Jitu katili lobilo k**m**ke ...dah huyu mjamaa sitakaa nimsahauLobilo, over
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jitu katili lobilo k**m**ke ...dah huyu mjamaa sitakaa nimsahauLobilo, over
Hizi shule mbili hizi zikikuwa hatari sana,yani wale wote waliosomaga hizi shule mbili mpaka Leo no wahuni tu na uzee wao.....miaka ya nyuma (1980 - 1990) kilikuwa na biff kali kati ya Kibohehe Sec na Kolila Sec. Ile ilidumu kwa muda mrefu, kwani ilikuwa hata mkikutana sehemu yoyote ni kipigana tu. Kibohehe chapa yao ilikuwa kuvaa Safari Boots na Kolila walitambulisha kwa kuvaa tasbihi shingoni.
Mo Town ilipata moto sana kwa ugomvi huo uliodumu kwa muda mrefu.
Jamani Shule za Boarding za Enzi hizo ilikuwa Raha Sana. Shule zenyewe zilikamilika. Mzungu alisema na tujenge Shule na ikajengwa Shule kweli. Mabweni Safi, Dining hall yenye kila kitu, Kitchen, Classrooms, Conference room, Chapel, Laboratory, infirmary, viwanja vya Michezo, Gardens, Staff rooms, Headmistress/ headteacher room, library, store, toilets and bathrooms zenye showers na flash toilets, fire place darasani Eneo la baridi, vioo vya Lucas au vya kufunga na kufungua, Sewage System Bora kabisa. Daaah nazikumbuka hizo Shule chozi hunitoka zilivyoharibiwa na Sisi.Lyamungo walishawahi kuleta noma shuleni kwao kisa wamepikiwa ugali siku ya wali viongozi wa vurugu wakafukuzwa kisa wali
Manase😂😂😂😂😂popote ulipo agiza bia gharama juu yanguManase huyo, anarusha ugali mita kadhaa usipodaka imekula kwako
pale walipo choma Bibiliaa [emoji16]Naikumbuka KIBITI.... Hizi shule dahhhh
Mkuu hapa kulikuwa na ka likikzo kama wiki 2 hivi sisi wa mbali na wengine ambao hawataki kwenda home tukabaki, sheria ikapitishwa kuwa ili ule lazima uwe umefanya kazi ya kusomba kuni na huko huko kazini mwalimu na viranja wanoko wanakupa kuponi ambayo ndo tiketi yako ya kuingia jikoni, hatujakaa sawa Headmaster Sanga akatangaza kuwa kipindi chote hicho cha likizo hamna kula wali! Vijana tukaona miyeyusho usiku mapema sana tukaenda kwa headmaster tukamsaidia kushusha vioo vya nyumba yake chini! Kesho yake defender kama 3 na FFU waliovalia zana zao wakatupa nusu saa ya kuondoka na hawakutaka hata mtu aache kivuli chake! Kwakweli mm sikwenda kwetu maana nlipiga hesabu ya 120k kwenda na kurudi nikaenda kwa mshikaji wangu kule Uchira tukapata dili la kupalilia mahindi heka moja 40k na kunyunyizia dawa, knapsack spray 1 tsh 3000, likizo ikaisha nikiwa don ila kwa sababu ya ujinga sikuchukua tahadhari wkt wa kupulizia dawa nikababuka mgongo wote! Nilirudi shule nikiwa na nido, sukari, blue band za kutosha room ilkuwa happy sana! Nilikuwa nakaa bweni la Aggrey[emoji1787][emoji1787]Lyamungo walishawahi kuleta noma shuleni kwao kisa wamepikiwa ugali siku ya wali viongozi wa vurugu wakafukuzwa kisa wali
Tuliosoma boarding school za serikali kulikuwa na raha yake sanaMkuu hapa kulikuwa na ka likikzo kama wiki 2 hivi sisi wa mbali na wengine ambao hawataki kwenda home tukabaki, sheria ikapitishwa kuwa ili ule lazima uwe umefanya kazi ya kusomba kuni na huko huko kazini mwalimu na viranja wanoko wanakupa kuponi ambayo ndo tiketi yako ya kuingia jikoni, hatujakaa sawa Headmaster Sanga akatangaza kuwa kipindi chote hicho cha likizo hamna kula wali! Vijana tukaona miyeyusho usiku mapema sana tukaenda kwa headmaster tukamsaidia kushusha vioo vya nyumba yake chini! Kesho yake defender kama 3 na FFU waliovalia zana zao wakatupa nusu saa ya kuondoka na hawakutaka hata mtu aache kivuli chake! Kwakweli mm sikwenda kwetu maana nlipiga hesabu ya 120k kwenda na kurudi nikaenda kwa mshikaji wangu kule Uchira tukapata dili la kupalilia mahindi heka moja 40k na kunyunyizia dawa, knapsack spray 1 tsh 3000, likizo ikaisha nikiwa don ila kwa sababu ya ujinga sikuchukua tahadhari wkt wa kupulizia dawa nikababuka mgongo wote! Nilirudi shule nikiwa na nido, sukari, blue band za kutosha room ilkuwa happy sana! Nilikuwa nakaa bweni la Aggrey[emoji1787][emoji1787]
