Volkswagen Polo Gti huyu mnyama acha kabisa!

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128

Volkswagen Polo Gti
Wakuu habari za jioni,

Niko safarini kwenda Tunduma, niko na jamaa yangu kaniomba kampani tuongozane kwenye msiba wa mkwewe.

Wazee nimebadili mawazo yangu na leo nakubaliana kabisa na wale wanaosema Toyota ni Usafiri sio Gari ,huyu mnyama ana pepea speed 240 hahaha lakini hatujafika huko mwamba mwisho 140 kwake lakini kinachofanya niandike sio hiyo speed maana ni kawaida, bali jinsi ilivyo na nguvu na nyepesi wakati wa kusepa Huyu mnyama njiani hana anayembakisha na jamaa yangu anataka saa 1 asubuhi itukute Tunduma na hapa ndo kwanza tumeiacha Chalinze doh mniombe.

Nikiokota hela nitanunua mnyama wowote wa German si kwa hii raha yaani chuma kimetulia barabarani hakuna hata kudundadunda.

Nimemaliza nitakieni safari njema.

Mrejesho
 
Mkuu soma tena uzi vizuri tatizo sio spedd angalia chuma inavyoamka kuchanganya + imetulia barabarani mzee huyu mnyama balaa
Mzee baba kuna Toyota zinatembea huyo Vw Golf mchumba tu, uje ujaribu mziki wa Toyota Celica yenye 3s-gte.

Au Toyota yeyote yenye 1Jz-Gte iwe ni Toyota Supra,Mark 2,Cresta au Tourer V. Achana na hizo 1jz-ge au 1jz-fse zilizo kwenye Brevis.
 
Kifo popote hata kitandani.
Endeleeni kukimbiakimbia hovyo barabarani, mkifanya mchezo mtakua wageni wa Yesu jioni hii. Maafande tunasema mwendokasi unaua.

PS: mkipigwa tochi tukiwaambia leta leseni sio unatoa tu lileseni lako, weka 10k kwa chini ebo!
 
Achana na mjerumani kabisa, hawa jamaa magari yao ni next level. Sintosahau siku tuko safarini na Harrier matako ya nyani tuko spid mbaya mara naangalia kwenye kioo kuna MB G Class moja inaomba kupita nikambania.

Tumeenda nae ivo ivo anaibia apite mi namtishia bodi anatulia, tumefika sehem barabara ina vipara nikajichanganya nipunguze kulipisha lile shimo, mwamba kanipita vuup. Aisee yule jamaa sikuwahi kumuona tena njiani utasema alifika sehem akapaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…