feyzal
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 7,683
- 15,128
Volkswagen Polo Gti
Niko safarini kwenda Tunduma, niko na jamaa yangu kaniomba kampani tuongozane kwenye msiba wa mkwewe.
Wazee nimebadili mawazo yangu na leo nakubaliana kabisa na wale wanaosema Toyota ni Usafiri sio Gari ,huyu mnyama ana pepea speed 240 hahaha lakini hatujafika huko mwamba mwisho 140 kwake lakini kinachofanya niandike sio hiyo speed maana ni kawaida, bali jinsi ilivyo na nguvu na nyepesi wakati wa kusepa Huyu mnyama njiani hana anayembakisha na jamaa yangu anataka saa 1 asubuhi itukute Tunduma na hapa ndo kwanza tumeiacha Chalinze doh mniombe.
Nikiokota hela nitanunua mnyama wowote wa German si kwa hii raha yaani chuma kimetulia barabarani hakuna hata kudundadunda.
Nimemaliza nitakieni safari njema.
Mrejesho
Wakuu. saa 11 tunarejea Dar es salaam...ila kwa uchache niseme yafuatayo japo mimi si mjuvi wa masuala ya magari maana hata baiskeli sina japo nimeendesha tugari vya kugongea ila kulekule Dar.
Mbeya niliingia saa 9 usiku na Tunduma saa 12 kasoro dk 23,kutoka mbeya na Tunduma hatukukimbia sana ni mwendo wa kiistaarabu.
Nilichojifunza kwenye huu mnyama.
1. Inachanganya fasta yaani kutoka 0-100 humalizi sec 10(kwa haraka haraka) na kutoka 0-200 humalizi hata sec 20(nimekadiria tu hapa).
2. Ina balance mno hata ukipishana na lori hutajua japo ni kadogo.
3. Mfumo wake wa spilingi(hapa sijui tunasemaje mnivumilie) ni imara hata ukipiga shimo ni tofauti sana na hata mark x yaani husikii imetulia.
4. unaweza piga bumps kwenye 100+ lakini ukawa salama mara kadhaa jamaa alipiga bumps maana njia anaijua yote.
5. Hii gari mziki wake ni ule ule uliokuja na gari lakini unapiga poa sana kama umeweka mziki wa kununua wa wastani.
6. Siti ya abiria ya mbele iko poa haichoshi wala kuumiza miguu(nyuma sikukaa) na ni gari iko kisasa zaidi kiufupi nimenjoy safari...niliwahi safiri mara nyingi na magari mbali mbali kama Mark2 gx 110,verossa,Land cruiser vx ilikua na engine 1Hdt ,noah na kadhalika ila hii imenikosha sana .
7. Hii gari ni chuma halisi maana huo mlango ukifungua tu unajua tu hapa nipo kwenye gari ni tofauti kabisa na vigari vidogo vya toyota nilivyozoea.
8. Mfumo wake break uko vizuri hata ukiwa 100+ inawahi simama fasta.
Cha kuongezea hii njia ya Dar -Mbeya -Tunduma inabidi uwe makini sana hasa safari za usiku maana kuna ligi sio mchezo nakumbuka kipande cha Ruaha mpaka Makambako tulikua tunakimbizana na magari ya IT wale jamaa noma sana wanatembeza gari vibaya na hao ndio waliombusti jamaa kutembea sana maana kuna Chuma sijajua inaitwaje wanakaa abiria wawili tu ilitukata pale mbuyuni tukiwa 160 tulisumbuana nayo mpaka Iringa mjini tukaiachana pale kwenye beria lakini tulifika hadi 200 lakini ilikua mbele mita si zaidi ya 100 na hatukuvuka ikabidi jamaa akae nyuma tu ile ni sport car iko poa sana(naitafuta picha nikiona nitaijua ile gari).
Naanza safari yangu japo leo hatuko wawili tupo wanne mniombee.
Jioni Njema