Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

Vodacom Tanzania yadaiwa kutowalipa mawakala wake wa huduma ya kifedha(M-Pesa) kamisheni zao

mtaji wa laki 6 kupata milioni 3 inawezekana kabisa. wateja wakitoa ukafika laki 6 unaenda kutoa cash bank mpesa unarudishiwa laki 6 yako unaendelea na kazi. hiyo laki 6 unaweza kufanya miamala hata ya milioni 10 kwa siku.
 
mtaji wa laki 6 kupata milioni 3 inawezekana kabisa. wateja wakitoa ukafika laki 6 unaenda kutoa cash bank mpesa unarudishiwa laki 6 yako unaendelea na kazi. hiyo laki 6 unaweza kufanya miamala hata ya milioni 10 kwa siku.
Acha maelezo ya abunuasi ,soma tena ulichoandika vizuri usikurupuke kutulisha ngusugi
 
Sio kweli huu ni uongo wa kupindukia!
Swala la kuchelewa kwa comission wasiliana na wakala wako mkuu mbona wengine wote wamelipwa
 
Biashara mtandao
Unavuna ulichopanda
Watu hawajuagi tu bora kulima matiki au pilipili zinalipa badala ya kuhangaika na umessenger au ukuwadi wa hela za watu
Huu upigadebe wa hela sio
nani kakudanganya tikiti!! utamuuzia nani? njoo kwenye mbogamboga; kila mmoja analima kwake za matumizi na wafanyakazi/watumishi wamestuka wanalima hoho, chinese, sukuma wiki, kabichi kwenye makopo na salfet. kuuza masokoni kwataka moyo hasa..!

nilikuwa naamini nyie washika chenji vibandani mko vizuri tuwe tunajipitisha na mabeseni yetu ya nyanya mtuunge kumbe nanyi ni.....!
 
comission za voda ni ndogo sana ajui kwangu tu au zinashuka nashangaa hadi airtel anampita wakati miamala ninileile
 
mtaji wa laki 6 kupata milioni 3 inawezekana kabisa. wateja wakitoa ukafika laki 6 unaenda kutoa cash bank mpesa unarudishiwa laki 6 yako unaendelea na kazi. hiyo laki 6 unaweza kufanya miamala hata ya milioni 10 kwa siku.
Kweli wewe kisandu kabisa kama sio deo
 
Kamisheni zenyewe za kipumbavu sana. Yaani mtu anatoa laki mbili yeye anakatwa elfu 5 af wewe wakala unaambulia mia sita. Huo si Ugolo? yaani hamna biashara ya kijinga kama uwakala huu. Kwa jicho LA nje watu wanaona kama ni biashara nzuri ila ukiingia ni upuuzi tu. Kuna watu ndio wanafaidi kama wakala mkuu na voda wenyewe ila we unaepingwa jua na kuzungufusha pesa yako ni njaa tu. Unapewa mpaka sh 100 kwa muamala wa elf 10? Ndio maana Mzee wakala hapo juu anawenge anaulizia kamisheni saa moja asubuhi ya tar 1 as if tar 1 imaisha bila kupewa hyo kamisheni ya elf 43 kwa mwezi.
Mimi nimepata kamisheni ya 19,476/=.
 
Mimi nimepata kamisheni ya 19,476/=.
Elfu kumi na Tisa kwa mwezi mzima? Vp mfanyakazi na frem unalipa sh ngapi? Af kuna pimbi humu anaongea utumbo wa nzi .eti alikuwa na laki 6 akapata m 3. Nshamwambia akafie mbele hope kesha rest in peace. Kampuni za simu zibadilike aisee twende nusu kwa nusu, otherwise tcra ichunguze vzr. Kunauzi unakuja wa kuwachana hawa watu wa mitandao watuondolee upuuzi wa mawakala wakuu coz hakuna kazi ya maana wanayoifanya zaidi ya kusubiri wewe urisk pesa zako ye achukue kamishen kubwa we uambulie elfu kumi na Tisa.
 
Duuuuuh lakini vijana tunataka kupata faida kiasi gani? Ndio turizike hakuna biashara isiyokuwa Na changamoto tujaribu kuwa wavumilivu ni Bora hio ya kupata kidogo sio kukaaaa kijiweni kuongelea siasa
 
Duuuuuh lakini vijana tunataka kupata faida kiasi gani? Ndio turizike hakuna biashara isiyokuwa Na changamoto tujaribu kuwa wavumilivu ni Bora hio ya kupata kidogo sio kukaaaa kijiweni kuongelea siasa
Unajua unatakiwa uwekeze sh ngapi upate hyo kidgo unayotuambia hapa? Acha kudandia treni kwa mbele Dada
 
Hamna biashara yenye raha na faida ya bure bure kama MPESA anae ichukia mpesa/tigo pesa huyo atakua ni mnyimi wa shukurani na hamna atakalo kaa afanyiwe ashukuru.

