Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huwaletea makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Mada ya leo ni a bit abstract, ambapo Nimesikia sauti ya Voices From Within ikiniambia JPM yuko Mbinguni kwa Baba, hivyo nauliza swali, jee wajua kuwa JPM yuko peponi, Mbinguni, Kwa BABA YAKE?

Why watu wengine waendelee kumshutumu, kumsakama na kumsimanga?. Kwa nini asiachwe ajipumzikie zake kwa amani!. Mtu ameisha tangulia mbele ya haki, kwanini watu waendelee kumsema sema kwa ubaya.

Mimi mwana jf mwenzenu ni Mzee wa Sauti za Ndani "the inner voice", unafanya kitu fulani na mara unasikia sauti from within ikikuambia jambo fulani.

Angalizo kuhusu Abstract Topics.

Issues na mtu akiisha kufa, we all knows what happens to the body, but roho huwa inakwenda wapi, no one knows for sure, hivyo tunategemea mafundisho ya dini zetu.

Kuna sisi dini za wana wa Nabii Ibrahim, Wakristo na Waislamu tumefunzwa kuhusu mbinguni, peponi, ahera, jehanam ya moto wa milele, na kuna siku ya mwisho siku ya hukumu ya mwisho ya kiama atakapo rudi Mwana wa Adamu, ambapo kutakuwa na ufufuko wa miili na uzima wa milele.

Kuna wenzetu wa Buddhism na Hindu ambao ni waumini wa karma, wao wanaamini kwenye after life na incarnation.

Hakuna yeyote awaye yote aliwahi kufa akayashudia hayo na kurejea duniani kututhibitishia mbingu ipo, peponi kupo na motoni kupo, wala waumini wa reincarnation no one can say for sure alikuwa nani before, zaidi ya ushahidi wa deja vu, hakuna uthibitisho wowote wa reincarnation Ila kwa vile na mimi niliishi India, I know for sure karma ipo and it's for real!

Hivyo hii mada ni mada ya imani, kama wewe huamini, please keep your faith nakuomba usibeze imani za wengine, ukijiona huamini, nakuomba jipitie zako kimya kimya, tuache sisi waumini.

Leo asubuhi nilikuwa nasoma michango ya wachangiaji wa bandiko langu hili. "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa!

Sasa ni wakati nasoma bandiko lenyewe, na naomba nililete hapa bandiko lenyewe lote kwa faida ya wavivu to follow links.
Ndipo nikaisikia sauti, voices from within kuwa JPM yuko peponi, ahera, mbinguni kwa Baba!

Kwa kawaida ya sauti, huwa inakuambia tuu kitu na haikupi sababu, hivyo naomba msiniulize sababu, hapa kazi yangu ni moja tuu kuwaeleza kile nilichosikia Leo ni JPM yuko peponi!

Hivyo baada ya kuisikia hiyo sauti nikamsikiliza tena JPM kwa makini sana katika video hii Nimejiridhisha bila chembe ya shaka, huyu mtu yuko mbinguni, peponi kwa Baba yake!, yuko na Baba yake!.

Hapa simaanishi kuwa JPM yuko peponi kwasababu he is perfect kama malaika, no!. JPM was a human being hivyo he is not perfect and no one is perfect, kilichofanya hiyo sauti ni despite his human mistakes JPM alitubu kabla ya umauti na kusamehewa dhambi zake zote na makosa yake yote, na ndio maana nimeambiwa, sasa he is in heaven now!.

Kwa bandiko hili, sasa ningewaomba watu humu, kutoendelea kumsakama, kumshutumu, kumsimanga na kuendelea kumsema vibaya, na badala yake tumwache apumzike kwa amani. Kama Mungu mwenyewe amemsamehe na kumuita kwake, who are you kuendelea kumsema sema vibaya?

