sitaki kukumbuka nyakati zile, hasa maiv ya yule mama na sauti ya mkuu wa wilaya akitangaza kifo cha mshkaji alisema hivi, 'mtoto akililia wembe mpe ajikate, vijana mmeenda kuchezea wembe mmejikata mmempoteza mwenzenu kwa upumbavu wenu' RPC utawaletea maiti ya mwenzao waje waione kabla ya mazishi yake' aisee ni bahati familia iliona si busara, nyakati zote mwili ulikua kama umepata ganzi hivi.
.
.
miaka michache imepita sasa nimegundua mwanaume akikaa mwenyewe kwa muda mrefu anakua na hasira za ajabu sana, dogo aliefariki alipigwa na slesha iliyonolewa kama jambia.. huku wa lyamungo amechinjwa kwa seng'enge.
.
.
kisa uhasama ambao tumeukuta toka kitambo, pale nahisi umachame na ukibosho umo ndani ya zile shule, umbwe tuliona ufahari sana kukuta viti vya shule ya lyamungo tumeviiba na tunavisomea.
.
.
mkuu wa wilaya akasema nimeskia skia kuna viti vinasababisha haya sasa WANAUME LETENI KITI KIMOJA TUWAKABIDHI KAMA ALAMA YA USULUHISHI, likapikwa pilau shule tule na lyamungo, wakaja viongoz wa lyamungo wadau wanataka watie sumu kwenye chakula, mara wawafungie ndani ya darasa wapige ambush,
.
.
unapigwa wimbo wa shule mtu anaimba kwa hisia, kama vile anaitetea nchi yake!
.
.
Mr financial asante kwa kumbukumbu, apumzike kwa Amani mwana Umbwe mwenzetu na Mwanalyamungo, Mola atusamehe kwa dhambi zile, ilikua ni mbaya sana yale mambo!