Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

This is one of the most ridiculous reason to believe in God.
 
This is one of the most ridiculous reason to believe in God.
Kama ilivyo haturuhusiwi kujiuliza kuhusu mwanzo wa Mungu, just God is Alfa and Omega. Vivyo hivyo, no ene needs and reason to believe God, mtu unazaliwa dini fulani, you just believe without any reason.
P
 
Kwani huyo Mwalimu wako ndiyo chanzo cha hii argument? Alibuni yeye? Hii ni Bertrand Russell ndiyo aliandika. Yaani wewe ni mjinga sana kwenye mambo mengi.
 
Kisayansi hakuna kitu kama roho au mtu kuwa na uwepo duniani baada ya kufa. Hiyo kitu hamna. Mtu akifa brain cells nazo zinakufa, na "mind" aliyokuwa nayo kwenye ubongo wake wakati anaishi nayo inakata. Bila ubongo hakuna "mind". Na ubongo ni cells zinakufa hata bado mtu yupo hai, achilia mbali akifa kabisa.
 
Kama ilivyo haturuhusiwi kujiuliza kuhusu mwanzo wa Mungu, just God is Alfa and Omega. Vivyo hivyo, no ene needs and reason to believe God, mtu unazaliwa dini fulani, you just believe without any reason.
P
Kuamini hata ukiamini mavi yako ni Mungu, sawa tu, hiyo ni haki yako ya kikatiba.

Lakini ukija hapa JF na kuanza kusema kuna Mungu, na mavi yako ni Mungu, tuyale tupate uzima wa milele, hapo itabidi tukuhoji ututhibitishie.

Sasa, wewe unakuja kutupa mavi tule, halafu tukikuuliza imekuwaje mavi yawe Mungu, unatuambia tuamini tu?

Lazima tukuone una some loose nuts somewhere.

Amini Mungu yeyote unayemtaka, sitakubughudhi.

Ukishaanza kuhubirihubiri, ushajitoa kwenye faragha ya kuamini Mungu, umejiweka wazi kuthibitisha na ku justify Mungu wako yupo kweli.
 
Upo sahihi asilimia 100 kaka Pascal.. Mambo ya rohoni hayatazamwi kwa macho ya mwili na nyama.. Wewe umesikia sauti ya ndani.. Ila wenye Karama ya kuona mambo ya Rohoni wameahaona kitambo kuwa The Great JPM amepumzika mbinguni kwa Baba Mungu..
 
Mshana wanachelewa wapi kukupa PhD ya heshima wanapewa wajinga wajinga tu akina msukuma?
 
sawa mtabiri manyota.. haya twambie na wewe utakuwa wapi ukinyakuliwa kama alivyonyakuliwa MEKO..
 
Pascal Mayalla said:
Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Je shetani naye anaweza kutubu akasamehewa? Je siku shetani akitubu na akaweza kusamehewa ina maana hakutakuwa tena na dhambi duniani?

Ona sasa ulivyonilazimisha kuuliza maswali ambayo sitakiwi kuuliza wala kupata majibu yake. Huko aliko shetani lazima hata yeye kashtuka, ama kashtukizwa?

Ndugu zangu nawaomba hizo sauti zenu from within ni vizuri kukaa nazo huko huko within. JPM kuwa peponi kunaweza kumfikirisha sana hata shetani mwenyewe!
 
Je shetani naye anaweza kutubu akasamehewa? Je siku shetani akitubu na akaweza kusamehewa ina maana hakutakuwa tena na dhambi duniani?
Mkuu Mag3, kiukweli kila nikikutana na mchango wangu kwenye nyuzi yangu yoyote huwa nafarijika sana kwasababu jf was meant to be home of great minds, wewe ni among the few real and true GT humu na una hoja za msingi sana.

Mwanzo shetani alikuwa malaika mkuu akaasi ndio akawa shetani, siku akitubu itakuwa ni furaha kuu mbinguni mwenye dhambi mmoja akitubu. Hili nimelizungumza vizuri hapa Malaika akijiunga na mashetani, anageuka shetani? Shetani akijiunga na malaika anageuka malaika?! na hapa Elections 2015 - Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?!
Ona sasa ulivyonilazimisha kuuliza maswali ambayo sitakiwi kuuliza wala kupata majibu yake. Huko aliko shetani lazima hata yeye kashtuka, ama kashtukizwa?
Haya ndio type ya maswali mimi ninayo yapenda.
Ndugu zangu nawaomba hizo sauti zenu from within ni vizuri kukaa nazo huko huko within. JPM kuwa peponi kunaweza kumfikirisha sana hata shetani mwenyewe!
Tumefunzwa tusihukumu tusije kuhukumiwa!, Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani! siku ya mwisho unaweza usiamini Osama, Saddam na Gadafi kuingia peponi halafu Bush, Blair na Osama ukawakuta motoni!.

