Vodacom wameanza wizi wa hela za M-PESA

Vodacom wameanza wizi wa hela za M-PESA

hamna kitu cha namna hio mkuu kifurushi ni chajero na breakdown ni hio! Voda naitumia sababu napokelea hela toka nje ya nchi ila kwa style hii ntatafuta mbadala tu! Huu ushenzi itafikia wakati tutaenda kuwavunjia computer zao vodashops! ili nao wasikie uchungu maana kama ndio style yao wanakukata na kukubambikia deni sintokubali!
Kama kweli kawashtaki ulipwe ma milion ya pesa kama fidia.
 
Piga simu customer care wakuangalizie zilivyoingia na kutoka kwa miamala mitano ya mwisho
Customer care kwani ipo sikuhizi? Kile kipengele cha mtoa huduma si wamehamishia whatsapp na facebook eti! Ukipiga 100 hamna option ya kukutanisha na mtoa huduma
 
Huenda wakati wa kununua kifurushi cha 500 ulibonyeza 0 mara 3 bila kuhakiki au 0 ya 3 ilichelewa kurespond mfumo ukasoma 5000
Ukinunua vocha ya elfu 5 lazma ikuletee ujumbe kuwa umefanikiwa kujiunga bando la 5000! Sasa corresponding text inasoma 500 unadhani hapo kuna nini kama sio janja janja?
 
Piga simu customer care wakuangalizie zilivyoingia na kutoka kwa miamala mitano ya mwisho
Nipe namba ambayo nikipiga nitaunganishwa na mtoa huduma. Maana ukipiga 100 unatangaziwa huduma zao tu sio kupatiwa mtoa huduma uongee nae.
 
Omba statement wewe miamala yote utapata kuiona na ayo makato utafahamu yamesababishwa na nn
 
mkuu songesha nafanyaga ila sijawahi chukua zaidi ya buku na ukiweka salio mpesa tu wanakata hela yao chap. So huwa sifugi madeni kabisa sasa hilo deni ambalo wao wanasema ni lipi?
Ungechek statement orodha ya miamala uliyoifanya tangu siku hyo pesa ilipobakia
Au ungepiga huduma Kwa wateja
 
Ukinunua vocha ya elfu 5 lazma ikuletee ujumbe kuwa umefanikiwa kujiunga bando la 5000! Sasa corresponding text inasoma 500 unadhani hapo kuna nini kama sio janja janja?
Hapo vodashop wanakuhusu kiongozi
 
Mkuu sijawahi kukopa wanioneshe hio list ya mkopo wao kama nahusika vipi sababu sijawahi kopa hela kwao na sidaiwi nao
Kama ungelikuwa na deni ungekatwa kwanza hio 500 ya kifurushi na ungepewa meseji ya balance ya deni lililobaki, kampuni haina haki wala uhalali wa kujichukulia pesa kwenye account ya Mpesa, sambamba na hilo ungalipaswa hapa useme hatua ulizochukua, majibu yao na hitimisho, use customer care services kwa simu na mawakala wa Karibu.
 
Ungechek statement orodha ya miamala uliyoifanya tangu siku hyo pesa ilipobakia
Au ungepiga huduma Kwa wateja
Huduma kwa wateja ni kama haipo ukipiga 100 hupewi option ya kukuunganisha na mtoa huduma. Inakuwa very useless ni mpaka uchat nao facebook sijui whatsapp. Nataka prompt answers sio kuanza kuchati na watoa huduma
 
Omba statement wewe miamala yote utapata kuiona na ayo makato utafahamu yamesababishwa na nn
Screenshot_2022-06-02-07-47-44.png
kaka siku ambayo nilitoa hio elfu 40 ndio siku ambayo salio lilibakia 15,000 kisha jioni nikanunua airtime ya 500 ndio kuhamaki imebakia elfu 10 then nikatoa 9000 usiku huo huo kwa hasira.

Hakuna muamala wowote wa tshs.5000
 
Tatizo ulikopa ukaingia mitini ukajua wamesahau, washarudisha chao.
Ni vema tukafikiri kabla ya kuandika. Amesema salio lilikuwemo hata kabla ya huo muamala. Akiwa na maana kwamba pesa imekatwa baada ya miamala zaidi kufanyika. na hata kama wanamdai huwa kuna meseji huambatana na ukataji wa salio, ilikuwaje wakakata kmyakimya? Mimi kuna siku nilitaka kusongesha ila sikufanikiwa. Ilikuja meseji yenye ujumbe "outgoing message"! Pesa sikuiona wala muamala haukufanikiwa, ajabu nilipoweka salio tu wakapita nalo kama upepo
 
Nipe namba ambayo nikipiga nitaunganishwa na mtoa huduma. Maana ukipiga 100 unatangaziwa huduma zao tu sio kupatiwa mtoa huduma uongee nae.
Piga 100, kadiri unavyoenda kwenye tatizo mahususi ndipo unavyokaribia kuunganishwa kwa simu na mtoa huduma. Usiishie kwenye menu ya kwanza, bonyeza namba ya huduma husika, bonyeza tena kuwa specific, bonyeza tena kuwa more specific mwisho utaambiwa "kuwasiliana na mtoa huduma, bonyeza n" where n is an integer representing the number of specific choice
 
Pole sana, kifurushi cha 500, gharama ya kukipata ni 2000.??
 
Back
Top Bottom