Wakuu habari za jioni,
Niko safarini kwenda Tunduma, niko na jamaa yangu kaniomba kampani tuongozane kwenye msiba wa mkwewe.
Wazee nimebadili mawazo yangu na leo nakubaliana kabisa na wale wanaosema Toyota ni Usafiri sio Gari ,huyu mnyama ana pepea speed 240 hahaha lakini hatujafika huko mwamba mwisho 140 kwake lakini kinachofanya niandike sio hiyo speed maana ni kawaida, bali jinsi ilivyo na nguvu na nyepesi wakati wa kusepa Huyu mnyama njiani hana anayembakisha na jamaa yangu anataka saa 1 asubuhi itukute Tunduma na hapa ndo kwanza tumeiacha Chalinze doh mniombe.
Nikiokota hela nitanunua mnyama wowote wa German si kwa hii raha yaani chuma kimetulia barabarani hakuna hata kudundadunda.
Nimemaliza nitakieni safari njema.
Mrejesho