Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Kimata kinatuka ilikua O level na A level. 2008 ilikua ya viongozi na wanafunzi (Mussa Mdee unamkumbuka?). Ya shabani ndo ilifanya tukatembea mpaka kwa mkuu wa mkoa
Wewe unachanganya mafile. Dogo shabani alifariki 2006 na ile vita iliewa jina la stone war 3. Vita iliyowaondoa form 3 na form 4 ilikuwa ni KIMATA-KIMATUKA WAR 1 hi ilikuwa mwezi wa 2 hivi na sababu kubwa ilikuwa ni ugomvi kati ya viranja na raiya
 
Nyama zililala zikaliwa kesho yake, balaa lilianzia hapo. watu wakaendesha mbaya kabisa.
Alikuwa Golikipa huyu dogo, namkumbuka hadi Leo, alikufa juu ya fomu nje ya ofisi ya waalimu, walikataa kumpa ruhusa. Then wakafoji foji na kusema kafa na malaria.
 
Uhuni tu wa MOB PSYCHOLOGY....

Maisha ni zaidi ya upumbavu wa kimakundi.....
 
Kimata kinatuka ilikua O level na A level. 2008 ilikua ya viongozi na wanafunzi (Mussa Mdee unamkumbuka?). Ya shabani ndo ilifanya tukatembea mpaka kwa mkuu wa mkoa
Daa huyu Mussa Mdee sitakaa nisahau kipindi hicho niko form one 2007. Alikua anatuamsha saa 11 tudeki baraza alafu unalinda mtu asipite mpaka saa 1. Hapo utoke ndo ukajiandae kuingia class. Ni zaidi ya jeshi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha tunarudi kwenye midahalo ya co education is better than single sex education. Sitasahau hizi balehe. Tulikaa muda mrefu sana shule. Hiyo wiki tuko mabwenini akicheka huyu anapokea huyu. Yaan hamna sabaabu. Watu mabwenini ni vicheko tu aisee.. nilikua kiongozi wa chakula. Niliona kwa macho yangu mafuta ya taa yakimiminiwa kwenye makande[emoji23][emoji23][emoji706]
Nilichofanya niliagiza kiepe nje ya shule. Watu kula wakalisikia hilo wese. Wacha walalamike. After a week ikaonekana jambo halijaisha ikabidi wadanganye kwamba hakuna chakula shule imeshindwa kulisha wanafunzi hivyo imefungwaaa.... weuweee mabasi kesho yake haya hapaa[emoji23][emoji23] kuna ticha wa kiume akanambia mkakunwe salama mkirudi tusisikie tena vicheko vya hovyo
Sasa sahivi shule za girls sio kicheko, ni ku "daggy" yaan kushake miguu, ila nyege mbaya sana daaah. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nikikumbuka ni ujinga tu,Tambaza vs Azania....tukapigwa suspension mwaka mzima wa mwaka uliofuata tukaripoti shule za bweni tena za huko mbali kabisa,vijana kibao walishindwa kuendelea na shule,maana shule za karibu zote zilikatazwa kupokea wanafunzi kutoka Tambaza..
Funza alikuja Nsumba
 
Nikikumbuka ni ujinga tu,Tambaza vs Azania....tukapigwa suspension mwaka mzima wa mwaka uliofuata tukaripoti shule za bweni tena za huko mbali kabisa,vijana kibao walishindwa kuendelea na shule,maana shule za karibu zote zilikatazwa kupokea wanafunzi kutoka Tambaza..
Nakumbuka wengine walikuja Mazengo Dom
 
Mzee nipe historia fupi yamtu mmoja anaitwa MAN PEACE, huyu jamaa aliondoka baada ya hiyo vita akahamia shule ya nyerere nako alianzisha mgomo, lakin sijajua huyo jamaa katika hiyo vita alikuwa ni nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu mwanafunzi wa lyamungo kufa mlilishwa matango pori,ni mwanafunzi wa umbwe tu aliyeshambuliwa kwa mawe na matofali.
 
Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache

Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.

Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.

Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.

Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.

12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.

May the Lord grant us his Mercy.

Huwa napenda ku-reference hii ishu na nyimbo ya Dr Dre ft Snoop Dogg - Lil ghetto boy

Kuna vijana wa Lyamungo walihamia hostel zetu(Majengo Sec.) kwa mawiki kadhaa kwasababu ya hizo vurugu
 
Nakumbuka mnyukano kati ya Azaboy vs Benjamini.
Akikatiza mwanafunzi wa kibasila na jezi zake kama hana kitambulisho anajumuishwa kwenye vita na wao wakikamata na mwanafunzi wa veta wanamshuhulikia.
Azaboy tukaletewa wanawake formfive 2001 lakini walipomqaliza form 6 hawakuletwa wengine tena
 
Back
Top Bottom