Vunja mifupa ngumu bado meno ipo, Makonda sasa umekwiva

Vunja mifupa ngumu bado meno ipo, Makonda sasa umekwiva

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Nimesikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda. Hakika ana mabadiliko makubwa sana na amezungumza kwa weledi. Amejitahidi kuelezea na kuangazia maswala ya kiuchumi na miradi ya maendeleo inayoendelea Arusha kwa Sasa.

Ameongea kiume na kwa haiba ya uongozi na hakika ana mabadiliko makubwa sana katika maongezi yake.

Ameandaa sherehe na anachinja ng'ombe zaidi ya miambili kuandaa chakula choma na kuwakutanisha wakuu wa taasisi na wawekezaji wa Arusha.

SWALI langu Je wazee wastaafu ambao ni wenyeviti wa bodi wataweza kula nyama choma ngumu ama watavunja meno tu?? Nashauri pia awachemshie wazee supu wale nyama laini na michuzi.

Soma Pia: RC Makonda aandaa hafla ya Wakuu wa Taasisi za Umma na Wafanyabiashara Arusha

NB: Hapo mwisho pazingatiwe
 
Napenda tu kukwambia ipo siku utamuona Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara akishika nafasi moja kati ya

Urais

Umakamu Wa Rais

Uwaziri Mkuu .

Shika maneno haya na utakuja kuyakumbuka baadaye baada ya kutokea.
Kama akiukwaa urais basi namuomba wazee wetu wastaafu waachwe wapumzike na wajukuu na wasirudishwe kazini kwa kisingizio cha uenyekiti wa bodi.. angalia Sasa wakila nyama ngumu wakavunja meno itakuwaje?
 
Watapewa nyama laini laini kama Maini .
 
Napenda tu kukwambia ipo siku utamuona Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara akishika nafasi moja kati ya

Urais

Umakamu Wa Rais

Uwaziri Mkuu .

Shika maneno haya na utakuja kuyakumbuka baadaye baada ya kutokea.
Ndoto za mchana. Mungu alishapanga yake kuhusiana na uongozi wa taifa lake tangu kitambo. Amesikia kilio Cha watu wake.Tunasubiri wkt wake utumie.
 
Back
Top Bottom