VPL 8 Aprili 2015: Yanga Afrika vs Coastal Union

VPL 8 Aprili 2015: Yanga Afrika vs Coastal Union

Kwa waarabu nahisi timu itakuwa imetimia hata Coutinho anaweza akawa kapona...
Kwa kweli leo mmekomesha, hongereni sana kwa ushindi mnono. Angalizo; Msije mkalinganisha waarabu na hii Coastal Union la sivyo siku mkikutana nao hasa kwa msije mkashindwa kula bure.
 
Nimeingia mtaani na gari nimejikuta nimekanyanga mkaa makopo matatu ya 500/= kila mmoja nikalipa 2,000/= na kusepa. Mwenye mkaa kafurahi kuingiza kipato ghafla na huku mabaki ya mkaa nimemwachia, nimepaki, siondoki tena.

Ee Yanga mbona unatuingiza matatani?

Hahahaaa mkuu Makoye Matale umenichekesha sana.
Huyo muuza mkaa kama namuona alivyofurahi.
 
Last edited by a moderator:
Wanayanga mie ni mwenzenu ni mgeni humu ndani,na pia huku ndiko nikupendako,nikaribisheni ili tuwe kitu kimoja mpaka kifo.Mimi ni Yanga DAMU!!!

Karibu sana Wonderful.Usijali, jisikie kama uko nyumbani mitaa ya Twiga na Jangwani.
 
Last edited by a moderator:
Ahaaaaa!!kumbe ratiba ya hii gemu ilikua tar18.04.2015.
Nimemsikia Julio kwamba wachezi wake walikua kwenye mapumziko ya pasaka na jana ndio kapata ratiba ya game leo Dar!!!Sasa msijisifie tena,tena komeni kujisifia!!!

hayo unayajua wew sisi tunachojali ni ushindi tu mengine mtakuwa mnajijazia wenyewe
 
Mimi Boss mwenyewe ila leo nimechoka sana mwili i need to rest.

Mapumziko mema Ankal.Wakati mwingine ni vyema zaidi kujipumzisha ili kuupa mwili nafasi nzuri ya kujijenga pia kiakili.
 
Ahaaaaa ahaaaaa ahaaaaa hakika furaha yangu imezidi kipimo nitaludi tena baadae
 
Timu yenyewe costal union yaan unaua sisimiz kwa tofali alafu unaondoka huku unashingilia na kujisifia

As long as wanashiriki ligi kuu, lazima nishangilie... Real Madrid kuwafunga Granada goli 9 -0 mmeshangilia. Mimi kushangilia Yanga kuifunga Coastal Union tena ya Julio, imekuwa nongwa. Mwee makubwa hayo!!!!!!!!!!!
 
Kwa kweli leo mmekomesha, hongereni sana kwa ushindi mnono. Angalizo; Msije mkalinganisha waarabu na hii Coastal Union la sivyo siku mkikutana nao hasa kwa msije mkashindwa kula bure.

Tumesema hizi mechi za Coastal na MCC ni sehemu ya maandalizi kuwakabili hao ESS. Tuko makini Mkuu, yaliyowapata Platinum yatawakuta pia hao Waarabu.
 
Kwa muda mfupi niliotalii humu nimeweza kuwajua baadhi ya mashabiki wa MIKIA na WANA WA JANGWANI!!!
 
Julio anaxema kwa yanga hii kama leo ingekutana na simba bac simba ingepingwa 10 vijana wake wamejitahd wale yanga wako vzr nawapongeza huyo ni julio
DUNIANI WIKI HII

Washambuliaji waliofunga magoli mengi katika mechi moja

1. Ronaldo 5- Real Madrid-Hispania

2. Amis Tambwe 4-Yanga-Tanzania

Wengine malizia wewe.
 

Attachments

  • Surrender.jpg
    Surrender.jpg
    8.6 KB · Views: 199
Back
Top Bottom