Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Piga ua Mitandao ya simu lazima ihakikishe faida yao kwa siku au kwa mwezi au kwa mwaka lazima ibakie pale pale au ipande, elewa hilo. Watafanyaje sijui, ila kwa vyovyote ni kuongeza tozo kwa mtumiaji. Hivi unajua Rostamu alivyo na nguvu nchi hii, hivi unajua wakubwa kibao ni wanahisa huko vodacom, kumbuka Msekwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi ya vodacom mpaka akatoa tusi maarufu la "mna wivu wa kike" kwa kumuonea gere nafasi hiyo. Kipindi hicho bado ni spika wa Bunge. Kumbuka kumbuka ndugu.Kwahio maboresho
Yanahusu kuongeza makato?
kwanini mnapenda kupotosha ninyi!!
Ktk m-pesa kulikuwapo kipengele cha kutuma kwenda mtandao mwingine?
Wakati wanafanya maboresho uliongezewa makato?
Kwa ntumiaji wa mara kwa mara wa huduma hizi
kitu maboresho ni chakawaida
Haijawai kufika mwezi mzima voda bila kuwapo na kitu hicho
Duhh, waswahili walinena kambale mkunje bado mbichi, akisha kauka hakunjiki! Sijui sie bado wabichi au tushakauka. Ila hili iltairudisha nyuma sekta hii ya Mpesa ambayo imekuwa ni gumzo hapa ulimwenguni. Sijui kama tutafika!INTRODUCTION
Kampuni ya simu ya VODACOM inasemekana leo imeanza rasmi mchakato wa kuongeza tozo kwa wateja wake wanaotumia huduma za MPESA kwa lengo la kukabiliana na gharama za uendeshaji ifikapo 01/07/2016. Serikali iliamua kutoza 10% ya kodi ya miamala, kiasi ambacho ukijumlisha na 18% ya VAT unapata 28%. Ili kuepuka kupata hasara, kampuni imeamua kuongeza 28% ya gharama za utumaji na utoaji fedha kwa wateja wote wanaotumia huduma za MPESA.
USHAHIDI
Zifuatazo ni meseji za KIKATILI ambazo zimetumwa kwa wateja wa VODACOM kuhusu “maboresho” ya huduma za MPESA:
MESEJI NO 1
Ndugu mteja, tunafanya maboresho ya MPESA hadi Jumapili saa 7 mchana. Kutuma pesa kwenda mitandao mingine nenda M-PESA > TUMA PESA > Chagua MITANDAO MINGINE . Time: 6/17/2016 3:01:40 PM
MESEJI NO 2
Leo saa 4 usiku hadi Jpili saa 7 mchana hautaweza kubadili PIN au lugha ya M-Pesa kupisha maboresho ya M-Pesa. Ukihitaji kufanya mabadiliko hayo yafanye mapema. Time: 6/17/2016 3:02:04 PM
TUTANYOOKA
Wale waliokuwa wanatuimbia kwamba “TUTAISOMA NAMBA” ngoja tuisome sote sawia. Huu ni mtego wa panya ambao utanasa waliomo na wasiokuwamo. Hadi ifikapo 2020 tutakuwa tumenyooka. Na bado……mabenki nayo yapo mbioni “kuboresha” huduma zao! Ngoja tunyooshwe hadi tunyooke.
INTRODUCTION

hizo meseji toka last week walikuwa wanazituma mbona tozo yoyote iliyoongezeka toka last week hadi leo,hayo maboresho yalifanyika ya last week ni yapi na ya this week ni yapi yatakayofanyika??wewe huwezi kuunganisha nukta? unaona mkia wa mbwa ulipo halafu unashindwa kuonyesha mknd ulipo? poor you!