Tetesi: Vodacom wameanza maboresho ya kuongeza tozo kwa miamala ya fedha

Piga ua Mitandao ya simu lazima ihakikishe faida yao kwa siku au kwa mwezi au kwa mwaka lazima ibakie pale pale au ipande, elewa hilo. Watafanyaje sijui, ila kwa vyovyote ni kuongeza tozo kwa mtumiaji. Hivi unajua Rostamu alivyo na nguvu nchi hii, hivi unajua wakubwa kibao ni wanahisa huko vodacom, kumbuka Msekwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi ya vodacom mpaka akatoa tusi maarufu la "mna wivu wa kike" kwa kumuonea gere nafasi hiyo. Kipindi hicho bado ni spika wa Bunge. Kumbuka kumbuka ndugu.
 
wapi wamesema wanaongeza tozo mazafanta.
 
Sasa hivi itabidi tuache kutuma pesa kwa njia hizi. Mabasi yatahusika. Hi mitandao itatumika patakapokuwa Na dharura tu.!
 
Duhh, waswahili walinena kambale mkunje bado mbichi, akisha kauka hakunjiki! Sijui sie bado wabichi au tushakauka. Ila hili iltairudisha nyuma sekta hii ya Mpesa ambayo imekuwa ni gumzo hapa ulimwenguni. Sijui kama tutafika!
 
unakuta jitu linakuja kutetea wizi huu wa dhahiri wakati kila mmoja anaumia...mijitu mingine bhana!
 

ktk post yako sioni sehemu waliyisema wanafanya marekebisho ili waongeze ghalama, au umesahau kukiweka? unafiki unawaua nyie watu.
 
Hii thread ni ya Uongo sana mabadiriko hayo hayahusiani kabisa na gharama za M-PESA ni vizuri kabla hujapost kitu ukajiridhisha na hiyo taarifa yako kuliko kudanganya watanzania wenzako kwa habari zisizo na uhakika kwani mabadiriko hayo yanahusu system ya M-PESA na si gharama ya M-PESA kama mtoa thread alivyobainisha kwanza alitakiwa kujua kwanini wamesema mabadiriko yataathiri kuchange PIN na vitu vingine, ingekua ni mabadiriko ya tariffs ingekua simple tu isingechukua muda kiasi hicho wadau upuuzieni huu ujinga wakusambaza habari za uongo. Wote upuuzieni uongo huu na kama kuna mtu alikua na wasiwasi basi jua hii taarifa ni fake na izimwe kama zilivyozimwa simu fake
 
Mtoa mada acha kupotosha uma. Hakuna uhusiano wowote kati ya meseji ulizopata na kuongeza tozo katika miamala ya Mpesa. Ni maboresha ya kawaida ya systems za Mpesa. Huawei is taking over.
 
Fear of unknown.Ivi izo msg zinazumza kupandisha viwango? Watu mnapenda kijitia preshaaaa
 
Hii kodi ya miamala hasa haifahamiki...
Jee ni kweli !
mimi nipo katika kutoa huduma ya bima , wateja wetu wengine hulipa kwa mobile money na kuwapeleka cover zao ma offisini jee ikianza kodi hii itakua makato yapo vipi ? Mbona haya eleweki ? Nini maana ya miamala ?
Natoa mfano mmoja kwa gari la private mteja wangu analipa
100,000 + VAT 18% (18,000) =118,000
Ananitumia hio 118,000 kwa Mpesa.
Jee hii premium ita tozwa tena 18% VAT ?
Jee hii itatozwa tena juu yake 10% ya kodi mpya ?

Hapa hesabu haziko sawa, ..ita ua huduma za mobile money..hakuna mteja atae kubali kulipa extra 28,000 juu kwenye bima yake....
Nadhani tueleweshwe vizuri ...na sheria iwe very clear . Nawajua watu wa TRA hii ikipita ni wagumu kujua fomula gani inatumika ...ni wazito sana kutafsiri sheria za kodi zao wenyewe.
Ila kama kodi hii itatumika kwenye base amount ..serikali imekosea sana sana na ikae ifikirie mara mbili...
Itasa babisha kutembea na cash jambo hatari kwa usalama.
 
wapi wamesema wanaongeza tozo mazafanta.
wewe huwezi kuunganisha nukta? unaona mkia wa mbwa ulipo halafu unashindwa kuonyesha mknd ulipo? poor you!
 
ALAFU KILA WEEKEND WANAFANYA MAREKEBISHO YA HUDUMA ZA M-PESA, PUMBAVU ZAO!!! NGOJA NIKATOE MASALIA YANGU NA NIACHANE NA HUDUMA
 
hizo meseji mbona hata last week zilitumwa unataka kutuambia toka last week bado wanafanya hayo maboresho??
 
wewe huwezi kuunganisha nukta? unaona mkia wa mbwa ulipo halafu unashindwa kuonyesha mknd ulipo? poor you!
hizo meseji toka last week walikuwa wanazituma mbona tozo yoyote iliyoongezeka toka last week hadi leo,hayo maboresho yalifanyika ya last week ni yapi na ya this week ni yapi yatakayofanyika??
 
VODACOM.....
SHIVACOM....
ALPHATEL.....
LOWASA......& ROSTAM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…