PreGE2025 Voices From Within: Tundu Lissu kuachiwa Huru kwa Nolle ya DPP, Serikali has no Interest kuendelea na Kesi ya Uhaini?

PreGE2025 Voices From Within: Tundu Lissu kuachiwa Huru kwa Nolle ya DPP, Serikali has no Interest kuendelea na Kesi ya Uhaini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wanabodi

Leo saa hizi,ni usiku mkubwa!,hii ndio mida wenye mamlaka ya kweli,huongea na watu wao,, achilia hawa wenye mamlaka ya kukasimiwa,hapa tunazungumzia mamlaka iliyo KUU ya Ukweeli, achilia hizi
mamlaka za kuja na kupita za dunia hii,hapa nazungumzia mambo ya ulimwengu wa roho,sio huu ulimwengu wa mwili!。

Nilikuwa nasoma JF, jinsi Tundu Lissu,anavyokuwa treated kule mahabusu,mara ghafla nikaisikia ile sauti ya voices from within,ikiniambia Tarehe 1 Julai,Tundu Lissu ataachiwa huru kwa Nolle ya DPP !。 DPP ataieleza mahakama Kisutu kuwa serikali haina nia ya kuendelea na kesi hii!yaani, the government has no interest kuendelea na kesi ya uhaini!.

Hiyo voices from within, pia imenieleza sababu za DPP
kuifuta hii kesi kwa nolle!,lakini kwasababu kwa mujibu wa sheria,DPP anapoamua kuifuta kesi yoyote kwa nolle,hawajibiki kutoa sababu yoyote kwa yeyote,na uamuzi wa DPP kutumia powers zake za nolle,uamuzi huo ni wa mwisho, final and conclusive, na hauhojiwi na mamlaka yoyote, hata rais wa JMT,hawezi kuhoji!,hivyo na mimi naomba nisizitaje sababu nilizoelezwa,kwa sababu fulani!na naomba msiziulizie!

Wakati mimi nikiandika hapa leo kuwa DPP ataifuta kesi ya Lissu kwa nolle,siku ya tarehe moja,isikute hata DPP mwenyewe,saa hizi,hajajua kuwa ataifuta hiyo kesi hiyo tarehe 1 Julai kwasababu yeye DPP bado hajaambiwa!

Hii sio mara ya kwanza kwa mimi kuambiwa kitu,na kupewa sababu,huku mhusika mwenyewe hajaambiwa, na mimi huja kusema humu bila kuzieleza sababu!。

Mfano mzuri ni ule mwaka 2014,nilipoelezwa Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na
nilielezwa sababu lakini sikuzieleza humu!。

February Mwaka 2015,nilimshauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein na nilielezwa sababu ila sikuzitaja humu!,ila hili lilitokea! Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Mwaka 2019 nilielezwa hili,Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... nikaelezwa sababu,sikuzitaja,likatokea!

Japo ni kweli urais wa Samia ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu,tupo akina sisi,tuliona toka 2017 na tukasema humu Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020

Kitu kizuri kuna baadhi ya ushauri wangu huwa unasikilizwa,mfano angalia tarehe ya uzi huu Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam kisha angalia aliteuliwa lini!

Au ushauri huu Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Hata mgombea wa CCM 2025, nilielezwa na nikaambiwa sababu,kwenye HII sauti ni sauti ya kweli nimeeleza tu nilicho elezwa,ila sijazieleza sababu!

Je hizi sauti za the voices from within ni sauti ya nani na lazima itokee?
Jibu ni ,the real voices from within ni sauti yake YEYE, ila kuna YEYE ambaye ndie mwenyewe,na kuna yeye ambaye siye YEYE, lakini anapenda ku pose kama YEYE
,na sometimes huji superimposed kama YEYE kumbe sio YEYE bali ni yeye!。

Hivyo kama hiyo sauti nilioisikia ni yake YEYE mwenyewe ambaye ni YEYE,then tarehe 1 Julai,Lissu anaachiwa huru!,ikitokea asiachiwe,then hiyo sauti sio yake YEYE,ni sauti ya yeye!。

Hivyo suppose ni sauti yake YEYE,na Lissu anaachiwa,je
,Chadema itashiriki uchaguzi hata bila ya reforms?.

Chadema wakikubali kushiriki uchaguzi hata bila ya reforms,wana bonge moja la fursa Pre GE2025 - Hata Kusipofanyika Reforms, 2025 CHADEMA Ina Fursa!, Ila They Are Just Too Blind to See!, Hawajitambui! No Election ni Utopia!. Wake Up!

Tundu Lissu akiachiwa huru,Chadema,wakaendelea kushikilia msimamo wao wa NRNE,I'm not sure what they are expecting to achieve kwa kususia uchanguzi,ila kitu ninachoelewa ni uchaguzi utakuwepo kama kawaida kwasabu Chadema has no ability,capacity wala capability to stop the election!。

Mungu Mbariki DPP aweze!
Mungu Ibariki Chadema to be able to do the right thing,
Mungu Ibariki Tanzania!

Paskali
Lord Denning anataka wakaze amna kushiriki uchaguzi
 
Mkuu, mbona unaandika vp vinavyojipinga ndani ya mada moja.?
lakini kwasababu kwa mujibu wa sheria,DPP anapoamua kuifuta kesi yoyote kwa nolle,hawajibiki kutoa sababu yoyote kwa yeyote,na uamuzi wa DPP kutumia powers zake za nolle,uamuzi huo ni wa mwisho, final and conclusive, na hauhojiwi na mamlaka yoyote, hata rais wa JMT,hawezi kuhoji!
👇
Isikute hata DPP mwenyewe,saa hizi,hajajua kuwa ataifuta hiyo kesi hiyo tarehe 1 Julai kwasababu yeye DPP bado hajaambiwa!
Umesema maamuzi ya DPP hayaingiliwi wala hayahojiwi, sasa vp tena hajaambiwa?
 
Hii Iko kwenye Additional Mathematics, huanzaga Form 3Chapter 9 ni Probability. Unatoa utabiri huku na kule huyu stakufacyule atapona tutapata dhahabu na kedha wa kadha. Katiba tabiri 100 ukiipata moja kwa mfano ya Magufuli uliyoweka baada ya Lowassa kwenda UKAWA, unajinadi kuwa utabiri. Hongera essentially kwa kujifurahisha ni haki yako Kikatiba mradi hauvunji Sheria.
 
Back
Top Bottom