Pamoja na mleta mada kuwa ameshapata malipo yake,naomba kumsaidia ili siku nyingine asije kulalamika. Commission huwa zinalipwa kuanzia tarehe 1-5. Hii ni kwa mitandao yote. Kwa hiyo unaweza kuwasiliana na wakala wako mkuu baada ya tarehe 5 km utakuwa hujapata. Na kwa wale wanaovunjwa moyo kufungua hii biashara msidanganywe,hakuna biashara rahisi na nzuri kufanya km hii ya miamala ya pesa. Kikwazo pekee kwenye hii biashara ni majambazi tu.
Kuna mtu hapo amesema alifanya miamala ya thamani ya milioni 33 na akapata laki 4 na 20. Lkn hajasema mtaji wake ulikuwa bei gani. Unaweza kufanya hata miamala ya thamani ya bilioni 1 Kwa mtaji wa laki 5 na ukapata milioni na nusu kwa mwezi. Hizo ni pesa za wateja wanaokuja ku-depost na ku-withdraw. Nimefanya hiyo biashara tangu mwaka 2011 hadi leo. Pesa zako muda wote zipo Salama,na ni pesa ambayo ukitaka ikusaidie inakusaidia hapohapo. Maana muda wote ama itakuwa kwenye simu au unayo cash. Na wakala ukitaka kutoa pesa zako hukatwi. Hiyo nyumba iliyopo kwenye avatar yangu,nimejenga kwa hiyo biashara. Na nilimvua mtu kwa milioni 14 nikaivunja nikajenga hiyo. Wale mnaotaka kufungua msikatishwe tamaa,karibuni tufanye biashara.