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
PASKALI nimesoma andiko lako kwa tafakuri kubwa sana! Unaweza kuwa sahihi kwa sauti yako ya ndani ambayo iko juu ya uwezo wako kuweza kui control.. Lakini tukija kwenye uhalisia wa maandiko kwa imani ya mhusika ni kwamba wafu bado hawajafika peponi bali wote wako kaburini wakisubiri kiama ama mwisho wa dunia ambapo kila mtu atapewa hesabu yake
Niliwahi kuandika hapa kwamba zana ya pepo/peponi na Jehanum kuzimu iko pale kaburini, kwamba wale waliotenda mema roho zao ziko pale zimelala kwa utulivu lakini wale waliotenda mabaya (kwa tafsiri yoyote ya ubaya) roho zao zinahamanika na kuhangaika huko na huko, hiyo ndio tafsiri ya kuzimu/jehanum

Kwa upande wa karma.. Hii sote tunajua haikopeshi.. Tendo kwa tendo ..ubaya kwa ubaya na wema kwa wema.. Hivyo inategemea nani anaamini kwenye nini ndio atamuweka mhusika huko..

Kuna hili la mizania ya haki.. Hili hupimwa kwa matendo ya mtu mabaya na mazuri..Asili ndio huhukumu., hapa si dini bali ni asili, asili itakuchagulia njia yako kutokana na maisha uliyoishi kabla ya kifo

Hapa kuna ishu ya uumbaji ambayo kupitia mikono yake kwa tafsiri yoyote ile uumbaji huo uliumia, uliteseka na pengine kudhulumiwa haki ya kuishi.. Hapa ishu ni zile sauti zinazolia na kusononeka kwa namna yoyote ile.. Hapa ndio muunganiko wa mizania ya haki na asili hutokea... Kuna vitu viwili ambavyo kiimani vinapaswa kutendewa kwa tahadhari kubwa mno navyo ni uumbaji/uhai na ardhi.. Kwa waamini vitu hivi tumeonywa tusivichezee..!

LA mwisho ni hili la kuonya wadau wasiendelee kumsakama marehemu kwakuwa tayari alishafanya kitubio na yuko peponi..brother sidhani kama maneno yao yatakuwa na athari zozote kwenye hili.. Japo sasa kama ni kweli bado hata baada ya kufa watu wanaendelea kumsema vibaya basi lazima tutambue kuna tatizo kubwa mahali kuhusiana na yeye..!
 
NI sahihi kwa Jinsi alivyokuwa mzalendo naimani kaitendea haki nafasi aliyopewa ingawa Kuna mapungufu yaliyosababishwa na chama chake na watendaji wake aidha makusudi kumchafulia au na yeye akawa directly Masterminder...mfano lisu kushambuliwa na risasi why Kama Rais asitoe tamko zito kulaani
 
Ah ah, mzalendo hasiwe Mamako aje awe uyo mwizi?? Kojoa ukalale
 
Uko sahihi mleta mada. Marehem anapaswa kuachwa apumzike kwa amani. Ila matendo machafu au masafi yaliyogusa watu sio rahisi kuacha kusemwa kwa hisia tofauti tofauti.

Hivi unafikiri yule mwanachi aliyaefanyiwa jema akajengewa nyumba pale Mapipa utaweza kumnyamazisha vipi kumsema Marehem?

Ama yule mwingine aliyepotezewa mwanae hajui hata mwili wake uliko, au yule aliyetumikia Taifa kwa miaka mingi alafu miaka michache tu kabla ya kustaafu, anakuja mtu anamtumbua na kutaifisha mafao yake yoote kisa alitumia cheti Cha mjomba wake kujielimisha na kupata kazi, unadhani anaweza kujizuia kumtaja taja huyo Marehem?
 
Suala la wapi mtu anaenda baada ya kifo ni la kiimani zaidi. Ni kati ya Muumba wake na mhusika. Sio ndugu, Rafiki, jamaa Wala mpenzi wa marehem anajua au anaamua marehem anaenda wapi au anakua wapi baada ya kifo.

Cha msingi ni angalizo ulilolitoa tu kwamba Mtu akishafariki, aachwe apate kamisheni sawasawa na matendo yake.
 
Umeelewa babu Pascal Mayalla sio kuyomba yomba hovyo kama 🐒 siku ingine ukileta nyuzi za aina hii tunakupiga
 
Kusikia Voices from Within, hii hali hunipata pia. Nimewahi kusikia sauti ya mwimbaji maarufu (marehemu) akilia kwa uchungu, wakati huo nilikuwa nasikiliza moja ya wimbo wake. Ndipo nikajua nyimbo za kidunia zinaunguza kila aimbaye Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…