 2,000/=
Ni noma mkuu...hapo kuna ushuru TRA, kampuni ya katikati, mawakala wakuu na makorokoro mengine kibao.Fedha zote zinaenda kwa Wahindi.
Hata kama sitegemei si haki yangu lakin?
Kwanini nisipewe
Naunga mkono hoja....
Ni biashara ya kipumbavu sana basi tunafanya hakuna namna.....
Ni kweli tunanyonywa sana lakin hata hicho kidogo tupewe
Kabla ya kupiga simu nimeona niulize humu pengine ni Nchi nzima....
Nimesoma uzi huu nikiwa najiandaa kusajili line ya Mpesa, stimu yote imekata bora tuhela twangu tubakie huko huko benki!Nilikuwa naiwaza hii biashara lakini kwa comment hapo juu inaonekana ni biashara kichaa siifikilii tena
....hii sio biashara kabisa unakuwa na mtaji wa laki 5. alafu kamisheni mwezi mzima unalipwa elfu 43...naifunga mwezi huu bora nikauze mifuko mipya ya makamba.Nilikuwa naiwaza hii biashara lakini kwa comment hapo juu inaonekana ni biashara kichaa siifikilii tena
...kwanza unaweka roho yako hatarini vibaka na wezi wa mtandao wanakuwinda kama swala bado kamisheni ndio hivyo ni za kinyonyaji bado kwenye kamisheni utakayopata ata kama ni elfu 10 inakatwa kodi 10% yaani aisee tumekua watumwa wa makampuni ya cm ndani ya nchi yetuNimesoma uzi huu nikiwa najiandaa kusajili line ya Mpesa, stimu yote imekata bora tuhela twangu tubakie huko huko benki!