Shetani watu wanamchora tuu vibaya, mnaweza kukuta triple 666 ni yule mzee wetu wa lile dhehebu kubwa kuliko yote!. Nasisitiza tusihukumu, no one knows alizungumza nini na muumba wake kabla roho haijachukuliwa.

Kuna watu mmeaminishwa ukifa unashukia kuzimu kusubiria ile siku ya kiama ya ufufuko wa miili na hukumu ya mwisho!. Its not!.

Ukifa tuu, mara baada ya mwili kupandishwa, unakwenda hukumuni na pale wanatumia mzani kupima mema na mabaya, mema yakizidi unaingia peponi hata kama ulifanya uovu mkubwa kiasi gani, ukafanya wema mkubwa kabisa kuliko ule uovu, unaingia mbinguni.

Siku za mwisho za Blaza alikuwa mtu mwema sana akitembea na mabulungutu ya minoti!, kusema ukweli kwa baadhi ya makabila hata usome vipi, ushamba haukutoki, tena zile za kutembea na mabulungutu ya fedha na kugawa zilikuwa ndio zangu!. Nilikuwa nikishuka kijijini kumcheki Maza, kijiji kizima kinajua!. Na huku mjini kwa ajili ya yale mambo yetu yale, kiukweli watu wamefaidika sana!.

Nikitolea tuu mfano kuwa ni mimi ndio nimempoteza Ben Saanane, Azori Ganda, Lujwabe na kuamuru zile pyu pyu za Lissu na ile miili kwenye viroba!.

Uovu huo unategeneza a negative karma forces ili kuufidia uovu wangu napata mapigo.

Nikaamua kubadilika kuwa mwema, nikaanza kutembea na mabulungutu ya minoti na kuwagawia masikini, fungulia mahabusu wenye fedha, samehe wafungwa hata wabakaji. Ile negative karma inakuwa reversed into positive, hivyo wema ulioufanya ni mwingi na mkubwa kuliko ubaya, then kwa vile ulikula kichwa, hivyo karma ni lazima ile kichwa, hivyo wakati karma inakula kichwa chako, uko kitandani unagalagala kupigania uhai wako, utatambua kuwa zile powers, pesa, madaraka, mamlaka, cheo, and everything is nothing!, unajutia uliyoyatenda, unatubu dhambi zako kwa mola wako, unajikabidhi Roho yako ichukuliwe, Mungu ni mwenye huruma na anasamehe 7×70!.

By the time Ziraeli mtoa roho anakufikia, anakukuta wewe ni clean kabisa, anaichukua roho yako, roho inaacha mwili, anaikabidhi kwenye mzani wa kupima mema na mabaya, mema yakizidi, naingia peponi!.

Hivyo Mkuu Mag3, nakuomba uniamini!. Hizi the voices within, some ni sauti yake YEYE mwenyewe and they never be wrong!, huyu jamaa yuko peponi!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Japo humu jf tunadharauliana sana, mimi nimeamua kila nikisikia sauti naileta humu, 2025 tutaheshimiana sana maana ni mimi nimeshauri Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! lakini nikaisikia hii sauti Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke, sasa tusubiri 2025 tutaheshimiana tuu!.

Unaweza kuziangalia baadhi ya trends zangu za kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba?. Shuhudia.., angalia zipi zimetokea!.
Vijikauli vidogo vidogo hivi kutoka kwa watu wa dogo who are nobody, sio vya kupuuzia, na mtu akiforce king, karma haina mswalie Mtume, wala hatujui au kujali nani ni nani, inakula tuu kichwa!.

