Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

Habarini za asubuhi wanajamvi.....

Si kawaida Voda kutokuwalipa mawakala wao wanaotoa huduma kwa wateja wao mpaka sasa muda huu napoandika Uzi huu,

Huwa ukiamka asubuhi siku ya tarehe 1 unakuta message ya kamisheni kwenye simu yako lakin Leo mpaka sasa hakuna kitu kulikoni?

Je humu jamvini kuna wakala wa MPESA
na mpaka sasa haoni chochote kwenye simu yake?

Si kawaida Voda kutokuwalipa mawakala wao mpaka sasa
Kama kuna tatizo kwanini hawakutoa taarifa mapema kwamba hawatopewa kamisheni Leo?

Mwenye kujua tatizo atusaidie...
Hivi tarehe moja imepita?…. #Acha kutuchosha
 
Kamisheni zenyewe za kipumbavu sana. Yaani mtu anatoa laki mbili yeye anakatwa elfu 5 af wewe wakala unaambulia mia sita. Huo si Ugolo? yaani hamna biashara ya kijinga kama uwakala huu. Kwa jicho LA nje watu wanaona kama ni biashara nzuri ila ukiingia ni upuuzi tu. Kuna watu ndio wanafaidi kama wakala mkuu na voda wenyewe ila we unaepingwa jua na kuzungufusha pesa yako ni njaa tu. Unapewa mpaka sh 100 kwa muamala wa elf 10? Ndio maana Mzee wakala hapo juu anawenge anaulizia kamisheni saa moja asubuhi ya tar 1 as if tar 1 imaisha bila kupewa hyo kamisheni ya elf 43 kwa mwezi.
inamaana unatumia laki mbili kumpa mteja aliyetoa pesa, wanamkata elfu 5, wewe unalipwa buku? huu ni wendawazimu.
 
Biashara mtandao
Unavuna ulichopanda
Watu hawajuagi tu bora kulima matiki au pilipili zinalipa badala ya kuhangaika na umessenger au ukuwadi wa hela za watu
Huu upigadebe wa hela sio
 
Ahaaaa!! ha ha haaa! jamani kumbe kulia kupokezana!

Mbona sisi siku ile ya mishahara kuchelewa mlikuwa mnasema humu kwamba tuwe na njia mbadala!!!

Kumbe na nyie hamna njia mbadala!!!!
 
Biashara kichaa kabisa, yaani kwenye buku 5 wakala anapata 600?
 
Naunga mkono hoja....

Ni biashara ya kipumbavu sana basi tunafanya hakuna namna.....

Ni kweli tunanyonywa sana lakin hata hicho kidogo tupewe

Mkuu sipati picha ikifika saa sita usiku hujapewa hilo gawio itakuwaje. Naona kama voda wanakulazimisha kwenda magereza kwa nguvu.
 
Nimesoma uzi huu nikiwa najiandaa kusajili line ya Mpesa, stimu yote imekata bora tuhela twangu tubakie huko huko benki!
...kwanza unaweka roho yako hatarini vibaka na wezi wa mtandao wanakuwinda kama swala bado kamisheni ndio hivyo ni za kinyonyaji bado kwenye kamisheni utakayopata ata kama ni elfu 10 inakatwa kodi 10% yaani aisee tumekua watumwa wa makampuni ya cm ndani ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom