mkolaj
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 3,023
- 1,089
Michezo ni undugu, urafiki na afya bora.Mkuu usijali, mavi ya kale hayanuki. Hata mimi niliingia katika mtego wa shetani wa kukuchukia wewe kwa lugha zako za kiasherati. Mimi nilishakusamehe toka zamani sana, nasikitika kuona wewe bado una kinyongo na mimi. Mpira ni mpira tu mkuu, usitufanye tukagombana na huku hatujuani hata kwa sura, ni hasara kubwa sana kwetu endapo tutakubali ujinga wa kugombana hapa jukwaani.
Hebu fikiria siku moja tukikutana nami nikajitambulisha kwako kuwa mimi ndiye Makoye Matale na wewe ukajitambulisha kuwa ndiwe grafani11, endapo tutakuwa na ugomvi hapa jukwaani hali itakuwaje? Lakini kama hatuna ugomvi, hali itakuwaje pia?
Last edited by a moderator: