Vodacom wamenifanyia unyama, kesho naenda makao makuu na mwanasheria wangu.

Vodacom wamenifanyia unyama, kesho naenda makao makuu na mwanasheria wangu.

Hapo umefungua ya kariakoo na ya baltazar bado una lia
 
Vodacom kwa kula MB wanatafuna kama mchwa
 
Wamezd, alaf naona jf nayo inatafuna mb et sku hz natumia chrome au mm tu? Toka waanze matangazo
 
E
Nimejiunga na kifurushi cha SME package ya 50k kwa mwezi yenye GB 50 pamoja na dakika 2000, GB ziliisha juzi nikabaki na dakika ambapo mpaka ijumaa usiku nilikua na dakika 998

View attachment 3154486
Matumizi yangu kwa siku ya jana hayajazidi dakika 300 kwa mujibu wa call history.
Sijapokea sms yoyote kuonesha dakika kuisha na wala nisingeweza kutumia dakika 998 kwa siku ya jana,
Leo nimeamka asubuhi napiga simu naambiwa sina salio, baada ya kuangalia salio nakuta sina dakika hata moja
View attachment 3154516


Nimeongea na mhudumu wao yeye mwenyewe baada ya kukagua amekua shoked na kunipa zile sound zao za ombi lako litashuhulikiwa baada ya masaa 24 nimemwambia kauli hii sio ngeni jijini labda kwa wageni wa mji, kesho asubuhi sina kazi wafanyakazi watanikuta getini na sitoki ofisini kwao bila dakika zangu kuwepo kwenye simu



Sitakubali sound yoyote ile ya nenda dakika zako zitarejea otherwise wanirudishie pesa yangu.
Nenda Medson usikubali kuibiwa kizembe ,naomba baada ya kuwabananisha vizuri unipe majibu rafiki
 
Network pia ipo slow sana
Akili yangu ndogo inawaza tu....haiwezi kuwa mpango wa starlink sijui ya bwana Elon Musk kufanyia figisu voda wateja tuhame ikija..au wajiunge watengeneze kitu cha pamoja cha kuuzia wateja?
 
Back
Top Bottom