kindikinyer leborosier
JF-Expert Member
- Jan 6, 2018
- 456
- 833
Kipindi Cha makange umbwe ilifika hatua tukaiita college kulikua na ufree uliopitiliza, migomo isiyoisha, walikua kupigwa ilikua ni mwendo wa uharamia, watu mda wowote wanaenda kulewa mpaka wanazima wanaletwa shuleni hawajielewi
Lyimo nae shule ilikuja mshinda tatizo ni wapigaji wa hela, shule ikawa na matatizo mengi kwa migomo ikawa kila uchwao
Kipindi hicho form one mpaka six sare moja ya kaki ukija mgeni ukikaa vibaya unaingizwa mjini sababu huwezi tofautisha uyu ni form one au form four
Umesahau ile fujo ya mwaka 2003 mlipokuja mpirani pale Umbwe mzee.?Aiseee!! lyamungo niliyosoma mimi 2005 rudi nyuma,ilikuwa ya watulivu japo imejaa wavuta bangi kule shamba la kahawa( research) na wapiga chuma(gym) pale dom la lumumba kwa chini.Tulikuwa chini ya mkuu wa shule wa kuitwa burreta,mkuu wa shule alikuwa mbabe sana.
unafikiri ni kwanini
1 umriunafikiri ni kwanini
Iwe oli mulokozo CBG, au Edi CBG[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]Nawakumbuka sana hawa vijana! Kuna jamaa alkuwa anaitwa charles(2012-2014 HGL) alikuwa anajenga hoja kama zitto! Sijui yu wapi now?
Tatizo idadi ya wanafunzi, wakati tunasoma Kuna wanafunzi kama 2000, munalala wanafunzi wawili kitanda cha futi 2 na nusu, matundu ya vyoo hata 10 hayafiki Maputo huko. Kula chakula vurugu, prepo vurugu, darasani vurugu, kwenye mpira vurugu, kila sehemu vurugu.
Vyoo vya mabweni vya kisasa vina space unakuta vimefungwa na wababe wanaishi huko, Dorm leader na marafiki zake.
Just imagine mamia ya wanafunzi wanakaa kwenye bwalo la shule Wana Angalia Ngono, hizo guts wanazitoa wapi? Viongozi wenyewe wa shule wanachaguliwa kwa kuangalia nguvu na influence, wengi nguvu nyingi kichwani sifuri. Unakuta mtu ana miaka kama 20 ama 30 hivi yupo form 1, hajielewi hata kidogo.
Unasoma shule mpaka unamaliza Kuna class mate huwajui, kila siku unakutana na sura mpya.Nakumbuka kidato Cha pili tulipiga pepa tupo Mia Saba na ushee.. kidato Cha Kwanza tumeanza na jamaa Wana umri wa miaka 25 /28 darasa letu pekee Lina mikondo mitano Cha ajabu zaidi mabweni yalikua manne tu yenye uwezo wakubeba wanafunzi 160 tu kwakila bweni .
Boys kawaida sana hiyo, ikiwa tu kitanda cha deka kinakaa juu ya dali.Sembuse kukaa na mapanga.Hii shule mpka wanafunzi mnapanga yoye hayo uongozi uko wapi😳😳😳
Hujafikiria juu ya Golikipa SHABANI aliyeugua mpka kufa 2008?Tuliandamana mpka kwa mkuu wa mkoa...tukasambaratishwa ktk shule za kata..mpka leo sidhani kama kuna o level pale Lyaboys
Maroho hayo bifu la wamachame na wakibosho.. zile dongo za wamachame na wakibosho zipo vitaniSuper memories mdogo wangu..
Ila Umbwe ipo Wilaya ya Moshi vijijini na Lyamungo ipo Hai
Unasoma shule mpaka unamaliza Kuna class mate huwajui, kila siku unakutana na sura mpya.
Manase huyo, anarusha ugali mita kadhaa usipodaka imekula kwakoSure mkuu. Kuna tukio moja headmaster. Alipokelewa beg lake na mwanafunzi alafu akatembea nalo mazima . Lyamungo ilikua vituko sana, mpishi mwenyewe alikua mbabe sana ukijichanganya huna bahati,anatembea na sime maana wanafunzi hawatabiriki muda wowote wanakugeuka.
Mkuu unazimia kwa njaa ya siku 1 tu ? Dah kweny harakati za kibandidu watu tunakaa siku 3 hatujagusa ktu had ukinywa maji unaskia utumbo unavyoumaUboyzini acha tu
Nimesoma Olevel Ihungo Boys Bukoba tuligoma wkt sina hela na tukawa haturuhisiwi kula, tukaenda kimya kimya uwanja wa mayunga pale bkb town, tumefika tu defender zikaanza kuzunguka uwanja. Hamna kutoka kwenda mtaani na ilkuwa usiku na asbh sikuwa nmepata breakfast na mchana nikawa nimepinga pass ndefu, ilipofika saa 6 usiku nikazimia kwa njaa rafiki yangu Edmund akanipa maandazi mawili(Mungu ambariki) roho ikarudi[emoji1787][emoji1787].
Musoma tec Vs Songe ndo ilikua kisanga ingine fujo zimeisha songe walivyo baki girls peke yao Tec wakabak boys uhasama ukafakulikuwa na hizi battle na ilikuwa ni balaa
1. Milambo Vs Tabora Boys
Milambo washatembeza sana kichapo kwa Tabora Boys mpaka Tabora Girls tena Tabora Girls walienda kumwaga hadi Divi.
2. Musoma Tech Vs Mara Sec
hii ilikuwa vita zaidi wa Wanchari na Wairege,wakikutana lazima kiumane
3. Tambaza Vs Azania
battle la watoto wa mjini hili
4. Musoma Day ( Morembe) Vs Songe
5. Zanaki Vs Jangwani
battle za kitaaluma
1. Mzumbe Vs KIBAHA vs Ilboru
Kuna kichwa kilikuwa kinaitwa LyaruuSure mkuu. Kuna tukio moja headmaster. Alipokelewa beg lake na mwanafunzi alafu akatembea nalo mazima . Lyamungo ilikua vituko sana, mpishi mwenyewe alikua mbabe sana ukijichanganya huna bahati,anatembea na sime maana wanafunzi hawatabiriki muda wowote wanakugeuka.
Alistaafu siku nyingi. Kipo kichwa kingine kilikuwa kinaitwa Lazaro. Saa moja asubuhi keshalewa saa nyiiingi.Manase huyo, anarusha ugali mita kadhaa usipodaka imekula kwako
Naukumbuka huu Wimbo ila tune nimesahau . Walikuja mawenzi wakaka wa umbwe wakauimba asee maeneji kama yoteeTukitaka kwendaa mbelee bwana haaa ,haa shetani atuziaa......mkemee mkemee ebwaana.....ebwanaa mkemee..
Meku damu ya mtu hutesa sana,waliohusika lazima wanapata msongo wa mawazo mpka leo hiiYap, alijikuta captain akaendelea kurusha mawe watu wakaanza kumkimbiza akafika uwanjani alipigwa mtama hapo ikawa kila aliyemkuta anapiga sio mwenye fyekeo, mwenye mpini, mwenye jiwe, wengine walimkanyaga dah so sad mpaka akakata kamba. Kuna mwenzake nae alikimbilia nyumbani kwa mpishi alichomolewa akaletwa pembeni ya mwenzake. Nae alikula kichapo ila wakamuonea huruma. Akapelekwa KCMC ila nadhani alipona. Na kama alipona nadhani alipata kilema cha maisha.
Sent using Jamii Forums mobile app