Volkswagen Polo Gti huyu mnyama acha kabisa!

Volkswagen Polo Gti huyu mnyama acha kabisa!

View attachment 1511460
Volkswagen Polo Gti
Wakuu habari za jioni,

Niko safarini kwenda Tunduma, niko na jamaa yangu kaniomba kampani tuongozane kwenye msiba wa mkwewe.

Wazee nimebadili mawazo yangu na leo nakubaliana kabisa na wale wanaosema Toyota ni Usafiri sio Gari ,huyu mnyama ana pepea speed 240 hahaha lakini hatujafika huko mwamba mwisho 140 kwake lakini kinachofanya niandike sio hiyo speed maana ni kawaida, bali jinsi ilivyo na nguvu na nyepesi wakati wa kusepa Huyu mnyama njiani hana anayembakisha na jamaa yangu anataka saa 1 asubuhi itukute Tunduma na hapa ndo kwanza tumeiacha Chalinze doh mniombe.

Nikiokota hela nitanunua mnyama wowote wa German si kwa hii raha yaani chuma kimetulia barabarani hakuna hata kudundadunda.

Nimemaliza nitakieni safari njema.

Mrejesho

Hivi kumbe polo nae ana GTI version yake ,, Asante JF ndo nimejua leo
 
Mkuu Mlikuwa na Land Cruiser mkonga nje yenye 1hz au 14B au 2H kama ni gari za watu binafsi wengi Land Cruiser wanazonunua Msumbiji au Malawi ni zile zenye 2H.

Njia ya Mpapa kwenda Dar Porini mpaka Msumbiji kwenye machimbo kule wengi wanatumia Land Rover 109/110.

Land Rover kwangu mimi naona ilipewa heshima sababu ndio ilikuwa gari ya kwanza kutumika sana nchini. Ukilinganisha Land Cruiser yenye 1hz na hizo Land Rover. Cruiser inakupa kila kitu huwezi kukwama na ukitoka porini uwazi service.

Hiyo njia ya Mpapa -Dar Porini huko Land Rover nyingi sana, Land Rover kwa kazi za pori inaua sana bearing na bush. Huko Dar porini ukipeleka L/Cruiser utapigwa vita ya kila aina na wenye 109/110.

Land Cruiser mkonga naipa salute off road. Nakumbuka kuna siku tulienda Mbeya huko mlimani wanapolima viazi tukakodisha moja tukapanda nalo.

Aisee ile gari ni balaa
 
Hivi kumbe polo nae ana GTI version yake ,, Asante JF ndo nimejua leo
Yes polo kaleta Gti a.k.a mdogo wake na golf gti, used ukitaka mfano ya 2012-2014 CIF na kodi ya Tra ni kama chini ya m22 so utagundua ni cheap kulinganisha na golf Gti,pia engine yake ni ndogo cc 1300 ila sasa ina Nguvu kubwa na speed 280 ukikosea tu kanapaa ako.
 
Mkuu Skoda kwanza haijawahi kushinda WRC. Kwenye ERC wacha ziwe nyingi sababu zipo nyumbani kwao ulaya.

Ukweli ni Japanese wapo vizuri Toyota Celica GT,Subaru,Evo wamewahi kubeba WRC.

Hao wazungu unaowakubali wenyewe wanamheshimu mjapani.Ndio maana Ford Fiesta na Proto wao huko Ulaya saizi wanatengeneza Body Shell za Rally Car na injini wanaweka ya mjapani Mitsubishi Evolution 10.
Vipi toyota 86?
 
Back
Top Bottom