VPL: Simba v Prisons 28-02-2015

VPL: Simba v Prisons 28-02-2015

Prisons msikate tamaa,mpira dk 90 mbona hao mikia wanafungika 2 mungu yu pamoja nanyi
 
kumbe kuna tatizo kubwa sana klabuni

Kuna tatizo kubwa sana, na inasemekana wamerudi kama masaa 48 kabla ya mechi ya leo toka shinyanga, sasa hii nini tena! Uongozi wa Aveva sijui una malengo gani na timu.
 
Alafu kitu kingine hasa ndala mnatakiwa mtambue kuwa ktk VPL ushindani umeongezeka. Hivi mnajua mmetuacha michezo mingapi? Uwezekano wa Simba kuwa bingwa upo kabisa maana bado hamjacheza na sisi, hiyo mechi ni six pointer, tukiwafunga mnalo, na mnajua simba hata ikiwaga "mbovu" lakini kwa yanga wembe ni ule ule.

Hakuna uwezekano huo mkuu...Tuache kujifariji pasipo na sababu

Baada ya mchezo wa leo tutawazidi yanga game moja

Tutakuwa na point 23

Yanga wana point 31 na game moja mkononi

Assume yanga wanashinda hiyo game ya mkononi watakuwa na point 34 ...

Tofauti ya Point 11

Manake ni kwamba yanga wapoteze mihezo minne kwa kufungwa,

Thats totally impossible

Tuache kujifariji...Tushughulike na matatizo ya timu yetu
 
Na mwisho wa ligi hakuna pointi ambazo zinakuwa classified kwamba ni za ushindi wa kubahatisha.

Sawa...simba ni yetu sote....

Tunaitakia mema...Na long term solution ya matatizo
 
TANZIA🙁imethibitishwa)

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya C CM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar.
 
Hakuna uwezekano huo mkuu...Tuache kujifariji pasipo na sababu

Baada ya mchezo wa leo tutawazidi yanga game moja

Tutakuwa na point 23

Yanga wana point 31 na game moja mkononi

Assume yanga wanashinda hiyo game ya mkononi watakuwa na point 34 ...

Tofauti ya Point 11

Manake ni kwamba yanga wapoteze mihezo minne kwa kufungwa,

Thats totally impossible

Tuache kujifariji...Tushughulike na matatizo ya timu yetu

Pamoja na matatizo yaliyopo ya timu yetu, gemu ya leo tuna point 3 mfukoni, Yanga watakuwa wametuacha point 8, gemu za mkononi zisihesabiwe maana zinaweza angukia upande wowote.
Tuangalie na upande chanya, sio kushoto tuu. Tukisuluhisha matatizo yaliyopo sasa na mapema ndani ya timu, ubingwa unawezekana kabisa. Point nane ni michezo miwili kama sio mitatu.
 
Pamoja na haya matokeo, bado uongozi unatakiwa ukae chini na kutafuta njia ya kufuta tofauti za wanachama.
Alafu nilikuwa naangalia sports bar jana, kuna mtangazaji alisema kuwa ni tetesi tu, hakuwa na uhakika ila alipenyezewa kuwa simba iliwasili jana asubuhi toka shinyanga, sasa kama hizi ni habari za kweli, uongozi una matatizo zaidi ya wanasimba tujuavyo.

Mkuu hiyo sport bar ni ya kituo gani cha TV, maana kama ni clouds huwa kinarushwa jtatu saa nne usiku na kurudiwa jnne saa kumi jioni sasa wewe cha jana ulikitoa wapi na je ilikuwa ni live au recorded?
 
Kuna kipindi walikuwa na kipindi pia ijumaa.
 
Back
Top Bottom