Tetesi: Vodacom wameanza maboresho ya kuongeza tozo kwa miamala ya fedha

Watu wataanza kuficha hela makabatini sasa maana hakuna namna....
itabidi turejee enzi za UJIMA za kutunza fedha kwenye michago na kufukia ardhini, hakuna namna.
 
G1 to G2 m-pesa won't be the same again. Maboresho makubwa ya huduma hiyo. Sio charges kuongezwa. Sheria za mitandao hapa ndo unaona umuhimu wake mtu anaamua tu kupotosha jamii
mpuuzy mkubwa! wewe ndiye CEO wa Vodacom? subiri ukamuliwe kama ng'ombe mpaka unyooke!
 
Hivi msichoelewa nini?! Huyo mteja wako akikutumia hio 118,000 kwa mpesa/tigopesa kwa kawaida tigopesa/mpesa watamkata/kuchaji ada 2000[mfano] sasa hio 2000 ndio itakatwa 28% ambayo itaenda serikalini.
acha upotoshaji wako wewe!
 
sasa sio TETESI tena....ni dhahiri makampuni ya simu yote nchini Tanzania yameongeza gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na tayari marekebisho hayo yameishasambazwa kwa mawakala wote. nimebahatika kuona nakala hiyo ila nilishindwa kuipiga picha na kuiattach humu kwa sababu simu yangu feki imefungiwa na TCRA. naomba mdau yeyote atakayeipata nakala hiyo aipige picha na kuitupia humu ila kila mtanzania aangalie maumvivu atakayopata. tafadhali administrators naomba mbadilishe status ya heading ya uzi huu kutoka kuwa TETESI na kuwa BREAKING NEWS. na bado.....mabenki nayo yataongeza gharama za kuchukua fedha na kuangalia salio very soon....stay tuned.....tuko pamoja katika maumivu haya hadi mwisho wa dahari!
 
Unatuma bila shida

Nilini ulikuta kipengele Tuma kwenda mtandao mwingine
hapo kabla?


1-Tuma pesa
2-Toa pesa
3-Nunua muda wa maongezi(japo kwa sasa kuna maboresho ya Vifurushi)

Kipengele cha kutuma mtandao mwingine kilikuwa namba ngapi hapo kabla?
je, sasa baada ya "MABORESHO" hicho kipengele cha TUMA KWENDA MTADAO MWIGINE unakiona? hebu tuambie kipo namba ngapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…