VPL leo tar. 21/04/2015: Yanga vs Stand United

VPL leo tar. 21/04/2015: Yanga vs Stand United

hawa yanga sifa sana, yaaani wakiamua tu wanafunga wanavyotaka, mpaka waamue yaaani!
 
Stand wamekamia sana...wakati huo huo wanafanya sana makosa
 
Ndio akili za wabongo zilipoishia, wanadhani mfadhili atakuwa anatoa hela siku zote tu. Mpira ni uwekezaji, na uwekezaji unahitaji fedha nyingi. Bila vilabu kutumia potential zilizopo (washabiki) katika kuingiza mapato, tutaendelea kutegemea wafadhili tena wasiotabirika. Mwaka jana Yanga walilazimika kumpigia magoti tajiri mmoja aendelee kuwa kiongozi ili awe karibu na timu.

Wenzetu akina TP Mazembe na akina Etoile walifanya hivi; walikusanya vyanzo vya mapato (wafadhili, viingilio, wadhamini, mikopo) wakawekeza katika kusajili na kuandaa wachezaji bora kabisa kutoka pande mbalimbali za Afrika. Timu zao zikaanza kuingia nane bora, wakati mwingine nne bora, halafu mabingwa. Ukiingia nane bora kwenda juu unapata ruzuku ya mamilioni ya CAF. Ukiingia mara nne mfululizo unakuwa na hela za kutosha kusajili kwa kiwango kile kile kwa kutumia hela za CAF na wadhamini bila ya kutegemea vyanzo vya wafadhili na viingilio. Kuanzia hapo klabu inakuwa inajiendesha kwa faida na si rahisi kuporomoka tena kwani inakuwa na hela za kusajili akina Samata na akina Frank Kom.

Lakini kwa Yanga, mawazo yote ya hela yanaangukia kwa mfadhili, na bahati mbaya mara zote timu inatolewa raundi ya kwanza!

UlivyomaliIa ndicho ulichokusudia kukiandika...mengine yote ni mbwembwe tu...half time YANGA 2 Stand united 1
 
Tulia hapohapo,magoli mengine yanakuja.

Sawa kushinda mtashinda.. Ila inakuaje mchezaji wenu ancheza akiwa uchi? Hamna jezi za akiba? Au inshu ya kuwa Yanga kuna Kansa inaitwa "ukata" inawatafuna taratibu, tuanze kuamini?
 
Kwani kila kitu lazima ufanye comparison ya Simba na Yanga?

Reading between the lines uliyoandika ndio maana yake hiyo. Azam ni issue nyingine na hatuwezi kuwa judge labda baada ya miaka mingine mitano hivi. Kwenye financial fair play bado wapo kama Yanga na Simba tu. Hela ni ya tajiri sio ya club kama commercial entity.
 
Yaani niko ukumbini hapa Kashai........Kata yenye wakazi wengi bukoba Manispaaa ambako uchaguzi wa serikalimza mitaa hakuna hata mjumbe mmoja kutoka ccm alipata chansi yaani mzuka umewapanda washabiki yaani ni burudani tupuuu. Shabiki mmoja wa Simba kesha maindiwa na mashabiki wa yanga.....wako wanachanga kiingilio atolewe nje.
 
Back
Top Bottom