Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Mmeambiwa hiyo ni sauti yake kutoka ndani ndio ameisikiliza, na hii sio mara yake ya kwanza kuizungumzia hiyo "voice from within", sasa mnampigia kelele za nini?

Kama mnamuhumkumu PASKALI kuwa ana chuki kwa huyo aliyepo sababu ni mwanamke, basi nami nawahukumu nyie kwa mahaba yaliyopitiliza, kwangu hivyo vyote ni makosa, nyie wote hamfai kuwa majaji wazuri kwenye hii kesi.
 
Kwa maoni yangu, Rais Samia Suluhu Hassan anafanya vizuri sana. Hali ya uchumi inasababishwa na matatizo ya uchumi wa kidunia. Lakini anafanya vizuri naa Hana uchu wa MADARAKA. Aachwe, apewe nafasi AFANYE KAZI Kwa uhuru mpaka kipindi CHAKE kiishe.

Bernard Camilius Membe pia ataweza kuwa Rais mzuri sana baada ya Rais Samia kumalizwa muda wake.

Mwingine ambae atamrudisha mshikamano, ataondoka dhulma ni Mzee WA chuga AbdulRahman KINANA. Pia anafaa Sana kuwa Rais wa Tanzania.
 
Paskali mzee wa voices from within or ancestral umekuwa unatabiri mambo mengi na kugeuka ukweli. Mi nakuunga mkono lakini sababu zangu zinatokana na Mrumishi mmoja wa mungu kutoka Zimbabwe Dr Ian Ndlovu mtafuteni you tube msikilize prophecy zake kuhusu Namba wani.



Lakini kwa mtazamo wangu usemi wako wa ampishe Mwinyi halafu yeye aje agombee baadae sidhani kama itawezekana. Ukimsikiliza mtumishi huyu wa mungu anasema mheshimiwa kuna makosa ya kiutendaji atayafanya na asipokuwa mwangalifu qoute " People from within her party will try to remover her. Binafsi naona suala la Kupanda gharama za mafuta na maisha kwa ujumla halipewi uzito unaostahili na wahusika, Nafikiri pia issue iliyomngoa Ndugai na hawa wanaomsagia kunguni mwendazake kila kukicha kwenye majukwaa mbalimbali ikiwemo humu online hawana siha kwenye mustakabali kwa wananchi.

Binafsi napenda raisi wangu aendelee kutuongoza na mola amlinde na ampe hekima,akili zaidi na busara za kutatua changamoto zinazotukabiki wananchi moja kwa moja na si kutegemea mawaziri wakae vikao ndio waje watende. Na naamini Mama atatupa mkeka wa katiba mpya 2026 na hiyo itawaumiza zaidi wale chawa wa chama chake wasiojua kuwajibika,Kazi iendelee mama mpaka 2035.
 
Wanabodi
Haya mambo ya mtu kusikia sauti, sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, haya ni mambo ya ulimwengu wa Roho...
Mimi naona hiyo 2025 Hussein Mwinyi angekuja kugombea Tanganyika! Halafu huyu mama aende akagombee Zanzibar, au apumzike na kuwapisha wengine.

Maana ni ukweli kwamba kwenye hii nchi, bado tulikuwa hatujafikia hatua ya kumkabidhi mwanamke madaraka kutokana na aina ya Katiba tuliyo nayo, lakini pia uwepo wa mfumo dume katika mazingira mengi yaliyo tuzunguka.

Na binafsi naamini pia hata Mheshimiwa aliye tutoka, hakuwa na imani kama msaidizi wake atakuja kuichukua nafasi yake kabla ya muhula wake wa pili alioshinda kwa zengwe kukamilika!

Na madhara ya kutojiandaa kuwa na Rais wa jinsia ya kike ndiyo haya sasa! Watu wanafanya vile wanavyo ona inafaa! Wafanyabiashara wakubwa wamekuwa ni majeuri kweli kweli, kiasi watu wa chini wanataabika! Huku mama akiwa hana cha kufanya.

I wish angetumia hii miaka michache iliyobakia, kutengeneza mazingira bora ya uchaguzi huru na wa haki hiyo 2025! Na hakika akifanya hivyo, basi atakumbukwa na vizazi vyote hapo baadaye! Badala ya kulazimisha kugombea tena kwa mashinikizo ya wachumia tumbo wachache, na mwisho wa siku kuishia tu kukumbana na upinzani mkali kutoka ndani na nje ya chama chake.
 
Naona fukuto linaendelea ,mpaka Pascal ametumwa kutaka kusikia upepo ukoje.Mambo yanazid kuwa moto.Mm nafikiri katiba mpya ndio suluhisho.
Hayo wamepanga wenye mamlaka yatokee bt tetemeko ndo litabadili maamuzi hayo Ili akabidhiwe Freshd. Ni Rahisi kusema hakutakuwa na uchaguzi 2025 maana muda wa KATIBA mpya umefika. Mwenye mamlaka Kutoka JUU anakitaka kiti. Utawala wa kuchaguana sijauona. Same msg imesemwa na manabii zaidi ya watatu hivyo UMETHIBITIKA.
 
Paschal kusema Jiwe alikua hajui sio kweli sababu hata taarifa hiyo uliileta baada ya kutonywa na jamaa zako huko jikoni.

Hata kusema huyu mama unasikia sauti sio kweli kwani kwa mwenendo huu hata mtu mmoja wa hapo mezani kwenu alishalisema hilo humu humu.
 
Mwinyi hawezi kuwa Rais wa nchi mbili tofauti, kashakuwa Rais Zanzibar...Hawezi kuwa Rais wa Tanganyika.

Mwinyi hawezi kuwa Rais wa nchi mbili tofauti, kashakuwa Rais Zanzibar...Hawezi kuwa Rais wa Tanganyika.

Soma katiba basi hata kidogo
Huku usipositi kitu kama huna uhakika nacho
IMG_9272.jpg
 
Back
Top Bottom