Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
WAKATI wanachama na mashabiki wa Simba wakianza kusahau machungu ya pilikapilika za kugombea jezi mpya za klabu hiyo, mwenye dili na uzi za Simba, Fred Ngajiro ‘Vunjabei, amevunja ukimya na kufichua hasara ya kupoteza Dola 150,000 (zaidi ya Sh349 milioni).
Vunjabei alisema hasara hiyo imetokana na kubadilisha mfumo wa jezi za awali baada ya kubadilishwa kwa mdhamini kutoka SportPesa na kuwa M-Bet.
Mfanyabiashara huyo alisema, mkataba mpya ulipokuja alikuwa ameshadizaini jezi za mdhamini wa awali, hivyo kumtia hasara ya kiasi hicho cha fedha za kuweka mdhamini mpya.
“Simba waliponipigia simu kuniambia juu ya kusitisha uzalishaji wa jezi kutokana na mkataba mpya basi ikanibidi na mimi nipige simu zoezi lisitishwe jambo ambalo limefanya jezi zichelewe,” alisema Vunjabei na kuongeza.