Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Mleta mada ahsante sana...tusiishie hapa mkuu. Ata mashuleni na vitabu vinavyo wasema akina Adolf Hitler,Idd Amin, Pinochet,Mobutu, Hideki Tojo ,Benitho Mussolin kua watu wabaya na awakufaa kuiishii vipigwe marufuku maana watu hao walisha kufa ni Mungu tu ndiye mwenye kazi nao kwa sasa.
 
Ukichunguza kwa makini utagundua wote wanaomtukana JPM wana kasoro, nati zimelegea, ni za kukaza ili watambue kazi kubwa aliyofanya JPM.
 
Aliua, kuteka, kupora na kutesa watu bila sababu zozote za maana.
Mungu muweza wa yote akapindua meza.
Laana ya kijana wa makambako aliyepigwa na polisi, Tiss na jeshi kwa amri yake itamuandama popote alipo.
Mungu hasamehi waovu
Huyu alikuwa muovu
Imeandikwa.
Ezekieli 18:21-24
[21]Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa.
But if the wicked will turn from all his sins that he hath committed, and keep all my statutes, and do that which is lawful and right, he shall surely live, he shall not die.
[22]Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi.
All his transgressions that he hath committed, they shall not be mentioned unto him: in his righteousness that he hath done he shall live.
[23]Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?
Have I any pleasure at all that the wicked should die? saith the Lord GOD: and not that he should return from his ways, and live?
[24]Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.
But when the righteous turneth away from his righteousness, and committeth iniquity, and doeth according to all the abominations that the wicked man doeth, shall he live? All his righteousness that he hath done shall not be mentioned: in his trespass that he hath trespassed, and in his sin that he hath sinned, in them shall he die.

Mungu anasamehe maovu ikiwa utatubu kweli, haijalishi uko SEHEMU gani.
 
Wanabodi,

Why watu wengine waendelee kumshutumu, kumsakama na kumsimanga?. Kwa nini asiachwe ajipumzikie zake kwa amani!. Mtu ameisha tangulia mbele ya haki, kwanini watu waendelee kumsema sema kwa ububaya.l

Paskali.
Ndugu yangu ni hatari kubwa mno kuendelea kumshambulia Hayati Magufuli.
Mkuu Daisam ,naunga mkono hoja, mtu huna sababu kumshambulia mtu anbaye hawezi kujitetea tena nashauri aache kabisa maana huko aliko, akikasirika tuu ni anamshutua tuu YEYE, na mtu anaitwa fasta dakika sifuri!.
Pamoja na mapungufu machache ya kibinadamu ya Hayati Magufuli wakati wa utawala wake, asilimia kubwa ya Watanzania walimpenda mno na bado hajatoka mioyoni mwa Watanzania wengi.
Ni kweli, alitenda mema mengi makubwa mazuri kuliko mabaya na maovu yake, na kabla hajatwaliwa alitubu, akasalishwa sala ya toba, akapakwa mafuta ya Krisma, hivyo dhambi zake zote za hapa duniani, zikaondolewa na zikasamehewa na Mungu mwenyewe!.

Saa hizi hivi tunavyozungumza hapa, sii wengi wanajua mahali alipo sasa, sisi wenzenu tuliojaaliwa kujulishwa tunaomba tuwaeleze kupitia Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 
Aliua, kuteka, kupora na kutesa watu bila sababu zozote za maana.
Mungu muweza wa yote akapindua meza.
Laana ya kijana wa makambako aliyepigwa na polisi, Tiss na jeshi kwa amri yake itamuandama popote alipo.
Mungu hasamehi waovu
Huyu alikuwa muovu
Mungu unayemwamini wewe na Mimi tofauti ,Mungu nayemwamini Mimi anasamehe waovu tena wauaji mfano Sauli ambaye alibadilishwa jina na kuitwa Paulo
 
Mungu unayemwamini wewe na Mimi tofauti ,Mungu nayemwamini Mimi anasamehe waovu tena wauaji mfano Sauli ambaye alibadilishwa jina na kuitwa Paulo
Nikweli kabisa, Mungu wetu ni mwema, mwenye upendo, anayesamehe Saba mara sabini!.
P
 
Wanabodi,

Why watu wengine waendelee kumshutumu, kumsakama na kumsimanga?. Kwa nini asiachwe ajipumzikie zake kwa amani!. Mtu ameisha tangulia mbele ya haki, kwanini watu waendelee kumsema sema kwa ubaya.
Paskali
Mkuu Sexless , unless una uthibitisho, na ushahidi.
Japo JPM hakuwa malaika, ila pia hakuwa shetani ndio maana amekwenda peponi, na hivi tunavyozungumza hapa, yuko mbinguni kwa Baba yake!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Kwa sisi Wakristo, tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo, hivyo kwa mujibu wa sheria ya karma, mtu hata ukitenda maovu kiasi gani, ukaja kutenda mema mengi kuliko yale maovu, unaingia peponi!. "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Magufuli pamoja na uovu wake wote wa mwanzoni, baadae ilikuja kubadilika na kuwa mwema kama malaika by the time anatwaliwa, he was a saint!.

P
 
Mkuu Pascal siwezi kupingana na wewe kwa sababu aliwekwa na huyo MKUBWA kwa kusudi maalumu,lakini alifeli vibaya sana kwa sababu maalum pia,ila kilichosababisha akachukuliwa sijawahi kusikia mtu yeyote akikitaja. Sababu zote zinazotajwa ni chanzo lakini sababu kuu ipo.
 
Fumbo hili
 
Jana alikula lunch kwa Ben Saanane leo atakula Dinner kwa Azori Gwanda....
 
Pascal badili dini kaka, wenzetu waislamu wanaamini kuna shetani mmoja Mungu alimpeleka Mbinguni kuishi na Malaika...
 
Anayeleta ndiye ametwaa, anapoleta huwa hatoi sababu na anapotwaa pia huwa hatoi sababu, hivyo hakuna yeyote ajuaye for sure the exact reasons za kutwaliwa, ila pia tupo akina sisi, ambao kabla hajawa, tulisema kitu, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Aliposhinda uchaguzi ile 2015, tukasema kitu Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Baada ya mtu kulalamikia matokeo pia tukasema kitu Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!

Kabla ya uchaguzi wa 2020 tukashauri Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!

Baada ya kushuhudia rafu zilizochezwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, tukasema kitu Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Kwenye hizo hoja zote, pia ninaweka kitu kinachoitwa causes and effects, kwenye effects naweka the consequences.

Kilichomuondoa Blaza ni the accumulation of bad karma "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Yaani ni karma imekula kichwa!.

Uzuri wa karma, ukiishalipa deni la karma, deni linakuwa limelipwa, unatakasika, unaingia peponi, ndivyo JPM alivyoingia mbinguni.
P
 
Haaaahaaaa!,sawa mkuu,umeshinda kwa HOJA na tuishilie hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…