Tatizo idadi ya wanafunzi, wakati tunasoma Kuna wanafunzi kama 2000, munalala wanafunzi wawili kitanda cha futi 2 na nusu, matundu ya vyoo hata 10 hayafiki Maputo huko. Kula chakula vurugu, prepo vurugu, darasani vurugu, kwenye mpira vurugu, kila sehemu vurugu.
Vyoo vya mabweni vya kisasa vina space unakuta vimefungwa na wababe wanaishi huko, Dorm leader na marafiki zake.
Just imagine mamia ya wanafunzi wanakaa kwenye bwalo la shule Wana Angalia Ngono, hizo guts wanazitoa wapi? Viongozi wenyewe wa shule wanachaguliwa kwa kuangalia nguvu na influence, wengi nguvu nyingi kichwani sifuri. Unakuta mtu ana miaka kama 20 ama 30 hivi yupo form 1, hajielewi hata kidogo.