Kweli kabisa Mkuu, shule kama Umbwe, lyamungo, Galanos etc ambazo nimewahi Fika ni shule za kisasa sana, hadi swimming pool ina heater. Ukuta ukiangalia tech yake huikuti mtaani.Jamani Shule za Boarding za Enzi hizo ilikuwa Raha Sana. Shule zenyewe zilikamilika. Mzungu alisema na tujenge Shule na ikajengwa Shule kweli. Mabweni Safi, Dining hall yenye kila kitu, Kitchen, Classrooms, Conference room, Chapel, Laboratory, infirmary, viwanja vya Michezo, Gardens, Staff rooms, Headmistress/ headteacher room, library, store, toilets and bathrooms zenye showers na flash toilets, fire place darasani Eneo la baridi, vioo vya Lucas au vya kufunga na kufungua, Sewage System Bora kabisa. Daaah nazikumbuka hizo Shule chozi hunitoka zilivyoharibiwa na Sisi.
Dahhh hiyo imekujaa baada pale hapajawahi poapale walipo choma Bibiliaa [emoji16]
Hawa wa Tambaza na Azania tulikutana nao Old Moshi miaka hiyo (siku hizi Moshi Sec) walimu wa kike walikuwaga wanaogopa kwenda kuwakagua usafi bwenini. Walikuwa wagumu na wasioogopa kitu chochote bangi nibangue. Hapo baada ya kizazi chao kuondoka ndipo tukaanza ugomvi binafsi na Umbwe kwenye kugombania mademu wa Kibosho Girls, Weruweru na Machame Girls...Mademu walikuwa wanatupenda sisi kwasababu tulikuwa tunapiga perfume na nguo za kisasa, Jamaa wa Ubwe walikuwa wanakunywa mbege sana na kuberi na hawajui kutongoza, walikuwa wanalazimishaNikikumbuka ni ujinga tu,Tambaza vs Azania....tukapigwa suspension mwaka mzima wa mwaka uliofuata tukaripoti shule za bweni tena za huko mbali kabisa,vijana kibao walishindwa kuendelea na shule,maana shule za karibu zote zilikatazwa kupokea wanafunzi kutoka Tambaza..
Ukiweka point ya kubebana kimehesabu inawezekana; Yale mabweni ya lyamungo cabin moja watu nane ambao hawajabebana, chukua 160 Mara nane nyingine ambao wababebwa jumla 900+ kwa bweni moja Mara nne inakuja elfu tatu na ushee ukoNakumbuka kidato Cha pili tulipiga pepa tupo Mia Saba na ushee.. kidato Cha Kwanza tumeanza na jamaa Wana umri wa miaka 25 /28 darasa letu pekee Lina mikondo mitano Cha ajabu zaidi mabweni yalikua manne tu yenye uwezo wakubeba wanafunzi 160 tu kwakila bweni .
Mkuu uzi wa masikitiko kweli, ungetuelezea polisi walichukua hatua gani?Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache
Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.
Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.
Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.
Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.
12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.
May the Lord grant us his Mercy.
Huwa napenda ku-reference hii ishu na nyimbo ya Dr Dre ft Snoop Dogg - Lil ghetto boy
Kuna ambavyo vilibaki na viko tofauti na viti vya umbwe
Umbwe walivyorudi kila mtu aliendelea na shughuli yake kama hakijatokea kitu polis walivyokuja walikua surprise sanaMkuu uzi wa masikitiko kweli, ungetuelezea polisi walichukua hatua gani?
Lyamungo ni machame, umbwe ni kibosho ule mto kombo ndo unaotenganishaMachame inatenganishwa na mto. Hivo kwa ninavojua mimi lyamungo ipo kibosho machame ni mpaka uvuke mto uliopo chin ya lyamungo kutoka kijiweni so sidhani kama lyamungo ipo machame