Tetesi: Vodacom wameanza maboresho ya kuongeza tozo kwa miamala ya fedha

Tetesi: Vodacom wameanza maboresho ya kuongeza tozo kwa miamala ya fedha

INTRODUCTION
Kampuni ya simu ya VODACOM inasemekana leo imeanza rasmi mchakato wa kuongeza tozo kwa wateja wake wanaotumia huduma za MPESA kwa lengo la kukabiliana na gharama za uendeshaji ifikapo 01/07/2016. Serikali iliamua kutoza 10% ya kodi ya miamala, kiasi ambacho ukijumlisha na 18% ya VAT unapata 28%. Ili kuepuka kupata hasara, kampuni imeamua kuongeza 28% ya gharama za utumaji na utoaji fedha kwa wateja wote wanaotumia huduma za MPESA.

USHAHIDI
Zifuatazo ni meseji za KIKATILI ambazo zimetumwa kwa wateja wa VODACOM kuhusu “maboresho” ya huduma za MPESA:

MESEJI NO 1
Ndugu mteja, tunafanya maboresho ya MPESA hadi Jumapili saa 7 mchana. Kutuma pesa kwenda mitandao mingine nenda M-PESA > TUMA PESA > Chagua MITANDAO MINGINE . Time: 6/17/2016 3:01:40 PM

MESEJI NO 2
Leo saa 4 usiku hadi Jpili saa 7 mchana hautaweza kubadili PIN au lugha ya M-Pesa kupisha maboresho ya M-Pesa. Ukihitaji kufanya mabadiliko hayo yafanye mapema. Time: 6/17/2016 3:02:04 PM

TUTANYOOKA
Wale waliokuwa wanatuimbia kwamba “TUTAISOMA NAMBA” ngoja tuisome sote sawia. Huu ni mtego wa panya ambao utanasa waliomo na wasiokuwamo. Hadi ifikapo 2020 tutakuwa tumenyooka. Na bado……mabenki nayo yapo mbioni “kuboresha” huduma zao! Ngoja tunyooshwe hadi tunyooke.
Katika ushahidi wako ni wapi VODACOM wameandika wataongeza tozo ya miamala kwa 28%?
 
Hii kodi ya miamala hasa haifahamiki...
Jee ni kweli !
mimi nipo katika kutoa huduma ya bima , wateja wetu wengine hulipa kwa mobile money na kuwapeleka cover zao ma offisini jee ikianza kodi hii itakua makato yapo vipi ? Mbona haya eleweki ? Nini maana ya miamala ?
Natoa mfano mmoja kwa gari la private mteja wangu analipa
100,000 + VAT 18% (18,000) =118,000
Ananitumia hio 118,000 kwa Mpesa.
Jee hii premium ita tozwa tena 18% VAT ?
Jee hii itatozwa tena juu yake 10% ya kodi mpya ?

Hapa hesabu haziko sawa, ..ita ua huduma za mobile money..hakuna mteja atae kubali kulipa extra 28,000 juu kwenye bima yake....
Nadhani tueleweshwe vizuri ...na sheria iwe very clear . Nawajua watu wa TRA hii ikipita ni wagumu kujua fomula gani inatumika ...ni wazito sana kutafsiri sheria za kodi zao wenyewe.
Ila kama kodi hii itatumika kwenye base amount ..serikali imekosea sana sana na ikae ifikirie mara mbili...
Itasa babisha kutembea na cash jambo hatari kwa usalama.
Hivi msichoelewa nini?! Huyo mteja wako akikutumia hio 118,000 kwa mpesa/tigopesa kwa kawaida tigopesa/mpesa watamkata/kuchaji ada 2000[mfano] sasa hio 2000 ndio itakatwa 28% ambayo itaenda serikalini.
 
G1 to G2 m-pesa won't be the same again. Maboresho makubwa ya huduma hiyo. Sio charges kuongezwa. Sheria za mitandao hapa ndo unaona umuhimu wake mtu anaamua tu kupotosha jamii
 
Bodi heslb wanagonga
Simu wanagonga
Mkopo benki unagongwa
Mchepu unakugonga
Faza hausi ngooo
VAT bidhaani nkwadaah!
Atm nkwch
family ngoo
Paye twaaf,! Nk
Ukitoka hapo ulimi nje...
...wacha tuisome namba eee...
 
Sasa hivi itakuwa ni mwendo wa vibubu mwanzo mwisho. Nikitaka kumtumia Bi' mkubwa hela nitapampa kondakta wa basi kama zamani vile.
 
Hivi msichoelewa nini?! Huyo mteja wako akikutumia hio 118,000 kwa mpesa/tigopesa kwa kawaida tigopesa/mpesa watamkata/kuchaji ada 2000[mfano] sasa hio 2000 ndio itakatwa 28% ambayo itaenda serikalini.

