Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Mdogo wangu viti vipo nilipita pale 2013 kumpeleka dogo nikavikuta baadhi maeneo ya karibu na nyumba ya Yule Maza muuza maandazi.

Sema mimi kama mzaliwa na mkazi wa DSM kwa experience ya maisha haya mpaka sasa niseme tu watu wa mikoani wana roho ngumu sana.

Kupigana mapanga,mtu kumwagiwa jagi la uji ni kawaida sana dah halafu kuna manzi alijichanganya wakampiga ambush watu kama 10+ wakamtupa Kwao mlangoni aisee watu walikuwa wanalala mbele na wauza vyakula ila Yule mzee muuza chai pale nje watoto wake watu walikuwa wanakaa nao mbali.

Watu wanatunga maswali wanawapelekea watoto wa somsom wanawadanganya ni necta na kupita nao
Yule ulomy mzee wa katizi,alishakunywaga damu ya mtu...ni noma
 
Kipindi Cha makange umbwe ilifika hatua tukaiita college kulikua na ufree uliopitiliza, migomo isiyoisha, walikua kupigwa ilikua ni mwendo wa uharamia, watu mda wowote wanaenda kulewa mpaka wanazima wanaletwa shuleni hawajielewi

Lyimo nae shule ilikuja mshinda tatizo ni wapigaji wa hela, shule ikawa na matatizo mengi kwa migomo ikawa kila uchwao

Kipindi hicho form one mpaka six sare moja ya kaki ukija mgeni ukikaa vibaya unaingizwa mjini sababu huwezi tofautisha uyu ni form one au form four
Nakumbuka binti yake makange kwa jina Nakiete,Somsom sec....Mara ya mwisho nilimuona Makange Arusha,kachoka sana.
 
Jamani Shule za Boarding za Enzi hizo ilikuwa Raha Sana. Shule zenyewe zilikamilika. Mzungu alisema na tujenge Shule na ikajengwa Shule kweli. Mabweni Safi, Dining hall yenye kila kitu, Kitchen, Classrooms, Conference room, Chapel, Laboratory, infirmary, viwanja vya Michezo, Gardens, Staff rooms, Headmistress/ headteacher room, library, store, toilets and bathrooms zenye showers na flash toilets, fire place darasani Eneo la baridi, vioo vya Lucas au vya kufunga na kufungua, Sewage System Bora kabisa. Daaah nazikumbuka hizo Shule chozi hunitoka zilivyoharibiwa na Sisi.
Mkuu umesahau sweeming pools,makanisa na misikiti...yaani hizi shule unachoka
 
Umbwe na vyoo vya shimo. Tena vimejengwa kinyume cha miongozo ya ujenzi. Vinajengwa mlimani afu mabweni bondeni kha! Any way ila Ile shule ni ni mti safi hata huku nje tunatambuana na kusalimiana kama mti safi.
Poleni mlioshuhudia vifo vya mapigano at that age.
 
Ni bahati pia kuwa nilisoma Lyamungo Sec A Level...ni miongoni mwa mwanafunzi aliyekuwepo kwenye form five ya kwanza mwaka 2001, July. Mwalimu Mkuu alikuwa Bureta na Nidhamu alikuwa Mwalimu Shoo.
Mwenyew nilikuwa hapo miaka hiyo
 
Jamani Shule za Boarding za Enzi hizo ilikuwa Raha Sana. Shule zenyewe zilikamilika. Mzungu alisema na tujenge Shule na ikajengwa Shule kweli. Mabweni Safi, Dining hall yenye kila kitu, Kitchen, Classrooms, Conference room, Chapel, Laboratory, infirmary, viwanja vya Michezo, Gardens, Staff rooms, Headmistress/ headteacher room, library, store, toilets and bathrooms zenye showers na flash toilets, fire place darasani Eneo la baridi, vioo vya Lucas au vya kufunga na kufungua, Sewage System Bora kabisa. Daaah nazikumbuka hizo Shule chozi hunitoka zilivyoharibiwa na Sisi.
Aisee kweli kama mm nilisoma Mwenge Singida, ukifika shule yale majengo yalijengeka kweli, lakini sasa hivi yalivyochakaa mpaka aibu
 
Ulisoma Ubwe kumbe dooooh mm ni
Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache

Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.

Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.

Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.

Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.

12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.

May the Lord grant us his Mercy.

Huwa napenda ku-reference hii ishu na nyimbo ya Dr Dre ft Snoop Dogg - Lil ghetto boy

lishuhudia A to Z lile tukio
 
Back
Top Bottom