P
 
Yes kabla ya kufariki aliongozwa sala ya toba tena na mlokole, ngoja niishie hapa siwezi Anika kila kitu, yupo zake mbinguni,
Mkuu Mnaso, asante kwa taarifa hii, tena inawezekana kilicho muingiza peponi ni hii sala ya toba toka kwa mlokole na sio yale mafuta ya mpako wa mwisho toka askofu Mkuu wa dhehebu lake.
Ukimuheshimu Mungu naye atakuheshimu, atakufanyia nafasi ya kutubu wakati wa kufa kwako. Mwenzetu alipata hiyo neema na haijalishi aliyofanya humu duniani.
Amen.
Yeyote anayechekelea kufa kwa huyu baba means hana moyo wa kusamehe na usiposamehe Mungu hatakusamehe, imeandikwa hivyo na ndivyo ilivyo. Kwa jinsi mioyo yenu ilivyo migumu mtakufa vifo vibaya vya kustukiza hata msipate neema ya kutubu.
Asante kuwaeleza watu hili!. Kuna wenzetu humu wana moyo wa ibilisi shetani Lucifer mwenyewe. Angalizo kwa Wana JF: Tuwaepuke "Prophets Of The Doom", kauli zao huumba!
Mwenzetu alijua kabisa anakufa na akakubali kuongozwa Sala ya Toba.
Naomba hili lifanye siri usiliseme tena, lina kiuka the right to privacy ya marehemu!. Kwa vile huyu ni Mkatoliki na amezikwa Kilatoliki, hii inamaani alianza kwanza kufanyiwa sala ya toba akaokoka, ndipo yakafuatia mafuta ya mpako wa mwisho ya Katoliki!, ila kilochomuingiza peponi ni ile sala ya toba na sio yale mafuta!.

Mimi pia ni Mkatoliki, kanisa letu lina vitu fulani vya kijinga jinga ambavyo havitendi haki.
  1. Zamani waligoma kufungisha ndoa kanisani na Muislamu, siku hizi wanakubali ila unatakiwa usile ostia bila kuungama kwanza!.
  2. Ukioa mtu wa dini nyingine yoyote isiyo Katoliki, watoto lazima wawe Katoliki.
  3. Mtoto akizaliwa nje ya ndoa wanagoma kumbatiza, mtoto anakosa gani?!.
  4. Ukiwa hushiriki Jumuiya ndogo ndogo, siku ukifa hawakuziki!.
  5. Ukifa huku ulikuwa na nyumba ndogo, wanakugomea kukuzika!.
  6. Ukijulikana umehamia makanisa ya wokovu unatengwa!, hivyo hiyo issue ya sala ya toba ifanye siri, ili tukikamilisha cannonization ya Nyerere akiishatangazwa Mwenye Heri, tuanze ya Mkapa kisha Magufuli!, siri hii ya sala ya toba ikitua on wrong hands, JPM will never be a saint!.
P
 
Kwani Kuna mtu kasema amepumzika kwa vulugu?.
Ndiyo!! wapo tena wengi tu! km hivi;

wanasema anasota rupango ya kuzimu kwa kuwapora watu haki zao kupitia vyeti fake!...hata km ilikuwa kweli ilipaswa walipwe haki zao sababu waliitumikia serikali na waliruhusiwa kufanya kazi hizo kwa mifumo yao mibovu!

Kuwakamata watu hovyo mpaka kusababisha hofu kuu wengine wakafa kwa hofu....Mfano mamake kabendera!.Ben saa nane!.....yule tajiri Muhindi! Gwajima na kundi lake nk!

Mayanga cons. comp ni yake!! ilivurunda sana na kuiba hela nyingi zasirikali maksudi!

Muongo muongo!! alisema hakopi kumbe alikopa kuliko yeyote!

Kuchukia watangulizi wake bila sababu za msingi! bila wao asingekuwa hivo lkn hakujali hilo wale walikuwa km wazazi wake, kwanza kabisa walikuwa ma-boss wake alipaswa kuwanyenyekea! km Mnangagwa anavo muheshimu Grace!.......Chiruba alikufa mapema bila heshima, sababu tu alimchukia Kaunda!

Kingine alikuwa na kiburi hakutaka kwenda kuchukua hirizi UNGA! sababu tu alilewa kutembea na Ma-body guard!

alikuwa mkurupukaji....anaweza akalala akakuota tuu! ujue kazi huna!..anakufukuza bila staha!.....''nendaaa, tokaaaa! tokaaa!!,,,kwendraaa! ....tumbafuuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…