Hapo sawa, lakini hii itafanya haya makampuni waongeze gharama zao pia ili wapate faida
 
Hii habari ni nzuri isipokuwa mtoa mada kaileta kipashukuna kama vile kaipeleka kwenye vibaraza vya mashangingi vya akina isha mashauzi......

By the way hayo sio maboresho bali ni maangamizi......
 
hapa kama kweli wanajiandaa kuongeza makato, inabidi regulator aonyeshe anafanya kazi kwa maslahi ya wananchi. maana tuliambiwa vodacom/mobile operator
wanakatwa kipato ambacho kilikuwa hakikawi kodi sio kwamba wameongezewa kodi
Mkuu usiwaami hata kidogo mbona walisema sukari iuzwe kwa 1800 bila kufanya utafiti kiwandani mfuko unauzwa bei gani na baadae wakasema sukari iuzwe 2300 yaani hawa wakikwambia tukutane tanga wewe usiende tanga nenda mtwara utawakuta
 
Sasa hivi itabidi tuache kutuma pesa kwa njia hizi. Mabasi yatahusika. Hi mitandao itatumika patakapokuwa Na dharura tu.!
Mbona mnakuwa wepesi kufanya judgement? Maboresho ni kuongeza gharama za kutuma/kutoa pesa tu? Nyie ndio mnafanya wasio na uelewa wa mambo kupanic, sasa kama nyie wenye uelewa kidogo mmeanza panic za namna hii, wale wa vijijini wawe vipi?
 
Kwahio maboresho
Yanahusu kuongeza makato?
kwanini mnapenda kupotosha ninyi!!

Ktk m-pesa kulikuwapo kipengele cha kutuma kwenda mtandao mwingine?
Wakati wanafanya maboresho uliongezewa makato?

Kwa ntumiaji wa mara kwa mara wa huduma hizi
kitu maboresho ni chakawaida

Haijawai kufika mwezi mzima voda bila kuwapo na kitu hicho
Hujaelewa, heb subir hyo tarehe utaelewa
 
Mbona mnakuwa wepesi kufanya judgement? Maboresho ni kuongeza gharama za kutuma/kutoa pesa tu? Nyie ndio mnafanya wasio na uelewa wa mambo kupanic, sasa kama nyie wenye uelewa kidogo mmeanza panic za namna hii, wale wa vijijini wawe vipi?
Wakati mwingine picha tu inaonesha sio hadi uambiwe.!
 
Watu wataanza kuficha hela makabatini sasa maana hakuna namna....
 
unakuta jitu linakuja kutetea wizi huu wa dhahiri wakati kila mmoja anaumia...mijitu mingine bhana!


Watu washangilia kwa ushabiki na wanawaona wakosoaji ni maadui bila kujua kuwa nchi inayumba na wananchi maskini wanaumizwa kwa serikali kuwalimbikizia kodi kila mwaka.

Mzunguko wa pesa utakua mdogo sana na wananchi wanazidi kuwa tegemezi kwa serikali na waoga wa kujiajiri.
Biashara zote za wanyonge zimekuwa kama ni za kuinufaisha serikali kisa eti elimu ni bure.
Binadamu ana mahitaji ya msingi ambayo ni lazima ajengewe au ajijengee uwezo wa kuyapata kabla ya mambo mengine yote.
 
HAWA WAIZI BADO WANAENDELEA NA UKARABATI WAO WA KUTUIBIA KAMA IFUATAVYO:

*********************************************************************

Ndugu mteja, tutaboresha mifumo ya M-Pesa leo jumamosi kuanzia saa 4:00usiku -kesho saa 7mchana. Ili kuepuka usumbufu, tafadhali fanya miamala kabla ya muda huo

Time: 6/18/2016 2:54:41 PM

********************************************************************
 
Watu washangilia kwa ushabiki na wanawaona wakosoaji ni maadui bila kujua kuwa nchi inayumba na wananchi maskini wanaumizwa kwa serikali kuwalimbikizia kodi kila mwaka.

Mzunguko wa pesa utakua mdogo sana na wananchi wanazidi kuwa tegemezi kwa serikali na waoga wa kujiajiri.
Biashara zote za wanyonge zimekuwa kama ni za kuinufaisha serikali kisa eti elimu ni bure.
Binadamu ana mahitaji ya msingi ambayo ni lazima ajengewe au ajijengee uwezo wa kuyapata kabla ya mambo mengine yote.
inasikitisha sana kuona kuna baadhi ya watu wanashabikia UKANDAMIZAJI huu huku wakifahamu fika kwamba tutaumia wote. ni sawa na mhalifu aliyehukumiwa miaka 5 kumtaja mhalifu mwingine aliyepo uraiani na akikamatwa wote wanafungwa miaka 5 kial mmoja.....kutaja au kushabikia kifungo cha mwenzako hakikupunguziii hukumu. katika sakata hili tutaumia wote pasipo kujali itikadi zetu za kidini, kisiasa, kikabila, etc.
 
Back
Top Bottom