Biashara ambayo gharama ya uendeshaji wake ni akili yako na simu yako kuwa na chaji unailalamikia?? kwa mwezi mtu unapata 900k plus bureeeeeee halafu unalalamika eti unaonewa kweliiiii???

so unataka voda wapate bilioni na wewe upate bilioni ukiwa umekalisha tu hapo na kisim chako? Kampuni za watu zinapitia magumu mengi,hasara,changamoto,nk halafu unataka upewe sawa na wao faida? shenz type!

Katka 10,000 unapata faida sh.600 hyo 600 hujaitolea jasho ni umekaa tu mteja katoa hela huko wewe unapata kamisheni 600 kilainiiiii halafu unalalamika hapa...

Kaulize wauza maji/soda/juice faida ya 600 huipata baada ya kuuza kiasi gani cha maji? Acheni lawama zisizo na maana 600 kwa siku unapata wateja wa 600 wangapi?? unafungua asubuhi saa 1 unafunga saa 4 usku au wale waoga kama sisi tunafunga saa 1 kamili..hv umepata 600 ngapi per day??

Aseee wanasemaga upele humuota asie na kucha NIMEAMINI KWAKWELI....miti huota pasipo na wajenzi...yani mtu unaweza miliki MTAJI WA TGO PESA,MPESA,AIRTEL halafu tayari unajiona umekua tajiiiiriiiiiiiii bosssssssiiiiiiii hutaki tena 600 (maskini hawatoisha tanzania hiii blal full)

Bakhresa angekua na dharau za maskini kama sisi tunaodharau 600 sjui kama angeuza ice cream hadi leo..bakhresa na mihela yake yote ile huwezi mshawishi hata kwa bunduki aache kuuza ice cream NEVER ila mi bongo hapa inapata 600 tena haina mlolongo kuipata alafu analalamika lalamika...

Acheni lawama embuuuuuu....Kuna kazi gani inalipa kama MPESA na TIGO PESA isiyo kutoa jasho hapa TANZANIA?? anitajie mtu hapa leo kazi yenye mshahara mil.2 kwenda mbele ambayo hutoi jasho wala kuwa na presha wala kuumia na mawazo...MTU MMOJA ANITAJIE HIYO KAZI kama ipo.

Kazi zinazolipa ni nyingi tena zaidi ya hzi MPESA ila kazi zote hizo lazima JASHO LIKUTOKE ndio upate hiyo amount,Wakati mpesa na tpesa unakaaa tu Then kwa mwezi TIGO wanaingiza 5M voda wanaingiza 2M EATEL wanaingiza 1.5M Halotel na wenzie kina tpesa wao kwa ujumla walete 500k...Halafu kuna mtu mmoja kakaa pale anaponda MPESA.


Nakuhakikishia nyie ndio wale mna mademu/wake wazuriiiiiii waliokamilika kila idara halafu mnawaacha mnaenda kuchepuka na vitoto vina sura kama Mawe ya MISRI.

Kama unataka HESHIMA mjini WEKEZA KWENYE BIASHARA YA PESA KWENYE MITANDAO YA SIMU NA BANK...Katafute mtaji shambani then njoo ule maisha uishi bila stress.
 
Ha ha ha haaa milioni 33 ? Duuh kweli uwakala noumaaaa. Yaani hyo pesa ungenunua hata hiace mbili kila siku ungekunja c chini ya laki. Cpati picha hapo ni miamala kama elf 80 hivi
ungepata hiyo hela zaidi hata ya hyo laki ila Ukumbke biashara ya daladala haipo costant kwamba kila siku upate LAKI au zaidi..kuna leo kupanda kesho kushuka kuna gari kuharibika,kuna dereva kuumwa,kuna ajali,nk ila hyo 420k alopata yeye ni uhakika na zaidi ya yote labda iongezeke ila sio kupungua.
 
Pamoja na mleta mada kuwa ameshapata malipo yake,naomba kumsaidia ili siku nyingine asije kulalamika. Commission huwa zinalipwa kuanzia tarehe 1-5. Hii ni kwa mitandao yote. Kwa hiyo unaweza kuwasiliana na wakala wako mkuu baada ya tarehe 5 km utakuwa hujapata. Na kwa wale wanaovunjwa moyo kufungua hii biashara msidanganywe,hakuna biashara rahisi na nzuri kufanya km hii ya miamala ya pesa. Kikwazo pekee kwenye hii biashara ni majambazi tu.

Kuna mtu hapo amesema alifanya miamala ya thamani ya milioni 33 na akapata laki 4 na 20. Lkn hajasema mtaji wake ulikuwa bei gani. Unaweza kufanya hata miamala ya thamani ya bilioni 1 Kwa mtaji wa laki 5 na ukapata milioni na nusu kwa mwezi. Hizo ni pesa za wateja wanaokuja ku-depost na ku-withdraw. Nimefanya hiyo biashara tangu mwaka 2011 hadi leo. Pesa zako muda wote zipo Salama,na ni pesa ambayo ukitaka ikusaidie inakusaidia hapohapo. Maana muda wote ama itakuwa kwenye simu au unayo cash. Na wakala ukitaka kutoa pesa zako hukatwi. Hiyo nyumba iliyopo kwenye avatar yangu,nimejenga kwa hiyo biashara. Na nilimvua mtu kwa milioni 14 nikaivunja nikajenga hiyo. Wale mnaotaka kufungua msikatishwe tamaa,karibuni tufanye biashara.
Kula tano👊

Nawambiaga watu mara zote na siku zote,kama unajijua una presha za hapa na pale biashara pekee ya kufanya mtu kama huyo ni MIAMALA...simshauri mtu akalime mpunga aje afe na kifafa,simshauri mtu afuge aje afe na Kiwewe ila nitamshauri mtu Afanye MPESA NA TIGOPESA na BANKING

Biashara ambazo hela yako unaipata muda wowote na wakati wowote...hamna ugonjwa wakuifata hela yako kama ukifuga,hamna ukame utaifata hela yako kama Ukilima...Mkuu wewe umeonyesha hyo AVATAR ila na wish ningeonyesha mabalaa niliyofanya kupitia hiyo biashara.

Biashara ambayo hata kikongwe anaifanya na faida inaonekana mtu unaiponda?...ebu mwambie kikongwe alime au afuge na mkongojo wake uone kama ataweza! lakini huku kwenye MIAMALA kikongwe anapiga kazi ilimradi tu ubongo wake uwe vizuri.

Kikwazo pekee cha hii biashara ni MAJAMBAZI...ila ukishaweza miliki BANK sidhani kama swala la ulinzi wako binafsi litakushinda...Biashara hiii MAJAMBAZI ndio ukame na ndio magonjwa ya PESA.

tofauti na hapo SIJAONA BIASHARA YA KUNIFANYA NIACHE NINACHOKIFANYA labda atokee mtu aniambie ni biashara gani halafu tushindane kwa HOJA akinishinda ntaifanya.
 
Na wewe usiwe mjinga,aliyekuambia wakala mkuu anapanga commission ni nani!?? Commission unalipwa na kampuni ya simu moja kwa moja. Na kwenye hilo,wakala mkuu hana hata ushauri. Halafu hii ni biashara km biashara zingine tu,hulazimishwi kufanya. Mimi hiyo ni kazi,naendesha maisha. Na km unataka kuamini na kujifunza hii biashara inalipa njoo pm me nakupa number yangu,uje ofisini hata sasa hivi km unaishi dar. Mimi nauli nitakupa 10 elf ili uje hapa useme ukweli. Mkuu unapofungua biashara yoyote,lazima uzingatie location,kwamba hilo eneo hiyo bidhaa inahitajika! Wewe unashangaa mimi kupata milioni!?? Mwaka 2013 niliwahi kupata milioni 3 na laki 1 kwa mtaji wa laki 6. Hapo ilikuwa kabla hatujaanza kukatwa kodi ya zuio.
usitumie nguvu nyingi waelekeza halafu unaniumiza unavyotoa siri nnje mkuuu..waache waende FOREX tulia mkuuu kula maisha,hao wanamwamini ONTARIO tu ila wewe hawakuelewi...

Mil.3 mkuu hiyo kamisheni ni ya voda tu kwa huku kwangu..nadhani sina haja ya kutaja Tigo maana utakua ushapata Picha boss... unavyotumia nguvu nyingi waelekeza mwisho watakuona Tapeli.

WAACHE WAKALIME na KUFUGA sio wote lazima tufanye biashara MOJA...
 
Hii biashara kwanza inabidi uwe wakala wa mitandao yote na pia benki kubwa zote......lakini pia uichanganye na biashara nyingine kama duka au steshenari
uwakala wa mitandao yote na Benki unatosha kabisa mkuu..usichanganye biashara hzo hzo znatosha..Uza pesa achana na kuchanganya biashara ya pesa na Vitu..

ila kama utataka kupasuka changanya BIASHARA.
 
Miamala ya m 33 unapata kamishen ya laki 4, amakweli huwo ni unyonyaji
miamala ya 33M lakini mtaji wake sio 33M nina uhakika huo...sasa kama mtaji wako sio hiyo 33M wewe unaumia nini? Pokea fungu lako Kausha..endelea kutafuta pesa zaidi.

December Tigo walinitumia msg kua nikifanikiwa kufikisha miamala ya kuweka ya 1B ntapata bonus ya 5M...aseeee pale ndio akili ilifanya kazi,maana nilifanya mchezo mchafu sana 1B yao ikafika nikapata BONUS yangu 5M imenyookeana paleee.

Aje mtu hapa anibishie....

Halafu aje mwingine aniambie kazi gani nitafanya nipewe 5m bure bure tuuuuu bila jasho kutoka....
 
Back
Top Bottom